Ningeshauri,miss wa mwaka uliopita ndiye awe Miss atakayeliwakilisha taifa kwenye mashindano ya Dunia.
Namaanisha,Miss Tz 2015 awe ndiye mwakilishi kwa mwaka 2016 na Miss Tz 2016 awe maakilishi Miss World 2017.
Kwa sababu inampa muda mwingi wa kujiandaa,yapata mwaka mzima na kuangalia vipaumbele na changamoto za kukabiliana nazo anavyojiandaa kuliwakilisha taifa.
Pia kamati itapata muda wa Kumfunza na kumshauri katika project yake atakayoiandaa na wadau pia watampa ushauri ili aweze kufanya vema.
Nchi nyingi zinafanya hivyo na ndizo hujitahidi kufanya vema. Miss TZ ni ngumu kushinda kwa sababu hukaa karibia wiki moja pekee kisha huhitajika kiufika kambini kujiandaa na Miss World. Mtu huyu atapata muda upi wa kuandaa project yake ili iwe na ushawishi?
Kwa mantiki hiyo,nashauri Tanzania isiwe na Mwakilishi mwaka ujao badala yake MissTz 2017 awe mwakilishi mwaka MW 2018.
Nawasilisha.