"Kilaza" Mfano mzuri wa ukuaji wa lugha ya Kiswahili

"Kilaza" Mfano mzuri wa ukuaji wa lugha ya Kiswahili

kamwendo

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
900
Reaction score
1,923
Nimevutiwa na na hili neno wakuu,nimelikuta hapa hapa JF na maana yake nimeijulia hapa..

Juzi nimejaribu kumwita rafiki yangu kwa jina hili, akaniambia tena yeye ni kilaza haswa, nikamuuliza unajua maana yake ni nini? Akashindwa kunijibu. Nilipomwambia namaanisha kwamba ni mjinga au mtu asiye na akili alibaki anacheka...

Tujivunie Kiswahili jamani.
 
Yaa ni neno muafaka, mimi kwa mara ya kwanza hili neno nililikuta pale UDSM mwaka 1999 nilipojiunga mwaka wa Kwanza, na sasa nimeliona hapa na limekuwa common sana hasa vyuo vikuu, pamoja na hili kuna maneno mengine pia kama KIHIYO yanafaa pia! kama neno "Tapeli" lilivyohalalishwa kuwa neno sahihi la kiswahili!
 
Kilaza ni mtu fulani anayelaza laza mambo. Mwingi wa ajizi. Hata jambo linaloweza kufanyika leo yeye atataka kulichelewesha, kiingereza anaitwa "procrastinator". Mzembe na mvivu. KWa sababu hii anakuwa mjinga.
 
Neno "kilaza" lilianza kama utani pale UDSM miaka ya 80. Mwanamuziki mmoja wa Morogoro, Juma Kilaza, aliyekuwa mtani wa Mbaraka ktk mambo ya muziki, alirudi ulingoni baada ya kutokuwepo ulingoni kwa muda mrefu.

Aliporudi, muziki wake ulikuwa wa kiwango cha chini ajabu. Si kama Kilaza wa miaka ya 60 na 70.

Basi hapo yakaanza masihari, kwamba "Unafanya kama Kilaza" Ndipo neno "kilaza" lilipopata umaarufu na kutumika zaidi na zaidi.
 
Kilaza ni mtu fulani anayelaza laza mambo. Mwingi wa ajizi. Hata jambo linaloweza kufanyika leo yeye atataka kulichelewesha, kiingereza anaitwa "procrastinator". Mzembe na mvivu. KWa sababu hii anakuwa mjinga.

Neno hili lilitokana na kejeli ambazo nguli wawili wa muziki marehemu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka na Juma Kilaza walipokuwa wakipambana......kwa kuwa Mbaraka aliishis kuwa juu basi watu wote wachovu wakalinganishwa na Kilaza
 
Ahsante kwa historia.

Kilaza ilikuwa na maana ya mtu anayelaza mambo kabla hata ya malumbano ya Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza kama kikojozi ilivyokuwa na maana ya mtu anayekojoakojoa au kiongozi mtu anayeongoza.

Ilikuwa rahisi kwa Kilaza kukejeliwa kwa sababu jina lake lilikaa kukejelika.
 
Okay.... kama ilivyo kanyaboya, kibonde nk etc
 
Kiranga na Safari_ni_Safari asanteni sana kwa hili la Kilaza, nilikuwa sijui kumbe lilitokea huko. Na Solemba nayo imetokea kwenye muziki? Maana kuna wimbo wa zamani wenye jina hilo lakini wenyewe ni jina la mtu.
 
Last edited by a moderator:
Yaa ni neno muafaka, mimi kwa mara ya kwanza hili neno nililikuta pale UDSM mwaka 1999 nilipojiunga mwaka wa Kwanza, na sasa nimeliona hapa na limekuwa common sana hasa vyuo vikuu, pamoja na hili kuna maneno mengine pia kama KIHIYO yanafaa pia! kama neno "Tapeli" lilivyohalalishwa kuwa neno sahihi la kiswahili!

ha ha ha,pia DESA,VIMBWETA,KUBEBANA...ha ha MLIMANI pale ndo penyewe kwa vijineno ivo
 
Desa lilitokea pia miaka ya 80 udsm. miaka ya sabini na themanini kulikuwa na riwaya iliyoitwa THE ODESSA FILE iliyoandikwa na F. Forsyth. Humo kuna hadithi mafaili yatoka enzi za NAZI ktk pande za Odessa. Basi wanafunzi udsm wakaanza kutumia title hiyo wakimaanisha mafaili yanayorithiwa na wanafunzi, mafaili yenye mitihani ya huko nyuma, makala, nk Kidogo maamna yake imebadilika kwa kuendeleza maana hiyo.
 
Asante kwa ufafanuzi wako mkuu.
 
na hili neno- simbi? au kujongo, kuingia mitini? kideo? muugro? nani anayakumbuka?
 
Neno "kilaza" lilianza kama utani pale UDSM miaka ya 80. Mwanamuzi mmoja wa Morogoro, Juma Kilaza, aliyekuwa mtani wa Mbaraka ktk mambo ya muziki, alirudi ulingoni baada ya kutokuwepo ulingoni kwa muda mrefu. Aliporudi, muziki wake ulikuwa wa kiwango cha chini ajabu. Si kama Kilaza wa miaka ya 60 na 70. Basi hapo yakaanza masihari, kwamba "Unafanya kama Kilaza" Ndipo neno "kilaza" lilipopata umaarufu na kutumika zaidi na zaidi.
6febfe347bae4b3891bda5d0b8fbe82f.jpg

Kwenye hiyo picha huyo kilaza ndo yupi?
 
6febfe347bae4b3891bda5d0b8fbe82f.jpg

Kwenye hiyo picha huyo kilaza ndo yupi?
Ni huyo wa mbele waliosimama; mwenye flana nyeusi (ameshika maracas)

scan0030.jpg

Kutoka kushoto waliosimama Capy John Simon, Shem Karenga, Muhidin Gurumo, Juma Kilaza, Ally Rashid, Kassim Mapili na Salum Zahoro.
 
kilaza asili yake nasikia ni msanii wa zaman hajui kitu ila alikuwa anajifananisha na mwishehee
 
Back
Top Bottom