Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Mkuu hapa naona cjakuelewa vizuri, GB 100?, mbn me nkiweka bando ya GB 2 naangalia mechi 2 kwenye kodi, na tofauti ni ipi kati ya laptop na tv box zote ziwe connected in wireless network, ipi itavuta bando kwa fujo hapo?
ameuliza kwa mwezi hivyo mkadirie sasa hio gb 2 kwa mechi mbili kwa mwezi ataangalia mechi ngapi?

na quality zinatofautiana ukitaka quality kubwa zaidi na mb zinaenda zaidi.

tv box na laptop zitakula mb sawasawa ikiwa wote mnaangalia source moja
 
Mimi natumia link hii direct kwenye browser.
www.goatdee.net
Kwa 600 tu nacheki game 2 au 3 zaidi.
Yeah naipata hyo link, nmeitumia sana bt inategemea na ntwrk ilivy, ikiwa na rate ndogo unachek game 1 na na kipande tu cha game nyingn, ni mzuri sana hyo website, en kuna cricfree.sc.
 
ameuliza kwa mwezi hivyo mkadirie sasa hio gb 2 kwa mechi mbili kwa mwezi ataangalia mechi ngapi?

na quality zinatofautiana ukitaka quality kubwa zaidi na mb zinaenda zaidi.

tv box na laptop zitakula mb sawasawa ikiwa wote mnaangalia source moja
Huh ok mkuu, nlidhani ni kwa siku 1
 
Kwangu natumia simu(android)lakini ukiclick kwenye mechi haifunguki naomba maelekezo
 
Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.

Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.

Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.

Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ?

Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.

KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
Kodi-devices-smudged.jpg


Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi

Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
9vW4MHp.jpg


KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
zNbDtYR.jpg

PppArCw.jpg


Hio hapo juu sky sport 3

Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.

Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli

Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
kutokana na request nyingi za watu nita updates hapa mara kwa mara plugins ambazo zipo avtive

1.DNA TV
hii ipo active nimetest chanell kama BT sport na Sky sport zinafanya kazi vizuri tu. install toka hapa
Tutorial How to Install DNA TV for Kodi
ina tatizo la kuandika servel full sababu traffic ni kubwa hivyo ikiandika hivyo angalia chanell nyengine au endelea kuclick hadi ikubali.

pia kwenye repository yake kuna clone za IPTV stalker ila sijazitest.

2.PHOENIX TV
kama uli install phoenix kama .zip file pengine sasa hivi huoni kitu utahitajika kueka version mpya, tumia hii link
Tutorial How to Install Phoenix Kodi XBMC
nimetest chanell za movie na mpira zinafanya kazi

3.ISRAEL LIVE TV
sio mbaya ukiwa nayo kama backup kwenye chanell zake za sports kuna chanell za portugal huwa zinaonesha mpira japo quality si nzuri.

Tutorial How to Install IsraeLIVE Video Add-On Kodi
Kama una swali lolote usisite kuuliza chini

jinsi ya kuangalia mpira kwa kutumia acestream(torrent)
watu wanalalamika matatizo ya buffering kwenye plugin za bure kodi kuna njia nyengine nzuri ya kustream mpira ambayo unatumia p2p kama torrent vile ila kabla hujaamua kuitumia elewa mambo haya

1.uzuri wake
njia hii haitumii server hivyo hakuna overload kwamba mkiwa wengi iwe slow, badala yake mkiwa wengi yenyewe ndio inakuwa na speed sababu mnarushiana hiyo stream wenyewe kwa wenyewe. concept yake ni kama torrent unapodownload hapo hapo unam uploadia mwenzako
bittorrent.gif


hii acestream ina quality kubwa sana mara nyingi stream zake zinakuwa ni hd au full hd hivyo kama una flat tv au simu/laptop/tablet ambazo ni high end utaenjoy

2.ubaya wake
-inakula sana bundles inaweza kumaliza zaidi ya 1gb kwa match sababu unadownload na ku upload kwa wakati mmoja japo unaweza kuamua usiupload uwe una download tu
-mkiwa wachache inaweza kuwa slow

3. ombi, kama kuna mtu anafahamu source ya link za acestream ambazo sio hd kwa watu wasio na bundle kubwa atuekee kwa faida ya wengine.

jinsi ya kueka acestream
-download aceplayer (ni modified version ya vlc) toka hapa
Ace Stream

-link za mechi husiku utazipata siku ya mechi link hizi
http://www.livefootballol.me

chagua link ilioandikwa acestream na url yake lazima inaziwe na
acestream://

ukipata url yake fungua aceplayer yako then click file halafu stream then paste url halafu subiri kidogo itaplay
mimi naomba muongozo mfano wakujaza hapa
4c54330c4a66d9b2f23066877355fd35.jpg
 
mimi naomba muongozo mfano wakujaza hapa
4c54330c4a66d9b2f23066877355fd35.jpg
mkuu siwezi kujua unachokitaka sababu hata sijui ni picha ya nini hio

ila mara nyingi mediacentre ni kama plex kazi yake ni kukusanya media zote na kuzieka mahala pamoja.

mfano una desktop, simu, tablet etc kupitia mediacentre unaweza ukaplay vitu vya desktop kwenye simu au tv

unaweza chagua kifaa kimoja mfano hio simu iwe kama server ili kuweza kuhamisha baina ya kifaa na kifaa, na hapo ndio unaandika configuration sasa

-media centre name unaandika chochote
-adress ni url ya kupitishia mfano urlyako.com
-port mfano ni 80 au 8080 au 3128 au 443 etc
-password ndio neno siri lako
 
mkuu siwezi kujua unachokitaka sababu hata sijui ni picha ya nini hio

ila mara nyingi mediacentre ni kama plex kazi yake ni kukusanya media zote na kuzieka mahala pamoja.

mfano una desktop, simu, tablet etc kupitia mediacentre unaweza ukaplay vitu vya desktop kwenye simu au tv

unaweza chagua kifaa kimoja mfano hio simu iwe kama server ili kuweza kuhamisha baina ya kifaa na kifaa, na hapo ndio unaandika configuration sasa

-media centre name unaandika chochote
-adress ni url ya kupitishia mfano urlyako.com
-port mfano ni 80 au 8080 au 3128 au 443 etc
-password ndio neno siri lako
asante ngoja nijaribu
 
Wataalamu kuna update imetoka ya kodi 17.0 lakini kwenye Simu yangu ambayo inatumia(KitKat) haionekani na vilevile hata ile niliyokuwa nayo siioni play store ila kwenye Simu naomba msaada.
 
Kaka kwenye simu hata mie nikiuninstall na kuinstall haibadiliki ila najua wana new version ya 17.0
 
Back
Top Bottom