DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu nchini Tanzania wametangaza kuwa mabalozi wa amani na usalama wa Tanzania wakati huu ambapo Taifa linajiandaa kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ili kila Mtanzania apate haki ya kumchagua Kiongozi wamtakaye bila ya hofu ama wasiwasi kuhusu usalama na utulivu wa siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Kagera, Rais wa Jumuiya ya wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu nchini Bw. Geofrey Kiliba amesema jukumu hilo wameamua kulibeba sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujitokeza kupigakura, kwa kushirikiana na Asasi na Taasisi binafsi zinazofanya kazi hiyo ya hamasa kwa wananchi ili kuweza kushiriki kuwachagua Viongozi wa Tanzania.