Kile kichaka cha CAF ranking kinakaribia kufyekwa rasmi na Yanga ndiyo maana stress na uoga ni mwingi upande wa pili

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Mpaka sasa Yanga anazo alama 34 kwenye CAF ranking na tayari keshaingia kwenye 10 Bora ya CAF ranking.

Simba baada ya kufuzu robo fainali kafikisha alama 38, endapo Yanga atafuzu robo fainali klabu bingwa atafikisha alama 39 na kumshusha Simba!

Kwa maana iyo ili Simba arudi kwenye nafasi yake tena ni mpaka afike nusu fainali ya shirikisho vinginevyo ataendeleza kuwa chini ya Yanga rasmi!
 
Calculator unayo?

Hebu angalia hiyo link. Mpaka 2024 Simba ailikuwa wa 7 point 39, Kwa kwenda Robo tayari ameongeza point 3 maana yake kibindoni ana poin 42.

Utopolo nafasi ya 13, point 31, tumia calculator mkifika final ya CAF Champion League mtakuwa na point ngapi na utahitaji kufika final mara ngapi na probability ya kufika final back to back ni ngapi kwenu.

Kwa maana iyo ili Simba arudi kwenye nafasi yake Tena ni mpaka afike nusu fainali ya shirikisho vinginevyo ataendeleza kuwa chini ya yanga rasmi!
Hapo umechemka. Nafasi ya timu haitegemei kitu kimoja tu cha kufikia hatua fulani, bali pia hatua za timu zilizopo mbele yako na mwaka husika (kumbuka weight ya points inapungua kuanzia mwaka husika kurudi nyuma miaka mitano)
 
Calculator
 
Duh unaelewa ulichokiandika? Unaelewa maana ya CAF 5 year ranking, alama zinazidishwa kwa coefficient za mwaka husika kwa miaka mitano nyuma kuanzia msimu huu, i.e 2025 robo shirikisho alama 2 ×5= 10, 2024 robo club bingwa alama 3×4=12, 2023 robo club bingwa alama 3×3=9, unaendelea hivyo mpaka msimu 2021 ukijumlisha unapata alama 38.Msimu huu Simba ameanza na alama 28 (ondoa alama za msimu 2020) ukijumlisha na alizovuna msimu huu robo shirikisho 28+10=38
 
Hapo umechemka. Nafasi ya timu haitegemei kitu kimoja tu cha kufikia hatua fulani, bali pia hatua za timu zilizopo mbele yako na mwaka husika (kumbuka weight ya points inapungua kuanzia mwaka husika kurudi nyuma miaka mitano)
Yupo sahihi, coefficient za msimu huu ni 5, i.e robo simba shirikisho alama 2 zidisha kwa 5 = 10, ukijumlisha na za misimu minne iliyopita(ondoa za msimu 2020) inakuwa 28+10=38 Yanga ukiondoa za msimu 2020 ana alama 24, akifuzu robo alama 3 zidisha kwa coefficient za msimu huu 3×5=15 ukijumlisha 24+15=39 anakuwa juu ya Simba na Wydad
 
Hapo umechemka. Nafasi ya timu haitegemei kitu kimoja tu cha kufikia hatua fulani, bali pia hatua za timu zilizopo mbele yako na mwaka husika (kumbuka weight ya points inapungua kuanzia mwaka husika kurudi nyuma miaka mitano)
Usidhani mpaka naweka ivyo sijafanya hesabu,,ebu fatilia vizuri utapata jibu la icho unachokizungumzia,,na yanga akifika nusu fainali anaingia top 5 ya vilabu barani Africa upo hapo!
 
Umemjibu vizuri anadhani tunafanya hesabu za vidole!
 
Akuna unachokijua wewe ebu Rudi darasani au waulize wenzako wanaojua namna point za caf zinavyotolewa,,naona uko mweupe kichwani
 
Mmebadilika nyumbu.Kwanza mlidai rankings hazina maana.Sasa mmerudi na ngonjera nyingine.Mmekuwa chini ya Simba kwenye rankings miaka mingapi?Kubalini hilo halafu tujadili yajayo.Rankings zimekuwa deal tena au?
Si mlikuwa mnatamba na izo rank au sio nyie? Sasa kinafyekwa tuone mtatamba na nini Tena maana ndio kichaka kilichokuwa kimebaki ni suala la muda tu!
 
Uyo achana nae akuna anachokijua ni wale mashabiki bendera fata upepo yupo yupo tu
 
Mmebadilika nyumbu.Kwanza mlidai rankings hazina maana.Sasa mmerudi na ngonjera nyingine.Mmekuwa chini ya Simba kwenye rankings miaka mingapi?Kubalini hilo halafu tujadili yajayo.Rankings zimekuwa deal tena au?
Taratibu mtazoea tu kua chini yetu.
 
Hivi unakijua ulichokiandika au unaleta umbumbumbu FC hadi huku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…