Kilango apasua jipu


Mkuu sidhani kama kuna mtu anakataa hilo............lakini usisahau kuwa shuka nyeupe ikiwa na doa basi inakuwa sio nyeupe kabisa......Mama Kilango kitendo cha kumsemea/kumpa sifa, Rais wakati wananchi wengi tumejaa na jazba ya vitendo vya ufisadi na hakuna hatua yoyote imechukuliwa dhidi ya hawa mafisadi.......Cha kuumiza zaidi hatumsikii Rais akikemea.....hapo ndipo utata unapoingia.

Mkuu naamini kuwa kuna haja ya kumsifia kiongozi anapofanya mema..(Unchangiaji wa visima vya Maji SAME)...na ni muhimu pia kumkosoa kiongozi anpoterereka hata ikiwa ni kidogo.......no more blank cheque to all viongozi
 
Anyway, sidhani kama maneno yako dhidi ya mama Kilango yatakuja kubadilika, kama nilivyosema ni kwamba tunategmea constructive criticism, ambazo zikiwa nzito zinaweza kumsaidia mama Kilango, binafsi, lakini hizi shutuma tuu name calling, hapana sasa unakosa hadhi hata wewe unayerusha hizi sumu,

Ndio maana tunasema hivi kama kuna personal beef hilo hatuwezi kumsadiai mtu, lakini kama ni kwa nia njema basi tutasikiliza, lakini hata wewe usipotoa blank check haina maana kuwa mama Kilango hatafanya shughuli zake,

Mama Kilango is doing great na umaarufu wake sas kwa Tanzania hauna mfano tena siku hizi, kuanzia wananchi mpaka wananchi muhimu sana kwenye jamii yetu wanamshimu sana, sasa sisi hatuwezi kumshauri kuangalia nyuma maana atageuka jiwe, pole sana mkuu lakini dunia imebadilika sasa hata kina mama ni viongozi shupavu pia, maana sisi Tanzania tukisubiri kiongozi anyefaaa kwa standard zako naona tutaishia kuliwa na simba na kiongozi tusimpate, sisi tunajaribu ku-deal na tulichonacho, lakini hatukosi usingizi kwa tusichokuwa nacho!

kina Mtikila ndio hao mambo yamewashinda, sasa sisi tunajaribnu kushikilia tulichonacho tena kwa mikono miwili!
 

Labda husomi post ukazielewa au ni mtu unayependa ku twist maneno....unaweza kunionyesha ktk post yangu ambayo kuna "name callin" kama unavyodai?

Ndio maana tunasema hivi kama kuna personal beef hilo hatuwezi kumsadiai mtu, lakini kama ni kwa nia njema basi tutasikiliza, lakini hata wewe usipotoa blank check haina maana kuwa mama Kilango hatafanya shughuli zake,

Mkuu namheshimu mama na sina bifu naye yeyote...yeye ni binadamu na kama kakosea kwa mwono wangu basi ni haki yangu kumkosoa ndio maana ya demokrasia tusiwe tunawapa free ride...mwishowe wanajisahau tushapewa fundisho.


Mkuu huu umaarufu ndio uliotufanya tumchague JK na umaarufu ndio uliofanya Zambia kumchagua Chiluba....Unajua matokeo yake.....nadhani kuna haja ya kuwa cautious kidogo ili tusirudie makosa yetu....Ni bora kuwatahadharisha viongozi kuliko kuwapa asilimia 100 ya sifa.
 
Binafsi Simjui Mama Kilango, Ila Katika Wabunge Wa C C M Ambao Wanaongea Na Kuponda Mambo Yanayofanywa Na Mafisadi Nimemsikia Sana Kwa Wanaokataa Hilo Naomba Mnitajie Wabunge Wengine Wa C.c.m Ambao Wanayasema Anayoyasema Mama Kilango. Fmes Limenipita La Kuchangia Ingawa Sitokei Huko Kwa Mama Kilango Lakini Ningeweza Hata Kutoa Elfu Ishirini Tuu Nadhani Ni Better Than Nothing (kwa People In Need Kama Wa Huko Same Mashariki)
 
mama kilango anafanya kazi nzuri ya kukemea mafisadi.

linalotuchukiza baadhi yetu ni hizi kauli zake za kumwagia sifa kikwete.

labda unaweza kusema tunaudhika bure, kwa sababu mama kilango hana choice ila kumwagia sifa kikwete ili aweze kuendelea na mapambano yake, kama vile msemo wa kiswahili unavyo sema "ukila na kipofu usimshike mkono".

kwa upande wangu nasubiri siku ambayo katika kura za bunge japo mara moja mbunge kutoka ccm atapiga kura ya kupingana na wenziwe wa ccm
 

Asante kwa ushauri mkuu. Lakini ningependa uelewe kwamba sina chuki binafsi na huyu mama. Simjui na wala hanijui.
Nilichokuwa nasema hapo juu ni kwamba huyu mama siku za nyuma alikuja juu sana pale bungeni na kukemea ufisadi na uchafu unaendelea ndani ya Tanzania na kusema wazi kwamba kama mapesa ya EPA hayatarudi na wahusika kutochukuliwa hatua basi pale bungeni hapakaliki.

Sisi si watoto, tunaelewa hasa nini kiini cha matatizo tuliyokuwa nayo Tanzania, na isitoshe hata majibu ya matatizo hayo tunayo ingawa hatuna uwezo wa kufanya majibu yetu yafanye kazi kimadaraka.
Tunaelewa kabisa kwamba Jakaya anahusika na uchafu huu (EPA, Richmond, IPTL nk) kwani ndiyo mapesa yaliyompeleka ikulu na ndiyo maana yuko kimya kuyashughulikia mambo hayo.

Kauli za huko nyuma za Mama Kilango kuhusu uchafu huo zina maana kwamba alikuwa anaungana na Watanzania wanaoibiwa utajiri wao katika kumtaka Jakaya na kundi lake warudishe utajiri wa Watanzania na hapo ndipo Mama Kilango alipopata support kubwa sana ya wananchi.

Lakini leo hii anapokuja na kauli inayopingana na kauli zake mwenyewe kwa kumsifia Jakaya eti ana uchungu na yote yanayotokea ndani ya Tanzania, huoni kama huyu mama anastaili kuitwa mnafiki kwa hilo?.
Tulimsifia kwa ukweli aliosema huko nyuma na hatutaona haya kumwambia ukweli kama anakosea kwa sasa.
Jakaya hana lolote alilolifanya kuondoa ama kukomesha uchafu unaoendelea nchini, hivyo hakuna haja ya kumwonea aibu na kuanza kumsifia (kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa). Inabidi aelezwe ukweli kwamba watanzania tunataka matendo na wala si maneno.

Tumechoka na tume juu ya tume ya kuichunguza tume na mwisho hatuoni wala kuambiwa la maana. Tume ya madini iliyokuwa chini ya Bomani imekabidhi report na matokeo yake yamekuwa nini?. Ndiyo kwanza report hiyo kapewa mwizi kabla ya wananchi kuipata. Miezi sita ya kuchunguza EPA imefika na sasa ni wiki toka Jakaya apewe report je umesikia ama umeona amefanya nini?. Hivi ni kweli kabisa unathubutu kusema kwamba Jakaya anaitakia mema nchi yetu?. Ni mila na desturi za wapi mwizi anabembelezwa na kutandikiwa kapeti jekundu?. Ushaidi wa kuibiwa upo na mwizi unamjua unaunda tume za nini, ama unachunguza nini tena kama si uzandiki?.
Kama Nalaila Kiula aliwekwa ndani na kufungiwa account zake kwa wizi wa shs bil 3 alituibia sasa hawa wezi wa EPA, Richmond, Kiwira mbona wanapeta mitaani?. Nina hasira sana na wewe ama na watu wa type yako.
 

Maelezo ni mazuri..Ila marekebisho kwenye highlight ni kuwa alisema pesa zirudishwe mwanzoni pale aliposema bungeni hapata kalika...Lakini sikumbuki aliposema washughulikiwe.
Na hapo ndipo kulipokuwa na mgogoro hapa jf kwani nilisema wazi kuwa kama hasemi mafisadi wakamatwe basi hakuna lugha nyingine ya kutu convince.
Tunashukuru kwa ujenzi wake wa visima.
Hapo Same kuna UKAME mkubwa sana licha ya uwezekano wa kulitatuwa tatizo hilo..Bado limekuwa likipigwa dana dana toka awamu ya kwanza ya Mwalimu.
Hivyo basi...Bado kipimo ni VITENDO DHIDI YA MAFISADI.
At least kwa wengi wetu hapa jf.
 

True patriot.

Loves country but watches his or her government.

Questions the ruling elite and calls out their bluff and chicanery.

A voice not very popular or easy to work out its true meaning. But priceless!

I demand to be enlisted now as a foot soldier to the next battlefield under your lead.

True patriot!
 
Jakaya Mrisho Kikwete Ni Rais, Narudia Wakuu Wangu Kuwa Jakaya Mrisho Kikwete Ni Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.

Yeyote Yule Ambaye Si Mke Wake Au Babake Hana Nafasi Ya Kumuita Jakaya Au Kikwete Always Ni Mh.rais Au Ndg.rais, Hiyo Ni Standard Ya Kidunia Ambayo Hata Mwenyezi Mungu Ameibariki.

Conclusion Yangu: Awe Kilango, Lipumba,mrema,rostam,lowasa,malecela,mkapa,mwinyi,mama Mariah Na Sisi Sote , Ni Wajibu Wetu Kumheshimu Rais Wetu, Ni Wajibu Wetu Kumsaidia Kiustaarabu Rais Wetu,kumshauri Kwa Heshima Rais Wetu,kumfanyia Kazi Kwa Adabu Rais Wetu, Kumheshimu,kumuamini,kumsikiliza Na Zaidi Kumuimarisha Rais Wetu. Hivyo Si Hekima Wala Nidhamu Kumdhalilisha Rais Just B'coz Kuna Rushwa Imetapakaa Nchini Mwake,yeye Ndiye Bora Ktk Miaka 5 Hii Tuliyompa,tusikufuru Jitihada Zake Na Wale Wanaomsaidia Kupambana Ktk Vita Nyingi Za Kifisadi Na Umaskini Nchini. Kilango Anaonyesha Wajibu Wake Ktk Kutii Mamlaka Alizopewa Ndg.rais Jakaya Mrisho Kikwete
 
Ndio uzuri wa JF, sio kila mtu amefukuzwa huko nyumbani kwa mama kilango, mama Kilango is doing great, sasa yuko Same East ambako alienda kuweka msingi wa visima 30 vipya vya maji katika jimbo lake,

Kikwete ni rais wa jamhuri, aliyechaguliwa kikatiba na ni clear kuwa atachaguliwa tena kwa term ya pili, strategy ya mama Kilango ya kushambulia mafisadi na kumpa heshima rais, hata mimi ningeitumia hiyo kwa nchi kama yetu ya Tanzania na mazingara yake kisasa, waliofukuzwa nyumbani kwake na sasa hawatakiwi tena hakuna cha kuwasadia, waendelee kulia lia hapa JF,

Wa-Tanzania wngi tunaridhika na kazi ya mama Kilango so far, kwa wwale ndugu zangu naona tutaendelea kufa ndani ya mioyo yetu, maana mama Kilango ambaye sasa anafuata na waandishi wa habari hata akienda jimboni ndio huyooo anaondoka na taifa tuko nyuma yake!

Mkuu FDRJr, heshima mbele kwa kuiweka hii ishu inapotakiwa! maana hapo umedhirisha kuwa sio wote hapa wamefukuzwa huko nyumbani kwa mama Kilango!
 
i dont have anything against mama Kilango, hatuwezi kuelewa yuko kwenye hali gani huko ndani ya ccm kutokana na msimamo wake, namsupport katika yote anayoyafanya katika kusimamia haki, lakini hapo ktk kusema kikwete ana nia.....i totally disagree with her, sababu miye binafsi sijaiona hiyo nia ya ndg kikwete hadi hapo nitakapoanza kuiona hiyo nia, kwasasa bado kabisa!
 

Mnanichekesha sana pale mnapopenda mambo ya West na ikifika kwenye issue nyeti mnachomoa na kudai eti heshima!

Kama alitaka kuitwa Jakaya na mama yake mzazi ama baba ama mke wake peke yake then asingegombea urais kwani kadhia yake inajulikana!

Hivi umeshawahi kuona kipindi cha katuni cha Little Bush?
 
Yeyote Yule Ambaye Si Mke Wake Au Babake Hana Nafasi Ya Kumuita Jakaya Au Kikwete Always Ni Mh.rais Au Ndg.rais, Hiyo Ni Standard Ya Kidunia Ambayo Hata Mwenyezi Mungu Ameibariki.

Kama ndio standard ya dunia basi kuna wengy wanahitaji kufundishwa.



Mbona, ustaadhi unaturudisha enzi za "yes mtukufu?"
 
Mbona, ustaadhi unaturudisha enzi za "yes mtukufu?"

Heshima ni kitu cha bure na ni kitendo kidogo sana kinacho-define utu na ustraabu wa mtu, kumheshimu rais au mwananchi yoyote kutokana na umri wake, au nafasi yake kwa jamii, haizuii kutokubaliana na mawazo yake kisiasa, hilo ndilo tatizo kubwa sana ambalo liliwakuta wanasiasa wa mwanzoni wa upinzani wetu bongo,

in fact mpaka leo bado wana-struggle sana kwenye hili la lugha ya ku-connect kisiasa na wanachi walio wengi hasa vijijini, kwa sababu sisi originally tulitawaliwa na Waingereza, waliotufundisha tabia za u-conservative na hiyo tabia imetukaa mpaka leo nationally, kitendo cha kiongozi wa upinzani kumkemea rais, tunaona ni kukosa heshima sasa kiongozi wa upinzani atatumia lugha gani wakati makosa yamefanyika hapo ni kazi kwa upinzani wetu ku-figure out!

Lakini mwananchi mstaarabu ni lazima kuheshimu viongozi, na pia kuwakosoa kwenye makosa, Otherwise, hata kama una hoja inaweza isionekane kutokana na kukosa ustraabu, hapa Mkuu FDRjr tupo ukurasa mmoja heshima lazima iwe mbele!
 


Hivi wewe unaishi katika dunia hii ama sayari ya kwako peke yako na wenye mawazo kama yako. Msimamo wako huu unanipa picha halisi ya matatizo waliyonayo Watanzania kwa mambo ya msingi. Kwa kauli yako hata Raisi akitembea uchi, bila shaka utamwona kavaa -yale yale!!

Raisi ambaye hawezi kusimamia maagizo anayoyatoa mwenyewe na kushindwa hata kukemea wale wanaoharibu, tumtafutie sifa gani. Na huyo mtu ambaye anashindwa kutambua kuwa Raisi katoka bila kuvaa na kuanza kumsifia anavyomereta bila nguo, tumwiteje. Na sisi tunaokataa na kumwambia ukweli kuwa hapo amechemsha, tuna kosa gani.
 
Na huyo mtu ambaye anashindwa kutambua kuwa Raisi katoka bila kuvaa na kuanza kumsifia anavyomereta bila nguo, tumwiteje. Na sisi tunaokataa na kumwambia ukweli kuwa hapo amechemsha, tuna kosa gani.

Unaweza kuitwa kuwa una makengeza, sababu sio kwamba wewe ukiomuona rais yuko uchi basi wote wanamuona hivyo, na huwezi kulazimisha kila mtu aone hivyo, sasa uweke hoja ichambuliwe,

Mama Kilango hajakosea kisu, isipokuwa hizi ni personal problems ambazo zinajaribiwa kulazimishwa kuwa ishus lakini si unaona hakuna anyezikubali kwa sababu Tanzania tuko wananchi 40,000,000 sasa, iweje mtu mmoja akimuona rais yuko uchi badala ya kujaribu kuwashawishi na wengine aanze matusi kila kona na kila jina la Mama Kilango linapotajwa, huo ni ujuha hiyo sio siasa in the process unapunguza heshima yko tu mkuu na maneno mengi against mama ambaye so far Tanzania karibu nzima inamkubali kuwa ni kiongozi safi!
 
Mkuu Mag3 hebu soma hapa chini uone kuwa sio kweli kwamba wananchi wote wanaamini maneno yenu against mama Kilango,

KONA YA KARUGENDO: Mama Socrates wa Tanzania

Padri Privatus Karugendo Julai 2, 2008

ANNE Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki, akichangia hotuba ya Bajeti Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo, alijifananisha na mwanafalsafa wa zamani Socrates. Alisema yuko tayari kufa akitetea ukweli.
ANNE Kilango Malecela Socrates alikataa kwenda kinyume na yale aliyokuwa akiyaamini na kuyatetea katika jamii ya wakati wake. Wafuasi wake walimbembeleza akubali kukana ukweli, ili apone kifo. Enzi hizo Socrates, alikuwa muhimu sana katika jamii na alikuwa mwalimu wa kutegemewa na watu wengi.

Hivyo wafuasi wake waliona ni bora, akane ukweli, ili aendelee kuwapo kuwafundisha na kuibua mambo mapya katika ulimwengu wa fikra. Lakini Socrates alikataa kukana ukweli, maana hakuna heshima ya mwanadamu kuzidi mtu kufa akitetea ukweli. Hivyo Socrates, alikubali kufa kwa kunywa sumu! Galileo Galilei, mwanasayansi na bingwa wa hisabati wa kale wa Italia, aliyeshutumiwa kwa mawazo yake kwamba dunia ilikuwa mviringo na inalinzuguka jua, alipata kusema kwamba “ ukweli mara zote ni rahisi kuuelewa pindi unapougundua; tatizo ni jinsi ya kuugundua.” Niongezee hapa kwamba na pindi mtu anapougundua ukweli, na kwa vile mara zote ukweli ni rahisi kuuelewa, ni lazima mtu awe tayari kuufia ukweli huo.

Anayekubali kusaliti ukweli, anausaliti utu wake na heshima yake kama binadamu. Imeandikwa kwenye Biblia, kwamba Musa, alinyosha mikono na jua likasimama.Usiku haukuingia, hiyo ikawasaidia wana wa Israeli kupambana na maadui zao. Uvumbuzi wa ukweli wa Gelileo, ulipingana na dhana hii, maana jua limesimama daima, na kinachozunguka ni dunia. Galileo, alikuwa tayari kufa akitetea ukweli huu. Ameheshimika hadi leo hii, na ukweli umebaki ule ule kwamba dunia ni mviringo na inazunguka jua.

Anne Kilango Malecela au Mama Socrates wa Tanzania, ameugundua ukweli juu ya udhibiti na ulinzi mbovu wa fedha za umma. Na kwamba fedha nyingi ziko mikononi mwa watu wachache. Na kwamba watu wachache hawa wakiendelea kushikilia fedha hizi peke yao, hatuwezi kuendelea. Ametoa mfano wa fedha za EPA, zilizoingia mikononi mwa watu wachache kwa njia za udanganyifu. Ukweli huu unamfanya mama huyu awe tayari kufa, kama alivyosema menyewe, kama watu wengine waliokufa wakiutetea ukweli.

Mwanafalsafa mwingine wa zamani wa Ujerumani, Arthur Schopenhauer, aliyeishi kati ya mwaka 1788 na 1860, alisema hivi ju ya ukweli: “ ukweli wowote hupitia ngazi tatu. Kwanza, ngazi ya kukejeliwa. Pili, ngazi ya kupingwa na hata ikibidi damu kumwagika. Na tatu, ni ngazi ya kukubalika; kwa kuwa ukweli hujisimamia wenyewe”.Hivyo kwa hoja ya Arthur Schopenhauer, haishangazi kuona akina mama Anna Abdalah, Chitalilo na wengine wanamkejeli Anne Kilango. Wanasema anapayuka, wanasema anazungumza kwa mbwembwe, wanasema lengo lake ni kutaka kugombea kiti cha Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, wanafikiri anakisaliti chama chake cha CCM, wengine wanakwenda mbali kusema kwamba ana hasira za kushindwa kuingia Ikulu 2005, kwamba mbio za Mzee Malecela ziliishia sakafuni.

Hizo zote ni hatua za kupita katika kutafuta ukweli. Na jinsi hali inavyokwenda, na labda ndiyo maana Anne Kilango, anasema haogopi- inawezekana hata hatua ya pili ya kumwagika damu tukaipitia, (bila hekima, busara na uzalendo) kabla ya ukweli wenyewe kukubalika na kujisimamia.


Ingawa sifahamu vizuri historia ya mama huyu Socrates wa Tanzania, hoja zake zinashawishi na kuwagusa Watanzania wengi wa kawaida. Uchumi wa Tanzania, uko mikononi mwa wachache. Wakati maisha yanaendelea kuwa magumu, bei ya mafuta inapanda, mfumko wa bei unashika kasi ya kutisha, lakini wachache wetu wanaogelea katika ufahari.

Wanafanya manunuzi na matumizi yao nje, wanasomesha watoto wao nje, wakiugua wanakimbizwa India, Ulaya au Marekani. Wamejenga majumba ya kifahari na wanaendesha magari ya bei mbaya. Ipo mifano mingi ya kuelezea jambo hili na Watanzania wengi sasa wanafahamu.


Panahitajika watu wachache wa kusimama na kutetea ukweli. Utafiti wa haraka unaonyesha kwamba idadi kubwa ya Watanzania inashawishiwa na mawazo ya watu kama kina Anne Kilango, kuliko ya Chitalilo na Mzindakaya.
Hoja yangu ni kwamba kila raia mwema wa Tanzania, hawezi kupuuzia msimamo wa kutafuta na kusema ukweli. Mbegu ya kutafuta na kusema ukweli haiwezi kuoza. Ni hekima kwa viongozi kuanza kusoma alama za nyakati.



Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa S. L. P. 114 Magu, Mwanza. Simu: 0754 633122
 

Mkulu unaniacha hoi

huo ni ujuha hiyo sio siasa in the process unapunguza heshima yko tu mkuu
 
Name Anne Malecela
Surname Malecela
First Names Anne Kilango

Country of Birth Tanzania

From To Organisation Position 2005 Same Constituency MP for Same
Date of Birth 9 Jan 1956
Political Affiliation CCM

Notes EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Chang'ombe Teachers' Training College Teaching Course 1978 1979

CERTIFICATE
Shycom Secondary School A-Level Education 1975 1976 HIGH SCHOOL
Weruweru Secondary School O-Level Education 1971 1974 SECONDARY
Jitengeni Primary School Primary Education 1964 1970 PRIMARY
--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date :KLM Airline Accountant 1993 1994, Gulf Air Corporation Financial Controller 1991 1993, Air Tanzania Corporation(ATC) Accountant 1983 1991, Kisutu Girls' Secondary School Teacher 1979 1983
--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Parliament of Tanzania 2000 2010
Chama Cha Mapinduzi - CCM Chairperson (UWT Kinondoni District) 1997 2003
[ Retrieved on 17/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…