Kilaza ni mtu fulani anayelaza laza mambo. Mwingi wa ajizi. Hata jambo linaloweza kufanyika leo yeye atataka kulichelewesha, kiingereza anaitwa "procrastinator". Mzembe na mvivu. KWa sababu hii anakuwa mjinga.
Neno hili lilitokana na kejeli ambazo nguli wawili wa muziki marehemu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka na Juma Kilaza walipokuwa wakipambana......kwa kuwa Mbaraka aliishis kuwa juu basi watu wote wachovu wakalinganishwa na Kilaza
Kilaza ilikuwa na maana ya mtu anayelaza mambo kabla hata ya malumbano ya Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza kama kikojozi ilivyokuwa na maana ya mtu anayekojoakojoa au kiongozi mtu anayeongoza.
Ilikuwa rahisi kwa Kilaza kukejeliwa kwa sababu jina lake lilikaa kukejelika.
Kiranga na Safari_ni_Safari asanteni sana kwa hili la Kilaza, nilikuwa sijui kumbe lilitokea huko. Na Solemba nayo imetokea kwenye muziki? Maana kuna wimbo wa zamani wenye jina hilo lakini wenyewe ni jina la mtu.
Yaa ni neno muafaka, mimi kwa mara ya kwanza hili neno nililikuta pale UDSM mwaka 1999 nilipojiunga mwaka wa Kwanza, na sasa nimeliona hapa na limekuwa common sana hasa vyuo vikuu, pamoja na hili kuna maneno mengine pia kama KIHIYO yanafaa pia! kama neno "Tapeli" lilivyohalalishwa kuwa neno sahihi la kiswahili!
Desa lilitokea pia miaka ya 80 udsm. miaka ya sabini na themanini kulikuwa na riwaya iliyoitwa THE ODESSA FILE iliyoandikwa na F. Forsyth. Humo kuna hadithi mafaili yatoka enzi za NAZI ktk pande za Odessa. Basi wanafunzi udsm wakaanza kutumia title hiyo wakimaanisha mafaili yanayorithiwa na wanafunzi, mafaili yenye mitihani ya huko nyuma, makala, nk Kidogo maamna yake imebadilika kwa kuendeleza maana hiyo.
Neno "kilaza" lilianza kama utani pale UDSM miaka ya 80. Mwanamuzi mmoja wa Morogoro, Juma Kilaza, aliyekuwa mtani wa Mbaraka ktk mambo ya muziki, alirudi ulingoni baada ya kutokuwepo ulingoni kwa muda mrefu. Aliporudi, muziki wake ulikuwa wa kiwango cha chini ajabu. Si kama Kilaza wa miaka ya 60 na 70. Basi hapo yakaanza masihari, kwamba "Unafanya kama Kilaza" Ndipo neno "kilaza" lilipopata umaarufu na kutumika zaidi na zaidi.
Ni huyo wa mbele waliosimama; mwenye flana nyeusi (ameshika maracas)
Kwenye hiyo picha huyo kilaza ndo yupi?
Vipi kuhusu chanzo cha neno "Changa la macho".