Kila ninapokuwa watu wananikodolea macho

Kila ninapokuwa watu wananikodolea macho

Kwa kweli una tatizo kidogo la kisaikolojia linalokufanya ujihisi hauko sawa Kama unavyostahili, pili waweza kuwa na nyota ya mvuto, tatu waweza ukawa una mwonekano fulan ivi wa kuvutia wengi, ila kama hadi watoto wanakushangaa basi hio ni nyota ya mwonekano Kama nilivosema hapo juu, nne pengine una hali Fulani znazowaachia watu mawazo hasi vichwani mwao ndio maana wanakushangaa mfano hali ya kunuka kikwapa, jasho, mdomo, na miguu Tano acha kushangaa pia watu sita Kama una tabia ya kujichua acha haraka hupelekea vijana wengi kutojiamin Saba Kama wewe ni handsome be cool magonjwa ni meng na usijiite kuwa mziri hakuna mwanaume anayejisema kuwa ni mzur hata Kama kweli ni handsome kwasababu hizo sio tabia za kiume nane Fanya utafiti kugundua zaidi nin sabab
 
Wakuu wa baraza heshima kwenu,

Kila ninapokuwa watu wananikodolea macho kupita kiasi. Niwe mitaani, barabarani, sokoni au sehemu yoyote watu wananishangaa bila kujua nini sababu. Watoto, wazee, watu wa rika langu, watu wazima na wa jinsia zote wamekuwa wakinikodolea macho sana. Wengine wanakodoa kwa kujificha na wengine waziwazi.

Nashtushwa na hiyo hali cause nikipita sehemu na kuwa kama mzimu uliofufukia kwenye mtaa uliozikwa kutokana na jinsi wanavyonishangaa. Sometimes inanilazimu kuingia chimbo kujikagua kama zipu ipo sawasawa au ndege ameninyea bila kujua ila najikuta nipo sawa. Nimevumilia ila nikaona si vibaya kuja kuuliza nini sababu ya watu kuwashangaa watu wengine pindi wawapo kwenye mishe mishe zao? Kama umewahi kumkodolea macho mtu mwingine sababu inakuwa ni kitu gani?

Asanteni!
Hahaha
 
Back
Top Bottom