Kila siku anahitaji Penzi jipya imekaaje hii

Kila siku anahitaji Penzi jipya imekaaje hii

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
16,789
Reaction score
5,401
Ni Binti wa miaka 26-27 siku zote ananishangaza na mienendo yake
Nadhani akikaa sana B/f haizidi 2 years hapo kajitahidi sana.kishafanya engagement zaidi ya 3 zote anawaacha wachumba.
Nilijaribu kumdadisi kwa nini anadai eti huwa anawachoka wanaume hajisikii kabisa kukaa na mwanamme muda mrefu..na akizidisha mwaka anakuwa kwenye mahusiano asiyoyapenda hata kidogo anaboreka ,anakosa amani na hatamani kumuona huyo mtu..
Yuko tayari kutafuta sababu ili aachane na boyfriend aliye naye ili atafute B/F mpya.
**Asaidiweje binti huyu**

Mie binafsi naona kama anashindwa kuelewa mwili wake ni wa thamani sio kila mtu anayekuja usoni kwake anastahili kupewa penzi...:A S 39:
..
 
Huyo ni lazima ana pepo wa ngono au wa pesa, pls naomba details zake kwani kuna mmoja nilikuwa nae na the way ulivoandika haka ka thread kama vile ni yeye, alinitosa bila sababu na mimi nilidhamiria kabisa kumuoa wakati tuko mwaka wa nne pale mlimani... Nashukuru kwamba leo siko nae but later nilisikia almost the same story ni hii unayoiandika hapa leo.

She needs prayers
 
Mi nimempenda sana huyo dada. Unajua amekuwa mkweli na hapendi kuikwaza nafsi yake wala ya huyo mpenzi au wapenzi wake. Hii hali ipo sana katika mahusiano mengi kuanzia kwa marafiki tu (boy/girl friends) hadi kwa walioko kwenye ndoa. Si wote walioko kwenye mahusiano wanafurahia ila tu ni aidha wanaamua kubaki humo ili jamii isiwashangae au kuna wale wanabaki kwa ajili ya vitu fulani kama vile fedha na mali nyinginezo au wengi wao utasikia kwa ajili ya watoto na mazoea kuwa huyu nimemzoea sana. Kwa hiyo huyo dada wala tusimlaumu na wala usihoji thamani ya mwili wake. Kama utakuwa unang'ang'ania kuangalia thamani ya mwili wako wakati roho na moyo wako unavurugwa wala haina maana.
 
Thanx Lord sio wewe FL1.....tungekua na marais wangapi sijui...
 
Huyo anahitaji moja ya vitu vifuatavyo:

1) Ushauri wa kisaikolojia
2) Maombi

Watu wenye tabia hizi wapo wengi. Huyu ndio mwanamke wa kwanza kusikia ana hii tabia. Ila nina rafiki zangu kadhaa (wa kiume) ambao wakilala na msichana mara mbili, basi hawataki tena kuwaona. Wanatafuta kila aina ya sababu wavunje uhusiano.
 
mmh i nzitooooooo!!!!!!!!!1
she is libearal theoritically n practicalyyyyyyyy dah kweli!!!!!!!!!!!!
bt ajue tu mwili wake ni hekalu la roho mtakatifu!!!!
wengi wamo katika ili sema tu hawajisemi
 
Mtoto akilila wembe...???mungu amponye tu na magonjwa na majanga!!!
 
Thanx Lord sio wewe FL1.....tungekua na marais wangapi sijui...

ha ha ha naona unanichokoza mapema asubuhi :confused2:
sio mie bwana ... ila najiuliza maisha ya binti huyu yataendelea hivi mpaka lini?
 
Mi nimempenda sana huyo dada. Unajua amekuwa mkweli na hapendi kuikwaza nafsi yake wala ya huyo mpenzi au wapenzi wake. Hii hali ipo sana katika mahusiano mengi kuanzia kwa marafiki tu (boy/girl friends) hadi kwa walioko kwenye ndoa. Si wote walioko kwenye mahusiano wanafurahia ila tu ni aidha wanaamua kubaki humo ili jamii isiwashangae au kuna wale wanabaki kwa ajili ya vitu fulani kama vile fedha na mali nyinginezo au wengi wao utasikia kwa ajili ya watoto na mazoea kuwa huyu nimemzoea sana. Kwa hiyo huyo dada wala tusimlaumu na wala usihoji thamani ya mwili wake. Kama utakuwa unang'ang'ania kuangalia thamani ya mwili wako wakati roho na moyo wako unavurugwa wala haina maana.

Hii post ni nzito lakini napenda nitofautiane na logic yako japo nakubaliana na yote yaliyoko kwenye nyekundu. Iliyoko kwenye blue imeniacha mdomo wazi.
Kama mwandishi ni mwanaume sitashangaa.Kama ni mwanamke nitashangaa kiasi changu.Nitatoa sababu zifuatazo:
1. Mahusiano siyo kitu cha kuchezea na hasa ukijua unacheza na moyo wako na wa mtu mwingine.Ninaamini kabisa kuwa back in the days, moja ya sababu zilizokuwa zinawafanya wazazi kuoza watoto wao hasa wa kike mapema ni kuwaepusha na hizo rusha roho wanazojipa hadi wanashindwa kudumu kwenye mahusiano.Mtu unajiweka kwenye mashaka mwenyewe pale unapoonja onja - utajichanganya sana hadi itakuwa vigumu kuwa na mtu. Utaona vimbwanga na vionjo vya kila aina na kila mmoja atakuwa na matamu na machungu yake, mazuri na mabaya yake... na utakuwa tayari umeshajiwekea benchmarks for comparison.
2. Hapo kwenye blue, maisha is not just about kujitafutia raha bila kujali wengine.Ingekuwa hivyo basi kungekuwa hakuna makatazo mbalimbali kimila,kidini, kisheria, kidesturi nk.
 
:focus:
Huyu binti kachelewa ku-mature kichwani....ata-mature siku moja, probably when she reaches 40....
BTW: FL1 zidi kumbusha kwamba Mr. Right hajazaliwa!
 
Kila afanyaye dhambi ni mtumwa wa hiyo dhambi, na dhambi unapoitenda unakwenda zako bila kukumbuka, ila utakujakuikumbuka siku pale mambo yakapokuwa magumu. Hebu soma

Nimekuja ee Bwana, mtumwa wako mdhambi, usinipeleke kwenye hukumu bwana, nilipoambiwa kusali nalisema nimechoka, nilipoambiwa kutoa zaka zaka, nilibakisha za pombe........ leo hivi sina kitu, leo hii ni mpweke, basi leo hii na wanizike, leo hii na wanivishe sanda nzuri na ya gharama, niko pweke na roho yangu kwenye kaburi, kweli asiyeona ubaya wa upofu, huuona akipofuka... Ukitaka article nzima PM me.
 
huyo bado sana!mwacheni aendelee ku-wanga huku na kule!....

pole yake atakaemuoa maanake atakuta hadi ile theory ya ELASTICITY imeshakuwa ''nullified''!atakutana na bwawa sijui kisima ai doo noo
 
hahaaaaaaaaaaaa lol Teamo acha uongo bana!! mwache binti afurahie maiha angali bado mbichi!!!
 
isipotumika inapotea ...si kuna such a theory in evolution jameni??
Teh hehe BHT!
Hii theory ya " you dont use it you loose it" inafaa tu pale uko kwenye pingu au husiano rasmi..siyo ukiwa huria kama huyu mdada!
 
Ni Binti wa miaka 26-27 siku zote ananishangaza na mienendo yake
Nadhani akikaa sana B/f haizidi 2 years hapo kajitahidi sana.kishafanya engagement zaidi ya 3 zote anawaacha wachumba.
Nilijaribu kumdadisi kwa nini anadai eti huwa anawachoka wanaume hajisikii kabisa kukaa na mwanamme muda mrefu..na akizidisha mwaka anakuwa kwenye mahusiano asiyoyapenda hata kidogo anaboreka ,anakosa amani na hatamani kumuona huyo mtu..
Yuko tayari kutafuta sababu ili aachane na boyfriend aliye naye ili atafute B/F mpya.
**Asaidiweje binti huyu**

Mie binafsi naona kama anashindwa kuelewa mwili wake ni wa thamani sio kila mtu anayekuja usoni kwake anastahili kupewa penzi...:A S 39:
..
Na hiyo tabia ya kudadisi wenzio umeanza lini? Tukianza kukudadisi na wewe utatoka salama?
 
Back
Top Bottom