Kila nikishusha Bei dhidi ya washindani wangu nao hushusha Zaidi yangu, nifanye nini kuongeza mauzo?

Usishushe sababu wengine wameshusha..., shusha kama tu bado unapata faida...,

Kama vipi achana na hio Biashara unless bado faida ipo (sababu kama kuna faida hata kama ni ndogo ni bora kuliko kutokuipata hio faida); lakini kumbuka kuweka gharama ya muda wako sababu kama unakaa unapigwa vumbi asubuhi mpaka jioni; january mpaka december kwa faida ambayo huenda ungeweza kuipata kwa kufanya kingine kwa miezi sita bora kafanye kingine.
 
Wengi wanatoa ushauri bila kuelewa biashara ya duka la jumla. Ngoja nitoe mwazo yangu kuhusu hii biashara kidogo.

Mosi, hii biashara kama una mtaji mdogo basi inatakiwa utafute sehemu ambayo utakuwa mbali na wenye mtaji mkubwa maana wao wanachukua mzigo mkubwa na huwa wanapata kamisheni wakimaliza ule mzigo. Kwahiyo anakuwa analenga faida ndogo ili auze haraka ili apate kamisheni.

Pili, inatakiwa uwe unafanya delivery bure kwa wateja wako, hii itasaidia sana kwa wale wateja wavivu ambao hawapendi kuzunguka yani wanapiga simu unawapelekea mzigo.

Biashara ya jumla ni biashara kichaa inayoumiza sana kichwa kama upo sehemu yenye ushindani halafu una mtaji mdogo
 
Nawaza labda kuuza bidhaa amabayo nchini haizalishwi au niagize bidhaa nje ya nchi ua nianze biashara yakuimport ktk bidhaa yoyote ile
Biashara ya kuimport unatakiwa uwe na mtaji kwelikweli (ila wewe jamaa nahisi unampunga mrefu sana, unawaza kuimport!)
Kuagiza kontena la futi 40 au futi 20 kutoka nje mpaka ufikishe tz , upitishe bandarini sio kazi ndogo.....fanya utafiti wa kina mno.
 
Wengi wanatoa ushauri bila kuelewa biashara ya duka la jumla. Ngoja nitoe mwazo yangu kuhusu hii biashara kidogo.

Mosi, hii biashara kama una mtaji mdogo basi inatakiwa utafute sehemu ambayo utakuwa mbali na wenye mtaji mkubwa maana wao wanachukua mzigo mkubwa na huwa wanapata kamisheni wakimaliza ule mzigo. Kwahiyo anakuwa analenga faida ndogo ili auze haraka ili apate kamisheni.

Pili, inatakiwa uwe unafanya delivery bure kwa wateja wako, hii itasaidia sana kwa wale wateja wavivu ambao hawapendi kuzunguka yani wanapiga simu unawapelekea mzigo.

Biashara ya jumla ni biashara kichaa inayoumiza sana kichwa kama upo sehemu yenye ushindani halafu una mtaji mdogo
Mkuu umesema sahihi kabisa..mim nafanya delivery bule..Ila Kama ulivosema naungana naww kuwa biashara ya jumla nibiashara kichaa manaa kila siku inaumiza kichwa hasa ukiwa ktk eneo lawenye mitaji mikubwa Zaid yako
 
Biashara ya kuimport unatakiwa uwe na mtaji kwelikweli (ila wewe jamaa nahisi unampunga mrefu sana, unawaza kuimport!)
Kuagiza kontena la futi 40 au futi 20 kutoka nje mpaka ufikishe tz , upitishe bandarini sio kazi ndogo.....fanya utafiti wa kina mno.
Sina uwezo wakuagiza kontena hata ka futi 20 siwezi Ila kamataji naweza gawa nkaagiza loose cargo uku nakomaa na hii ya jumla kusomachezo
 
Habar wakuu nimekuja kwenu kutaka fikra namawazo..Niko ktkt biashara ya duka la jumla lavyakula kwamuda Sasa changamoto iliyopo kila mshindani wangu analenga kushika wateja soko kwakushusha Bei chini Zaid nami nimekua nikishuka nao..Sasa Basi Hali hii imepelekea kuzid kukupunguza faida ktk kila bidhaa matokeo yake unajikuta ktk bidhaa unayoiuza 56000 unabakiwa nafaid200
Naukisema ubaki nabei juu tofaut nawashindani wako Basi wateja wengi hukimbilia kwa wenye Bei ndogo Zaid maana soko nidogo wateja niwale wale mnafanya kugawana wateja kwambinu yakushusha Bei..wakuu nin nifanye nitoboe maana nawaza mbinu nyingi Zina feli
Japo mimi siyo mtaalamu kwenye mambo hayo ila ningekushauri na wewe bidhaa zako tafuta supplier ambaye atakuuzia kwa bei ndogo, yaani jaribu kupata bidhaa zako kwa bei ndogo
 
Mkuu bidhaa tunanunua viwanda vya humu humu ndani sio kwamasupllier
 
Habar wakuu nimekuja kwenu kutaka fikra namawazo..Niko ktkt biashara ya duka la jumla lavyakula kwamuda Sasa changamoto iliyopo kila mshindani wangu analenga kushika wateja soko kwakushusha Bei chini Zaid nami nimekua nikishuka nao..Sasa Basi Hali hii imepelekea kuzid kukupunguza faida ktk kila bidhaa matokeo yake unajikuta ktk bidhaa unayoiuza 56000 unabakiwa nafaid200
Naukisema ubaki nabei juu tofaut nawashindani wako Basi wateja wengi hukimbilia kwa wenye Bei ndogo Zaid maana soko nidogo wateja niwale wale mnafanya kugawana wateja kwambinu yakushusha Bei..wakuu nin nifanye nitoboe maana nawaza mbinu nyingi Zina feli
LABDA NYOTA YAKO IMEFIFIA MKUU, KAISAFISHE
 
jaribu kuwa spy uwapeleleze washindani wako ujue wanapata wapi iyo jeuri ya kushusha bei ikiwa mnaagiza mzigo sehemu moja . kuna wafanyabiashara wa nguvu mpaka wanaweza kumpangia supplier nini cha kufanya
 
Boresha ubora wa huduma yako na quality ya bidhaa zako plus Good customer care then usishushe sana bei yako hyo sio solutions hasa kwa wabongo tunaopenda duplication ya vitu Matokeo ni kuua soko
 
Mkuu auboreshe vipi mchele na maharagwe
Anunue mchele mzuri na asichakachue huo mchele maana wengi waweza sema mchele original wa mbeya kumbe ni fake hauna quality wamepaka tu mafuta ukienda kupika utajua hujui.
Pia waweza badili location ya eneo Hilo ka wafanyabiashara wamekuwa wengi huku demand ndogo
 
Hii mbinu nimeitumia Sana kwenye biashara yangu kariakoo, kulikuwa na mchina anasumbua soko nikaamua kwenda nae kiroho kutu, akipunguza 1000 kwenye item moja mm napunguza 1500.
Ndani ya miezi mitatu akanyoosha mikono akaacha hiyo biashara, hapo sasa nikapandisha bei kadiri navyotaka.
Hao jirani zako wanakupeleka puta ukishachemka wanarudi kwenye bei ya kawaida
 
Mkuu Kama hutojali kariakoo ulikua unafanya biashara gani
 
Kwa lugha nyingine ibrand biashara yako badala ya kuendelea kupunguza bidhaa

Ktk biashara unachopaswa kufanya ni kucheza na saikolojia ya mteja Tu..

mfano wewe na mshindani wako wote mnauz mchele wa kyela kilo ni TSH 1500/=,mwenzio akapunguza bei akauza 1200/= wewe badala ya kuuza elfu Mia mbili km yeye badala yake pima kilo yako weka kwenye package mzuri kuliko mfuko(kifaa) aliikuja nao.custimer care pia ni kipengere muhimu sn..hapo utamfanya mteja ajiskie vizuri sn
Kwel nmeamin watu weng bado hawajaishtukia biashara hapa bongo.

Aliekwambia mbongo wa kawaida anapenda package nzur...tena wabongo wakiona unaremba sana ndo hawaji..wanaataka vitu vya kumwagwa barabaran..utakuta magar yanajaa hapo wateja kibao...mbongo akiona unaremba sana saikolojia yake inamtuma kuwa hapo ni gharama kubwa...chunguza hili mkuu utapata jibu..sehem zenye mbwembwe nying ukiondoa ma baa au gest etc..wabongo wanakimbia
 
Back
Top Bottom