Kila nkifanya ubunifu mshindani wangu anaiga ,wote tuko na aina moja ya biashara vinywaji na vyakula

Kila nkifanya ubunifu mshindani wangu anaiga ,wote tuko na aina moja ya biashara vinywaji na vyakula

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habar wakuu leteni uzoefu wenu,Niko katika biashara ya vinywaji na chakula kwamiaka Sasa ,mshidani wangu yuko mita50 tuko ofisi yangu, Sasa Kila nkifanya ubunifu wakibiashara basi ataiga,nkiigiza product mpya sokoni basi nae ataiga na ataipunguza Bei
Nini chakufanya biashara imekua pasua kichwa Kila ubunifu utakao uweka washindani wote wataiga
 
Usijali mshindani anafanya Nini wewe dili na biashara yako....
Na kama unaboresha au kuingiza bidhaa mpya ufanye hivyo kwa kuendana na soko la hapo ulipo kwa maana wateja usifanye mashindano au kufuata jirani kafanya Nini.
Ipambanue biashara yako weka juhudi, uvumilivu utayashinda yote.... Biashara zote ni pasua kichwa vumilia tu!
 
Wa

Wateja nao wananunua kiukabila
 
Fanya mpango kama unauza bidhaa then agizia stock mbali sana na hakikisha inakuwa nzuri kisha uza kwa bei ya chini hadi aombe poo.

Ukitaka kujua unafanya vizuri eneo la biashara ni pale utapoona wanaokuzunguka wanakuiga au wanaanza kuja kuwanga ofisini kwako jua hapo unapatia kisawa sawa usiondoke ongeza balaa hadi wakimbie wao.
 
Vp kwa upande wa mambo ya kiroho upo vzuri mkuu? Kama unamuamini MUNGU bs hakiksha kweli unasmama vema eneo hlo toa sadaka, toa fungu la 10, saidia inapobidi, acha uzinzi, matusi, woga na hofu, acha uwongo nk. kama unaamin waganga komaa nao bt skushauri sn hao maana ipo sku wataomba kafara ya family yako itaanza kuku, mbuzi, ng`ombe ksha bnadamu.
 
Wapo wanaoiga na hawaridhiki wanakuja kuuliza unanunua wapi, wanakushawishi uuze bei sawa na wao ili mugawane wateja wako.
Imetokea hii juzi tu.
 
Fanya mpango kama unauza bidhaa then agizia stock mbali sana na hakikisha inakuwa nzuri kisha uza kwa bei ya chini hadi aombe poo.

Ukitaka kujua unafanya vizuri eneo la biashara ni pale utapoona wanaokuzunguka wanakuiga au wanaanza kuja kuwanga ofisini kwako jua hapo unapatia kisawa sawa usiondoke ongeza balaa hadi wakimbie wao.
Yaani kuna binadamu ni mabingwa wa kuiga kwa weli.
 
Kama uko sehemu nzuri,

Pendezesha mazingira, then toa huduma nzuri, mteja akija asuuzike lastly pandisha bei.

Utapata wateja wachache na wakueleweka

Kwenye wateja wachache na wakueleweka utapata faida kubwa as running cost itapungua
 
Back
Top Bottom