Kwa sababu lugha yetu tunayoitumia ni Kiswahili, hakuna haja ya kujilazimisha kuongea Kiingereza wakati lugha hii ni tatizo kwako. Watu wengi hudhani kuongea kiingereza ni kielelezo cha ustaarabu (civilisation) na usomi - hii si kweli. Wazungu wakija hapa kwetu wanalazimika kuongea Kiswahili, japo wanachapia lakini hawana budi kukiongea sababu ndiyo lugha ya mawasiliano hapa kwetu. Sasa wewe mtanzania kwa nini ung'ang'anie kuongea Kiingereza broken hapa kwetu uswahilini?Ongea Kiingereza unapolazimika tu na katika mazingira yanayokihitaji, vinginevyo kama unalazimisha kuongea wakati hujui na hakuna ulazima lazima tukwambie tu kwamba unaongea broken English!