Kila siku naota nimeokota gunia la pesa

Wakuu tangu wiki iliyopita kila nikilala usiku naota nimeokota gunia la pesa, ila nikishtuka najikuta nimekumbatia pilow.

Je hizi ndoto zina maana gani?
kapime malaria sio bure hali ya uchumi ilivyombaya nani aangushe gunia la hela?
 
umasikini huo ndio unaokumbatia! iyo ni changa la macho pesa huja kwa kufanya kazi kwa bidii na akili usije ukawauwa ndugu zako!
 
Lovely!!!, japo huwa sielewi maneno kama haya hapa chini yanazoelekaje
  • Ndoo ya maji
  • Banda la kuku
  • Barabara ya lami
Ndoo yenye Maji

Banda la kuhifadhia Kuku

Barabara ya lami=Nafikiri hii ipo sawa tu,au unaweza kusema Barabara yenye kiwango cha Lami.
 
ukitaka kupata tafsiri sahihi ya ndoto igeuze iwe kinyume ndo uhalisia wake mfano ukiota harusi ujue kuna msiba..ukiota umefaulu ujue umeliwaa..ukiota upo kwenye harusi mnakula nyama ujue msiba utatokea muda si mrefuu believe me....pole sana mkuu najua imekuchoma lakini ukwel ndo huo unalo kakaa
 
....ongeza bidii ya kulala utatusua na kuishimaisha mazuri ndotoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…