Kila upande moto unashuka,hivyo tuseme haina maana kuwa na vipangua makombora??

Kila upande moto unashuka,hivyo tuseme haina maana kuwa na vipangua makombora??

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,523
Reaction score
5,159
Miaka mingi tulikuwa tukihabarisha kwamba kila mtu ana mitambo ya kujilinda,wapo waliotolea mfano nchi ya ahadi hata ukitupa jiwe haliwezi kufika kwenye ardhi yao,yaan linapanguliwa juu kwa juu.

Huku baba wa dunia akisema yeye ndio kiboko wa mitambo ya kudungulia takataka zote zinazoelekezwa kwake.

Irani nae hakuwa nyuma kwenye kujipiga kifua kwamba anamitambo THABITI ya kupambana na vilipuzi vyovyote kama vinaelekea kwake.

SWALI LANGU:

Sasa tunaona kila upande unawaka moto,maana unafikiwa si Israel wala ndugu yake USA,hali ilivyo kwa Irani .

Inamaana ile mitambo ya kuzuia kombora yanazidiwa,yanachoka maana tunaona kila mtu anapigwa.

"NINACHOTAKA KUJUA KWAMBA VITA IKIISHA SITAKI KUSIKIA SIJUI MTAMBO HUU AU ULE NI KIBOKO KWA ULINZI".
 
Vipangua makombora vinasaidia mkuu,
Mvua zinazonyesha Israel bila mifumo hiyo Israel ingekua majivu nchi nzima 🙏
 
Zile ni mbwembwe Tu, hakuna mfumo ulio kamili hata kidogo...Tumeona jinsi Irone dome na mifumo mingine huko Israel inavyo jam, yaani mfumo unarushiwa makombora Hadi unachanganyikiwa wenyewe haujui utungue lipi, Ngoma zinapenya Tu fyaaaaahh....Iran naye mzushi Tu wale Israel na US wanapaa angani kama wapo kwao vle wanajpigia Tu watakavyo.
 
Miaka mingi tulikuwa tukihabarisha kwamba kila mtu ana mitambo ya kujilinda,wapo waliotolea mfano nchi ya ahadi hata ukitupa jiwe haliwezi kufika kwenye ardhi yao,yaan linapanguliwa juu kwa juu.

Huku baba wa dunia akisema yeye ndio kiboko wa mitambo ya kudungulia takataka zote zinazoelekezwa kwake.

Irani nae hakuwa nyuma kwenye kujipiga kifua kwamba anamitambo THABITI ya kupambana na vilipuzi vyovyote kama vinaelekea kwake.

SWALI LANGU:

Sasa tunaona kila upande unawaka moto,maana unafikiwa si Israel wala ndugu yake USA,hali ilivyo kwa Irani .

Inamaana ile mitambo ya kuzuia kombora yanazidiwa,yanachoka maana tunaona kila mtu anapigwa.

"NINACHOTAKA KUJUA KWAMBA VITA IKIISHA SITAKI KUSIKIA SIJUI MTAMBO HUU AU ULE NI KIBOKO KWA ULINZI".
Hata ukiwa bondia hodari kiasi gani huwezi kupangua mvua. Kwahiyo, hata the best missile defense system can be overwhelmed, kama idadi kubwa ya makombora itarushwa kwa wakati mmoja (saturation or swarm attack) kuelekea targets tofauti.
 
Mnaofuatilia silaha na majeshi pale vita zinapoanza huwa mnakuja na akili za kukariri. Kwa vile Tyson alikuwa anashinda basi yeye hajawahi pigwa ngumu wala kupoteza pambano, kwa vile Bayer Munich anachukua makombe mfurulizo pale Ujerumani basi yeye huwa hafungwi. Mawazo yenu yako hivyo.

Air defense systems zina vitu vingi:
1. Interception rate. Hii ni muhimu sana. Ni uwezekano wa kufanya successful interception kwa mashambulizi, mfano Iron Dome ni kama 85%. Makombora yenye hit to kill yanakuwa na rate kubwa ila yana bei sana.
Yenye fragmentation warhead ni makubwa ila yana ufanisi kidogo, compensation ni kuwa na warhead kubwa. Ndio maana Urusi huwa wanatuma salvo ya makombora kadhaa sababu wao hawana hit to kill.

2. Engagement success rate. Mifumo kadhaa kama Patriot na S-400 inaweza fanya interception ya fighter jet, cruise missile, ballistic missile na drone ila kila kitu hapo mfumo unakuwa na engagement success rate yake. So ikitokea Russian area ilikuwa covered let's say na S-400 alafu ikatokea suicide drone yenye speed ya 300km/h inayopaa mita 70 kutoka chini mfumo utafanya matokeo mabovu mno sababu ulitengenezwa kwa lengo la long range na threats kubwa, ila ikitokea fighter jet yenye speed ya 2700km/h na iko juu 25km kutoka chini mfumo utakuwa na matokeo mazuri sana. Sasa utajuaje sehemu hii adui atatuma hiki na sehemu hii atatuma hiki? Ni speculation zenye sababu, kumbuka adui sio muuza gongo kwahiyo anajua utatarajia nini, anakuja kinyume.

3. Operation availability rate. Maintenance yake, spare parts, etc. Rate inabidi iwe kwenye 90% kama maintenance ni nzuri.

4. Coverage. India ina batteries nyingi za S-400 imezifunga upande wa Kaskazini karibu na Pakistan na China kwa sababu ndio maadui. Pakistan iliporusha ndege zake mwaka juzi zilipigwa na S-400 zikiwa mbali kabisa hata hazijajaribu kuingia anga la India. Ila sasa mfano China yenye aircraft carrier ikiendesha kwenye maji alafu ikatokea Indian ocean ikarusha ndege au cruise missile Kusini mwa India basi targets zitapita bila kipingamizi na wewe utakuja hapa na "si mlisema India ina S-400 basi sitaki kusikia, hamna kitu".

Wakati wao waliagiza 10 batteries na sasa wameishapokea 6 batteries zilizounda squadrons 3, battery moja ina launchers 3-4, launcher moja ina interceptors 4, maximum engagement range ni over 300km, maximum detection range ni over 500km. Na sababu nchi yao kubwa wana mpango wa kuagiza batteries nyingine kama 10 hivi baada ya hii order kuisha ila bajeti ni kubwa mno.

Ukitazama mashambulizi mfano kwa UAE, yeye alikuwa anazuia zaidi ya 85% ya mashambulizi aliyotumiwa. Ukiona kombora moja mawili yamepenya usidhani ndio pekee yamerushwa.

So, haya mambo sio rahisi hivi. Na hapa tupo upande wa defender tena nimedonoa kwa ufupi mno, tukianza kumjadili attacked kuna mambo mengine mengi sana.
 
Back
Top Bottom