Kila nikipika wali nakosea

Kila nikipika wali nakosea

hiyo rice cooker itabidi niitafute asante mkuu
elfu 65 tu kariakoo nunua westpoint nipo nayo mwaka wa tatu sasa haina problemu ukishanunua niambie nikuelekeze jinsi ya kupika wali mzuri huko
 
Inaonekana wewe ni Mnyarwanda maanake Wanyaru kwa mapishi ni sifuri sasa akikupikia wali utatamani ule ugali, akikupikia pilau bora unywe uji sio siri hawajui kupika kabisaaa..

N.B maelezo ya kingast yamejitoshleza sio lazima uwe na rice cooker kwa mapishi bora ni ubunifu. na sio lazima uwe na sufuria hata chungu chafaa tena wa chungu we!!
 
Wali kwenye chungu?! Ama kweli kuishi ni kujifunza. Unaugeuzaje na chungu chaoshwaje?

weka maji kwenye chungu bandika jikoni yakichemka kata majani upana wa chungu weka ndan ya chungu yanazuia wali kuungulia. Weka mchele kwenye maji koroga. Maj yakikaukia chukua jan la mgomba weka juu ( husaidia ku2nza mvuke na kuzuia wali kuungulia na moto ulopalia) ukifuatia mfuniko kisha palia.
 
Katika upishi wa wali kitu kikubwa ni kujua ujazo wa maji,kama ni mpikaji ukipika kama mara mbili utakuwa umeshajua kipimo cha maji na mchele,baado ya hapo ni kama unamsukuma mlevi,ila kama ni wali wa nazi hapo napo kuna mambo ya ziada na kama pia ni pilau au biriano au mseto hapo napo kuna ya ziada,lakini kama ni huu tu wali wa maji basi ni timing ya maji Vs mchele
 
Back
Top Bottom