Kilele cha wiki ya vijana mwanza chawaibua maelfu ya vijana wakiapa kusimama na Rais Samia 2025, wapinzani wabaki midomo wazi wasijue cha kufanya

Kada Mzalendo

Senior Member
Joined
Oct 9, 2024
Posts
142
Reaction score
97
Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Vijana kilichofanyika jana Mkoani Mwanza kimethibitisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi anayependwa na kukubalika na kundi kubwa la vijana.

Shangwe, nyimbo, na hisia za wazi zilizojitokeza zilionyesha jinsi vijana wanavyomuunga mkono kwa dhati.

Walimpongeza kwa kukamilisha miradi mikubwa haraka kuliko matarajio yao na kuzindua mipango mipya kwa kasi ya ajabu.

Vijana walisema kwa bashasha, “Hatukuamini kama miradi ya reli, barabara, na hospitali ingemalizika hivi karibuni, lakini mama kaweka mambo sawa!” Si mara ya kwanza kwa Rais Samia kushangaza, kwani ameendelea kupambana kwa ustadi na kuibua matumaini mapya katika kila sekta nchini.

Kwa vijana, Rais Samia amekuwa kiongozi anayejua mahitaji yao na mwenye dira thabiti.

Wanamwona kama mkombozi wao, aliyewapa nafasi na fursa mpya katika uchumi na ajira. Wameahidi kusimama naye, wakisema kwa furaha, “Mama endelea tu, sisi tuko hapa mpaka kieleweke!”

Ni dhahiri kuwa Rais Samia amekuwa kinara wa mafanikio haya, akivuka matarajio ya wengi kwa kutumia weledi na umakini.

Kasi ya utekelezaji wake inashangaza na inavutia, kama mvua ya baraka inayoshuka wakati wa kiangazi; kila mmoja anataka kuwa sehemu ya safari yake ya mafanikio.

Vijana wamejipanga kumpa sapoti, wakijua kuwa chini ya uongozi wake, Tanzania inazidi kung'aa.

 
Hao vijana wenyewe walivyochoka Kuna mmoja hapo na shati kashika tama haelewi
 
vijana wenye utimamu wa akili wote wanaishi kwa mwongozo wa ilani ya chama cha mapinduzi
 
Mnawajua vizuri vijanna wa kitanzania?
 
Kwanza kabsa waliokwenda kwenye maadhimisho haya wengi ni UVCCM mkuu hilo ni jambo ambalo wengi wanalifahamu hata usipokuwa na D mbili.
Hata picha zinaonesha vijana wengi waliokwenda ni UVCCM.
 
Tukatae tutakavyo lakini uhalisia ni kwamba upinzani wa kuiumiza kichwa CCM hamna. Hawa wa sasa hata mlenda una afadhali kwa ulegevu.
 
Wapinzani wanatakiwa wasimame imara, siasa za mitandaoni ambazo hazi reflect uhalisia wa wanachokiongea huku kwa wananchi kinawasababisha kuendelea kuporomoka Siku Hadi Siku

Am speaking because nipo field. Kipindi hiki tupo kwenye harakati za uchaguzi wa serikali za mitaa. Nipo huku lakini sijaona u serious wa vitendo kama walivyo wenzetu wa chama tawala..Vituo vya uandikishaji havina mawakala, ila Kuna vijana mtaani aged 17 Hadi 28 ndio wanaofanya siasa za kipinzani Vijijini ambao hata hawajui kwamba wasipojiandikisha au watu wao wasipojiandikisha hawawezi kupiga kura

Lkn there concern kura watapiga tu. Hapa ndipo tunapopoteza kura wapinzani, sio kuibiwa

Watu wetu hawapigi kura ,ila tuna idadi kubwa ya mashabiki na wanachama wasiojua Chochote kuhusu umuhimu wa kura

Upinzani wa kweli uamzie ngazi ya chini huku,then Ngazi ya juu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…