Kilango asema hana Ugomvi na Lowassa

Status
Not open for further replies.


Very true ... halafu comments zake zinaonyesha ka uoga fulani .. oooh mimi sina ugomvi nae... hatat tukikutana tunasalimia ... why all that details... hawa wanasiasa wetu vipi???
 
Unamwonea. Haropoki. Anasema anachoamini. Kwani jamani kila siku mtu aseme tunachopenda? Mama ana uhuru wa mawazo kulingana na imani ya chama chake cha siasa. Ana mipaka - CCM

Zitto

Mbona unamtetea sana huyu mama,kulikoni?tetea hoja bwana usitetee mtu.How far are you sure kwamba anachokisema ndicho anachoamini?umeingia moyoni mwake? USIUSEMEE MOYO! nyie wanasiasa wakati mwingine huwa mnazungumza tofauti na mnachokiamini including you Zitto.
 

Mkuu hii ni copy and paste from gazeti la Mtanzania,ni habari ilyoripotiwa na gazeti la jumatano nov 25 2009 au kosa kuwahabarisha wale ambao hawakusoma hilo gazeti lakini pia kupata maoni ya watu mbalimbali?
 
Mkuu hii ni copy and paste from gazeti la Mtanzania,ni habari ilyoripotiwa na gazeti la jumatano nov 25 2009 au kosa kuwahabarisha wale ambao hawakusoma hilo gazeti lakini pia kupata maoni ya watu mbalimbali?


- Mkuu acha kuhangaika nani amesema ni kosa of anything, hoja hujibiwa kwa hoja nimetoa hoja jibu hoja, umetoa maoni yako nimetoa yangu tatizo liko wapi?

es!
 
Lazima tukubari kuwa Lowassa ni powerful na inahitaji mtu mwenye kujiamini sana kisiasa kumkana hadharani. Na tukubari pia kuwa mama kilango alikuwa na haki ya kujibu vile anavyoona inafaa. Yale maswali aliyoulizwa hayakuwa ya bahati mbaya hata yeye anajua kuwa hayakuwa ya hapo kwa hapo bali yalipangwa mapema na lengo linaonekana wazi nalo ni kupima kama amesha lainika na ile warning ya mama simba. Maadamu sasa ameshailainika basi ataachiwa ajinyonge mwenyewe.

Ila kama angleeta jeuri tena wangelipua kingine mpaka watakapofika kwenye karata yao ya mwisho ya mapowwwwwder!
 
Why????????!!!!!!

Kwa sababu kasema hana ugomvi na Eddo?

Yes , mama kilango yupo sawa hana ugomvi na mtu , yeye shida yake ni SUALA or sema "ISSUE SIYO PERSONALITY"
 
Mkulu ES

Wewe ni mtoto wa kiafrika,zaidi ya yote unajua nchi hii ilipata vipi uhuru wake,unajua fika akina Mzee Malapa,Aziz Ally,Jumbe Tambaza ,Dossa Aziz walifanya nini pamoja na Mwalimu mpaka tukapata uhuru.

WALIFANYA MENGI.

Inapofika YULE ambaye WAZEE WA DSM walimwamini akasema "FULANI" hafai kuongoza nchi,HILO PEKE YAKE NI PIGO kwa "FULANI" unless hujua NCHI HII ILIPATA VIPI UHURU.

ES kuhusu suala la EL , sikosi usingizi.
 

Heshima kwako Shalom.

Naomba kutokubaliana na wewe kwamba Lowassa ni powerful.
Lowassa anaweza kuonekana ana nguvu kwenye mfumo usiozingatia sheria na taratibu katika uendeshaji wa nchi.Mfumo wetu unatoa fursa kwa aina yoyote ya wezi kushamiri / kustawi hata kufikia hatua ya kuwanyoshea vidole waadilifu.Laiti Lowassa angekuwa powerful kwa kufuata taratibu na sheria tulizojiwekea ningekubaliana na wewe lakini nguvu za kuchonga na kununua wajumbe wa kutetea dhambi hatuwezi kuziita ni nguvu bali ujambazi bila kuuma maneno.

Mkuu Shalom umewahi kujiuliza hata mara moja ni kwanini wajumbe wa NEC na CC ya CCM wenye kashfa za ufisadi hawapelekwi mahakamani ?.Napata hisia kina Basil Mramba na Daniel Yona wangekuwa wajumbe wa NEC wasingepelekwa mahakamani.Kwa maneno rahisi kabisa NEC na CC ya CCM ni chaka la majambazi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…