Kila Rais angekopa kama Hayati Magufuli, leo hii tungekuwa tunakopesheka na Magufuli angekopa wapi?

Kila Rais angekopa kama Hayati Magufuli, leo hii tungekuwa tunakopesheka na Magufuli angekopa wapi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Taarifa tunazosima zinaonyesha ndani ya miaka mitano tu Magufuli amekopa karibu sawa na mikopo aliyochukua Kikwete kwa miaka yote Kumi aliyokuwa madarakani.

Ukiacha Kikwete, kuna Mkapa, Mwinyi na Nyerere na hawa nao walikopa na kuna wakati walifanya juhudi tusamehewe madeni

Sasa najiuliza, kama na hawa maraisi waliopita wangekopa kwa speed ya Magufuli na kutofanya juhudi za sisi kusamehewa madeni, nchi hii leo hii ingekuwa inakopesheka?

Kama nchi ingekuwa haikopesheki, Magufuli angekopa wapi?

Na je, mikopo aliyochukua Magufuli, haipunguzi wigo wa kukopa kwa maraisi wataomfuatia hasa Mama Samia?

Mama Samia nae akiamua kukopa kama Magufuli ili afanye mambo mengi makubwa ndani ya muda mfupi, mzigo wa madeni nchi hii utakuwaje?

Majibu nawaachia wenyewe., leo naenda kuosha vyombo mwenyewe.
 
doner country si rahisi kupoteza uwezo wa kukopesheka na hata ikipoteza huo uwezo bado ina mali nyingo sana zakuweka bondi.
 
Kwa nini chadema wamekuwa ombaomba kipindi hiki cha Rais Samia.

Mbowe anapita mtaa kwa mtaa kuomba
 
Kwa nini chadema wamekuwa ombaomba kipindi hiki cha Rais Samia.

Mbowe anapita mtaa kwa mtaa kuomba
Mbona nyie kwa zaidi ya nusu karne mnaendesha nchi kwa kutembeza bakuli?
 
Back
Top Bottom