Siku ya Jumamosi tarehe 11/09/2021 nikiwa mmoja wa abiria ambaye nilipandia gari Moro kuelekea Dodoma muda wa jioni gari ikiwa inatokea Dar tulipofika Dumila ghafla dereva alianguka akiwa kwenye mwendo na kupelekea gari kwenda lenyewe hadi lilipozimika na Mungu jaalia halikuwa ktk mwendo na kwa habari nilizozipata siku ya jumanne nilipopita tena pale Msamvu niliambiwa kuwa yule dereva alikufa na ameshazikwa kwao Tanga na alikuwa na matatizo ya sukari ya kushuka
Angalizo ni wamiliki kuwapa mapumziko stahiki kwa madereva wao kwani wanabeba dhamana kubwa ya roho za watu na wakati wa tukio yaani hakukuwa na dereva wa ziada na ikabidi hadi tuamishiwe ktk gari nyingine