BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Kwa Mwaka wa tatu sasa mtawalia sisi wakazi wa Makongo na Makongo Juu hadi Goba, barabara inayoenda hadi mzunguko wa GOBA CENTRE tumelalamika sana kwenu kwa barabara yetu kukosa daladala.
Ahadi zenu zote zimekuwa HEWA mpaka sasa.
Kila mara tunapopiga simu dawati lenu la HUDUMA KWA WATEJA wamekuwa na jibu kuwa "Tutawakilisha kero yenu kwa Viongozi", lakini hatujawahi kuona chochote kikifanyika.
Tumefikia mahali pa kuamini kuwa ninyi ni wanufaika wa biashara ya BAJAJI ambayo ndiyo inayotawala barabara ya SURVEY hadi GOBA CENTRE inayopitia MAKONGO na MAKONGO JUU.
Daladala za MAKONGO Juu zinazotoka MAKUMBUSHO ni za kuhesabu, na wakati mwingine ni zile zinazobadili route baada ya kuona abiria wamejaa na hakuna magari. Isitoshe, route yao huishia pale MAKONGO JUU na kuwaacha abiria wa kipande kilichobaki hadi kufikia Mzunguko wa GOBA ENTRE wakitafuta tena BAJAJI za kuwafikisha ma kwao.
Tulishawapa ushauri kuwa muanzishe route mpya za kutoka:
1. MADALE CENTRE KWENDA MAKUMBUSHO kupitia MAKONGO na MWENGE
2. MADALE CENTRE KWENDA GEREZANI KUPITIA MAKONGO JUU, SAMM NUJOMA, DARAJA LA KIJAZI, KISHA MOROGORO ROAD, MANZESE HADI GEREZANI
3. MADALE CENTRE HADI KAWE kupitia MAKONGO na MWENGE
Hamjataka kuchukua hatua yoyote ili BAJAJI zenu zisipungukiwe na biashara.
Sisi wakazi wa barabara ya MAKONGO tumekuwa wahanga wa BAJAJI za shilingi 1,000 hadi 3,000 kwa safari moja, na hapo ni usafiri wa kuunganishwa abiria wanne kwenye BAJAJI moja.
Pia soma ~ LATRA yatangaza njia mpya za Daladala ikiwemo ya kupitia Makongo Juu
LATRA hakuna hata mara moja wamejibu hoja, na hata ukiambiwa "tunaifanya kazi na tutakujulisha majibu" hakuna hata siku moja unayopigwa kupewa mrejesho.
Tunateseka sana kuwa na viongozi wasiojali shida za wananchi wao kama mlioko LATRA kwa sasa.
Hivi mna sababu yoyote ya kuendelea kuwepo hapo ofisini?