Kili Marathon kugawa barakoa kwenye Mbio zitakazofanyika mwaka huu

Kili marathon kwa Hali ilivyo isimamishwe haraka iwezekanavyo.
 
Hawaogopi kugawa hizo barakoa,maana mwenye nchi yake anasema kuvaa barakoa ni kuwatia hofu wananchi.
 
Waachwe ujinga, Kuna mtu anaweza kukimbia na barakoa??? Waachwe tamaa waahirishe marathon
 
Watanzania wengi wameshagundua Covid-19 ipo sana nchini na wanachukua tahadhari kwa kufuata ushauri wa kisayansi wa wataalam wa nchi za nje na kuachana na ushauri wa vilaza wetu wenye PhD feki. Yule Jaji wa Mahakama Kuu wa Shinyanga alifariki lakini hakuna taarifa iliyotolewa juu ya ugonjwa wake wala kifo chake bali walionyesha kwenye luninga maziko yake Kagera, cha kushangaza wengi waliohudhuria walivaa Barakoa. Mwingine ni yule Jenerali Mbena mstaafu wa Jeshi Dar es Salaam hawakutangaza kuugua kwake lakini wakaonyesha shughuli za maziko lakini washiriki karibu wote ikiwa ni pamoja na Wanajeshi waliokuwa wanabeba Jeneza walivaa Barakoa licha ya Amiri Jeshi Mkuu kuagiza kuwa hakuna Covid-19 nchi nzimà. Meya wa Moshi aliwafukuza mkutanoni wote waliovaa Barakoa kujilinda na kumlinda Mstahiki Meya, lakini kwa agizo toka juu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro anasisitiza hakuna Covid-19. Miji mingi wakazi waliokuwa wanajifukiza na kula malimao na tangawizi wamegundua haisaidii kitu wamerudia kuvaa Barakoa na kufuata tahadhari zote za kujikinga ambazo walikuwa wamezitupilia mbali kwa agizo toka juu. Civil disobedience inaanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…