Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
Shekhe Amri Abeid ni mmoja ya washairi maarufu Tanzania na Meya wa kwanza Mwafrika ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakiwa wamesoma wote shule moja ya Tabora.
Siku moja Moja Shekhe Amri Abeid akiwa na Shekhe Mubaarak walikuwa wakipita katika mji wa Mombasa katika kazi za kuhubiri dini, lakini ghafla akaja mwarabu mmoja aliekuwa akishughulika na uuzaji bucha na kumpiga Shekhe Abeid Kibao ambacho kilimpeleka chini na kusababisha miwani yake kudondoka na kofia kutoka kichwani.
Amri Abeid kwa upole kabisa aliokota kofia na miwani take akajifuta vumbi na kuvaa, huku Shekhe Mubaarak akimwambia kwa upole waondoke, na wakaondoka.
Miaka michache baadae Shekhe Mubaarak alipita katika eneo hilo na kukutana na mtu mmoja kipofu na mtu yule akajitambulisha kuwa yeye ndie aliyempiga Shekhe Kaluta kibao hivyo anaomba msamaha.
Shekhe Mubaaraka alimsihi sana mtu yule kumuomba mwenyezi Mungu msamaha kwani wakati akifanya kitendo kile wao walikuwa katika kazi ya kuhubiri maneno ya Mwenyezi Mungu.
Tukumbuke kwamba Shekhe Kaluta Amri Abeid ndie mtu mwenye jina la uwanja wa mpira wa Shekhe Amri Abeid wa Arusha.
Ni mtunzi wa mashairi, mtaalamu wa fasihi na lugha ya Kiswahili, Waziri, Meya wa kwanza muafrika na Mkuu wa Mkoa.