Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza walikuwa ni mahasimu wa aina yake.
Alipofariki Salum Abdalah ambae ndie alikuwa kiongozi wa Cuban Marimba ndipo Juma Kilaza akashika usukani kuongoza bendi hiyo.
Kama mnakumbuka wimbo wa "Mkono wa Iddi" ulitungwa na Salum Abdalah.
Lakini Juma Kilaza akaanza zogo mjini Morogoro kwa kuimba wimbo wake uitwao Dada Kidawa (lakini nakaribisha mwenye kumbukumbu anirekebishe hapa).
Ndipo kuona hivyo Mbaraka akamjibu kutaka kumtuliza Juma Kilaza na kumkumbusha kwamba pale mji kasoro bahari pana walotangulia, akatunga kwa wimbo wake usemao "Matusi ya nini?"
Hii ni sehemu ya wimbo huo wa Mbaraka Mwinshehe kwenda kwa Juma Kilaza:
"Tulikua na Salumu mpaka kaenda Ahera wala hatukutukanana,
Alipoingia yeye aliyoleta si miziki bali ni matusi,
Mji wa Morogoro ulisifika sana kwa mambo ya miziki na nyimbo zenye maana ooo,
Amekuja mchafuzi wa jina la Moro Jazz na Mororgoro nzima,
Chorus Huyooo aona kijicho Sululu la chuma liko Imara,
Matusi yake Mjini Morogoro yameleta sifa mbaya,
Sifa ya Moro jazz ni ya Taifa chuki yake ni ya bure"
Juma Kilaza alikaa na kutafakari sana juu ya ujumbe huu, anapoambiwa atulie Morogoro.
Mwenyezi Mungu azidi kuwarehemu wanamuziki hawa magwiji.