Shida hapo inakuja anaipunguza Bei hiyo bidhaa ili avute wateja nawateja nao wanahamia kwake kufuata Bei ndogo
Kama anapunguza Bei Ina maana hiyo bidhaa kaipunguza bei na kiwandani kaipunguza ubora...
Wewe tulia uza bidhaa yako bila papara na uhakikishe ubora wa bidhaa yako uko pale pale!!!! Unaona energy ya Azam iko juu kwa bei na ubora kwa hapa Tanzania na hana mpinzani kwa soko la ndani japo mie sio mtaalamu lakini sababu kuu mojawapo itakua ni ubora!!!!
Hapo unateseka na ushindani na inaonekana wewe ni mtu yule unaumizwa kwenye harakati za ushindani,,, buni mbinu mbalimbali za kuuza hiyo bidhaa yako hakikisha sehemu uliyopo unafatilia harusi zote na misiba ukisikia harusi jiingize kwenye kamati ikifika muda wa vinywaji lazima utapata tenda,, siku hizi misiba iko tofauti watu wanalia na vinywaji na hela zao ukisikia vilio unasogea unasoma mazingira ukielewa beba vinywaji vyako,, viwanja vya mpira tafuta taarifa na habari kuhusu ligi kuanzia ligi kuu ,,ligi daraja la kwanza huko watu wanakula Bata na kina vibe wanajiachia mechi za basketball ball huko kote unaweza uza huku ukiendelea na biashara yako maana huko hayazidi masaa mawili...
Hakikisha upande wa masoko uwe na alternative Tena upande wa vinywaji hautesi unaweza kuuza hata kwenye mikutano ya hadhara....
Nikupe mfano wangu labda utakusaidia.
Nilianza kuuza solar ,tv , radio, sabufa pamoja na spare zake sokoni nilikutana na ushindani mkali wa bei, kujuana, kuchongeana tra, na uchawi juu yake. Tanzania hii nimeizinguka kidogo nikawaza uhitaji ni mkubwa vijijini na wanafika Bei kuliko mjini!!! Nilianza kupeleka bidhaa zangu maporini na vijijini huko nilisambaza mfulilizo miaka minne matokeo yake niliyopata mwaka wa sita ninavyoongea hapa huko maporini Nina jina na napokea oda inayokuja na hela cash ikifika msimu wa mauzo kwangu unakuta foleni kama ya bank wale washindani wananiita mtoto mchawi sana yule.... Na duka langu sasa hivi limekua la kuuza kwa oda zaidi yanii mwendo wa kutuma mizigo..
Kaa chini tafakari kama hiyo biashara unaipenda usiikatie tamaa Wala usimuwaze mpinzani wako!!! Tengeneza njia zako za kupata wateja na jipe muda utatoboa.