Kilichofanyika Msomera hakikuwa sherehe za kimila za Wamasai, zilikuwa sherehe za CCM

Wenye umasai wao wameshasema tamasha lao halifanywi kila mahali, hilo likikuww genge la Bibi sa100 na matahira wenzake.
 
Sawa tu, kwani kuna ubaya gani? Mila zetu tangiapo ziko pamoja na za Chama, yaani CCM ni mtoto wa hizo mila.
Wewe ungekuwa huumii ungempotezea tu
 
Wamasai hawawezi kuwa wanaccm?
 
Tangua yule maza kusema katiba ya nchi ni kakitabu ...... sina hamu nao tena .... hizo maigizo ni mwendelezo tu ..... nikashangaa wamasai lini wakawa wana ccm
 
Hivi nani alikuambia kuwa Ngorongoro ndiyo eneo asilia la Wamasai? Na je unajuwa kuwa Wamasai siyo jamii ya kwanza kuhamishwa kwenye makazi waliyopo na kupelekwa sehemu nyingine kwa ajili ya manufaa mapana ya kitaifa.

Wamasai walihamishwa kutoka Serengeti mwishoni mwa miaka ya 1950 kwa amri ya Governor wa Tanganyika wakati huo.

Pili kuna jamii za wachagga zilihamishwa miaka ya 1960 kutoka Kilimanjaro kwenda Turiani.

Kuna jamii za Wasukuma huku Bulyanhulu na Wakurya huko Tarime zililamishwa kupisha machimbo ya madini.

Wamasai kwenda Msomera Handeni ni kitu cha kawaida tu
 
Hii ni hoja nyingine
 
Huenda Wamasai ni wana-CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…