Kila ukipima mkojo unaambiwa kwamba una U.T.I?

Kila ukipima mkojo unaambiwa kwamba una U.T.I?

Masondoka

New Member
Joined
Aug 26, 2024
Posts
1
Reaction score
3
FAHAMU ILI KWANZA:
Urinary Tract Infection (U.T.I) ni maambukizi ya vimelea vya maradhi kwenye mfumo wako wa mkojo. Vimelea hivyo vipo vya aina tofauti tofauti hata matibabu yani aina ya dawa na dozi yanaweza kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.

KITU CHA KUFANYA:
Je, Mara kwa Mara unaambiwa una U.T.I kwenye vipimo vyako vya mkojo na hata kama ukitumia dawa za kumeza au kuchoma sindano ukikaa kwa mda flani unaanza kusumbuliwa tena na unaporudi kupima unaambiwa una U.T.I tena?

USHAURI:
Kwanza acha kujikatia tamaa kwa kusema eti "Mimi nina U.T.I sugu", tambua kwamba hili tatizo linalo utatuzi wake na utapona kabisa.

Kwanza:
Acha kununua dawa na kutumia hovyo hovyo kwa kushawishiwa na mtu asiekua mtaalam wa afya. Mtaani kuna watu wengi ambao wanajifanya wanajua kila kitu. Tambua utumuaji holela wa hizo dawa ni hatari kwa afya yako ya ini na figo, pia unaweza kupata usugu wa dawa (drug resistance).

Pili:
Nenda hospitali kapime kipimo cha "culture and sensitivity" hichi kipimo kitakusaidia wewe na daktari wako kufaham aina ya Vimelea vinavyokusababishia U.T.I na dawa sahihi ya kukutibu.

Tatu:
Hakikisha unajizingatia usafi wa sehemu zako za siri, epuka kufanya mapenzi kiholela bila kinga au bila kupima H.I.V, U.T.I na magonjwa mengine ya zinaa. Nenda kakojoe mkojo na osha viungo vyako vya siri Mara tu unapomaliza kujamiiana, pendelea kula matunda kama matikiti maji na machungwa ikiwa hayakuletei shida ya kiafya.

# Nitapenda kujifunza kwako pia, asante.
 
Back
Top Bottom