Mkuu ni rahisi tu...
Unaweza kutazama/kustream tv yoyote kwa kupitia Kodi maadamu uwe na url path sahihi ya mahali server ilipo ya content uitakayo...
Binafsi nishaweka Azam 2 na Star TV muda kidogo na huwa nazitazama inapobidi...
Hiyo link uliyoiweka hapo juu inabidi kuiedit kidogo ili uweze kutazama Azam 2
Ili uweze kustream lazima link yako iwe katika mojawapo ya format zifuatazo.
http://host/path/stream
au
mms://host/path/stream
au
rstp://host/path/stream
1. Step ya kwanza:
Tengeneza text file ambayo ndani yake utaweka hii link hapa chini na uisave kwa extention ya .strm (nakushauri tumia notepad++).
Lipe jina lolote mathalani Azam Two.strm na lihifadhi mahali katika folder mathalani C:\Azamtv
rstp://196.41.40.253:1935/live/myStream/
2. Step ya pili:
Fungua XBMC/Kodi na katika main menu bofya VIDEOS, then bofya Files na tena bofya Add Videos
3. Step ya tatu:
Itatokea dialog box kwa ajili ya kuingiza directory ya lile file ulilolisave katika Step ya kwanza.
Katika sehemu iliyoandikwa , bofya hapo na kuandika directory ya mahali ulipohifadhi lile file la Azam.strm
Mfano: C\:Azamtv\ (Azamtv ni folder ambalo ndani yake ndio kuna Azam.strm) tafadhali kwepa kuandika C:\Azamtv\Azam.strm
4. Step ya nne:
Bonyeza OK, then bonyeza OK na hapo file la Azam.strm litaonekana limekuwa added katika playlist.
Ukilifungua AzamTwo itaoneka kama una connection ya internet isiyo na shaka
Mwisho