Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi na Taasisi za Elimu, Ndugu Geofrey Kiliba, ametangaza kuwa atazungumza na vyombo vya habari siku ya kesho, tarehe 18 Agosti 2025
Katika taarifa yake kwa umma aliyoitoa kupitia mitandao Yake ya Kijamii leo, tarehe 17 Agosti 2025, Ndugu Kiliba ameandika:
“Panapo majaliwa, kesho majira ya saa sita mchana, nitaongea na Watanzania kupitia vyombo vya habari nikiwa kama Raia mwema na Mzalendo wa taifa langu, Tanzania.”
Kiliba amebainisha kuwa mazungumzo hayo yatagusa mambo nyeti na muhimu kwa maslahi ya taifa, huku akieleza kuwa anafanya hivyo kwa ujasiri mkubwa alioupata kwa neema ya Mwenyezi Mungu.
“Ni mazungumzo yanayohitaji ujasiri mkubwa, na kwa neema ya Mwenyezi Mungu, nimepewa na nimevaa ujasiri huo. Nimejiandaa kusema kile kinachostahili kusemwa kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu,” ameongeza.
Kiliba pia amesema kuwa eneo atakalotumia kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari litatangazwa jioni ya leo.
Akiwaasa vijana wenzake, hasa wale wanaotofautiana naye kimtazamo, Kiliba amesisitiza umuhimu wa kuvumiliana licha ya tofauti hizo, huku akitoa kauli yenye ujumbe mzito:
“NB: Ayeah wale Vijana wenzangu ambao ni wema sana lakini tunatofautiana katika Mitazamo, anzeni kujiandaa kwa mbinu mpya za ku-attack kwani Matusi, Ushauri wa kinafki na Vitisho vyote vimegonga mwamba”
Amehitimisha kwa ujumbe unaoacha tafakari:
“Huu si wakati wa kuelewana, tuvumiliane tu! Nchi Kwanza”