Kilichomkuta Mwarabu aliyempiga kibao Sheikh Amri Abeid

Mwandishi si mtunzi mzuri.anatunga hadith utadhani anaandikia watoto wa chekechea.toa version nyingine please.hii ni upupu tu. Kipofu alipomwona akajitambulisha kuwa yeye ndo alimpiga kibao sheikh....
 
Huyu bado mgeni tumsamehe wadau
Amejaribu, kutikisa jukwaa
 
Shekhe Amri Abeid ni mmoja ya washairi maarufu Tanzania na Meya wa kwanza Mwafrika ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakiwa wamesoma wote shule moja ya Tabora.

Siku moja Moja Shekhe Amri Abeid akiwa na Shekhe Mubaarak walikuwa wakipita katika mji wa Mombasa katika kazi za kuhubiri dini, lakini ghafla akaja mwarabu mmoja aliekuwa akishughulika na uuzaji bucha na kumpiga Shekhe Abeid Kibao ambacho kilimpeleka chini na kusababisha miwani yake kudondoka na kofia kutoka kichwani.

Amri Abeid kwa upole kabisa aliokota kofia na miwani take akajifuta vumbi na kuvaa, huku Shekhe Mubaarak akimwambia kwa upole waondoke, na wakaondoka.

Miaka michache baadae Shekhe Mubaarak alipita katika eneo hilo na kukutana na mtu mmoja kipofu na mtu yule akajitambulisha kuwa yeye ndie aliyempiga Shekhe Kaluta kibao hivyo anaomba msamaha.

Shekhe Mubaaraka alimsihi sana mtu yule kumuomba mwenyezi Mungu msamaha kwani wakati akifanya kitendo kile wao walikuwa katika kazi ya kuhubiri maneno ya Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke kwamba Shekhe Kaluta Amri Abeid ndie mtu mwenye jina la uwanja wa mpira wa Shekhe Amri Abeid wa Arusha.

Ni mtunzi wa mashairi, mtaalamu wa fasihi na lugha ya Kiswahili, Waziri, Meya wa kwanza muafrika na Mkuu wa Mkoa.
Hadithi za mtume hizo,mwarabu ampige kibao mueneza dini ya kiislam,never
 
Siyo kila mtu anao uwezo wa kuandika kitu kiufasaha.

Uandishi ni kipaji
 
1. Kwahiyo alimroga?
2. Kipofu alimtambuaje mpita njia mpaka akamfata kujitambulisha?
 
Even if the story is true, correlation does not equal causation.
 
Shekhe Amri Abeid ni mmoja ya washairi maarufu Tanzania na Meya wa kwanza Mwafrika ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakiwa wamesoma wote shule moja ya Tabora.

Siku moja Moja Shekhe Amri Abeid akiwa na Shekhe Mubaarak walikuwa wakipita katika mji wa Mombasa katika kazi za kuhubiri dini, lakini ghafla akaja mwarabu mmoja aliekuwa akishughulika na uuzaji bucha na kumpiga Shekhe Abeid Kibao ambacho kilimpeleka chini na kusababisha miwani yake kudondoka na kofia kutoka kichwani.

Amri Abeid kwa upole kabisa aliokota kofia na miwani take akajifuta vumbi na kuvaa, huku Shekhe Mubaarak akimwambia kwa upole waondoke, na wakaondoka.

Miaka michache baadae Shekhe Mubaarak alipita katika eneo hilo na kukutana na mtu mmoja kipofu na mtu yule akajitambulisha kuwa yeye ndie aliyempiga Shekhe Kaluta kibao hivyo anaomba msamaha.

Shekhe Mubaaraka alimsihi sana mtu yule kumuomba mwenyezi Mungu msamaha kwani wakati akifanya kitendo kile wao walikuwa katika kazi ya kuhubiri maneno ya Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke kwamba Shekhe Kaluta Amri Abeid ndie mtu mwenye jina la uwanja wa mpira wa Shekhe Amri Abeid wa Arusha.

Ni mtunzi wa mashairi, mtaalamu wa fasihi na lugha ya Kiswahili, Waziri, Meya wa kwanza muafrika na Mkuu wa Mkoa.

Hii hadithi ni ya kweli.

Sheikh Mubarak Ahmad, huyo alikuwa ni Mbashiri wa kwanza wa jumuiya ya Waisilamu wa Ahmadiyya kuletwa Afrika mashariki kutoka Pakistani, makao makuu ya Jumuiyya ya Waisilamu wa Ahmadiyya kipindi hicho (in 50--60s) yalikuwa yapo Kenya Nairobi, Sheikh Amri Abeid Kaluta alikuwa mbashiri wa kwanza mweusi wa jumuiya ya Waisilamu wa AhmadiyyaTanganyika.

Bila shaka masheikh hao walikuwa wakipita mitaani huko Mombasa kuhubiri dini, kama inavyofahamika, Jumuiya ya Waisilamu wa Ahmadiyya tunaamini kwamba utume usio na sheria bado unaendelea katika umma wa kiisilamu (hii ni kwa mujibu wa Qur'an na hadithi za mtukufu mtume saw), kwa imani hii inafanya wafuasi wa madhehebu mengine ya Waisilamu kuichukia jumuiya ya Waisilamu ya Ahmadiyya na hiyo ndiyo sababu ya huyo Muarabu, baada ya kuhubiriwa itikadi hiyo na kugadhibika ndipo alipompiga kibao shk Amri Abeid Kaluta.

Yawezekana baada ya miaka kupita nadhani Shk Amri Abeid wakati huo alikuwa karudi nyumbani Tanganyika ndipo Shk Mubarak akiwepo huko Kenya alienda kumtembelea huyo Muarabu kuona hatima/hali yake baada ya kitendo kibaya alichomfanyia Shk Amri ndipo akamkuta alishapofuka macho na bila shaka ni Shk Mubarak ndiye aliyejitambulisha kwa huyo Muarabu- kipofu naye akakumbuka jambo alilomfanyia Shk Amri na ndiyo maana akaomba msamaha akitambua kwamba pengine upofu wake ni adhabu ya Mungu ni kutokana na kumpiga kofi Shk Amri. (Mimi binafsi naamini hiyo ilikuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu).

Adhabu mbalimbali za mfano wa aina hiyo zimepata na bado zinaendelea kutokea kwa watu wanaoonyesha Uadui "mkali" dhidi ya Waisilamu wa Ahmadiyya.
 
Shekhe Amri Abeid ni mmoja ya washairi maarufu Tanzania na Meya wa kwanza Mwafrika ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakiwa wamesoma wote shule moja ya Tabora.

Siku moja Moja Shekhe Amri Abeid akiwa na Shekhe Mubaarak walikuwa wakipita katika mji wa Mombasa katika kazi za kuhubiri dini, lakini ghafla akaja mwarabu mmoja aliekuwa akishughulika na uuzaji bucha na kumpiga Shekhe Abeid Kibao ambacho kilimpeleka chini na kusababisha miwani yake kudondoka na kofia kutoka kichwani.

Amri Abeid kwa upole kabisa aliokota kofia na miwani take akajifuta vumbi na kuvaa, huku Shekhe Mubaarak akimwambia kwa upole waondoke, na wakaondoka.

Miaka michache baadae Shekhe Mubaarak alipita katika eneo hilo na kukutana na mtu mmoja kipofu na mtu yule akajitambulisha kuwa yeye ndie aliyempiga Shekhe Kaluta kibao hivyo anaomba msamaha.

Shekhe Mubaaraka alimsihi sana mtu yule kumuomba mwenyezi Mungu msamaha kwani wakati akifanya kitendo kile wao walikuwa katika kazi ya kuhubiri maneno ya Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke kwamba Shekhe Kaluta Amri Abeid ndie mtu mwenye jina la uwanja wa mpira wa Shekhe Amri Abeid wa Arusha.

Ni mtunzi wa mashairi, mtaalamu wa fasihi na lugha ya Kiswahili, Waziri, Meya wa kwanza muafrika na Mkuu wa Mkoa.
Wanaomdhihaki Mungu kwa makusudi huwa wanalipwa haraka sana.
 
Sio ajabu Tena Hilo Ni dogo kabisa, Kumbuka Sheikh Amri Abeid Kaluta alikuwa Ni Muislamu wa Ahmadiyya Muslim Jamaat.

Waislam wa Waahmadiyya wanaimani(itikadi) kuwa Nabii Isa/Yesu a.s hayuko Mbunguni Kama inavyoaminiwa na Waislam wengine (na wakristo pia) Bali Waahmadiyya wanaamini kuwa Nabii Isa/Yeah ameshafariki. Pia waahmadiyyah wanaamini Yule Masihi aliyetarajiwa kufika ameshafika tayari naye ndiye Muanzilishi ya Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya.

Sasa itikadi hizo mbili (Kifo Cha Isa/Yesu na Kuja kwa Masihi) huesabika Kama kufuru kwa Waislam wengine.

Na kwa sababu hii Waislam wa Madhehebu mengine mfano Suni na Shia ndio walikuwa wapinzani wakubwa wa Waislam wa Ahmadiyya pengine kuliko watu wa dini nyinginezo wakati uahmadiyya umeanza kuhubiriwa hapa nchini. Na hii ipo Hadi leo ingawa kwa hapa nchini, upinzani wa Sasa sio mkubwa Kama zamani lakini bado upo.

Baadhi ya Nchi Kama Pakistan waahmadiyyah wanauliwa na Ni kosa kisheria kwa nchi yao ukionekana unahubiri uislam wa ki Ahmadiyyah Bali hata Muislamu wa Ahmadiyya kujitambulisha tu kuwa wewe Ni Muislamu, Ni kosa ambalo haukumu yake ndogo Ni jela miaka 3. So Hilo la kupigwa kibao Ni Jambo dogo sana kwa mtu anaefahamu Hali halisi ilivyo.
 
Meya wa wapi?

Halafu ungeandika jina lote toka mwanzo
Mara Abeid mara Kaluta unachanganya
 
Back
Top Bottom