huyu anafaa kuwa mwanaume mkomavu mwenye kumiliki watoto wa jinsia zote ?????/[/QUOTE
Kumiliki watoto! m2 mbinafsi kwa mtizamo wangu hastahili kuwa na familia, nasema hivi kwa sababu nimeshuhudia mwanaume ambaye alikuwa mbinafsi na familia yake imesambaratika , baada ya mke kuvumilia na kushindwa aliamua kuachana, baba hakuwa anajali watoto wala mke hata baada ya kuachana bado aligoma kutoa matuzo ikiwamo ada kwa watoto wake mwenyewe hata pale alipoamuriwa na mahakama , matokeo watoto hawana mbele wala nyuma.
Kusema uongo ni rafiki wa karibu wa ubinafsi huwa vinakwenda pamoja, kwa mf hapo juu huyo jamaa aliidanganya mahakama juu ya hali yake ya kipato na mali ili tu asihudumie watoto tena kwa kutumia wakili ambaye alikuwa rafikie.
Ukatili ni rafiki pia wa ubinafsi ili m2 aweze kufanya jambo kwa uhuru wake binafsi anatafuta njia ya kujikinga ili asihojiwe juu ya uhalali wa kufanya hilo jambo, we unashindwa kuuliza jambo kwa sababu aidha utatukanwa au kupigwa, watoto wanahitaji upendo, kuenziwa na kujaliwa, mbinafsi hana muda huo.