Tetesi: Kilichomponza Balozi Adadi Rajabu hiki hapa

Tetesi: Kilichomponza Balozi Adadi Rajabu hiki hapa

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kama mtakumbuka, kipindi hiki cha miaka mitano ya utumwa ya bwana yule kulitokea upuuzi wa Polisi kukamatakamata watu hasa upinzani kipuuzipuuzi.

Kuna siku Balozi Adadi alisimama bungeni na kueleza kuwa kilichokuwa kinafanyika ni uhuni na kwamba kuna taratibu zake za kumkamata mtuhumiwa na kwamba Polisi wanazijua vyema.

Alienda mbali na kusema kuwa, huwezi kumkamata mtu kienyeji tu kwa shinikizo la wana siasa!! Kauli ile najua haikumpendeza bwana yule Na kwakuwa jamaa ni mtu wa visasi basi huu ndio ulikua muda muafaka wa kulipiza kisasi.

Mungu ibariki Tanzania

Soma

Video kutoka Maktaba: Hotuba nzuri sana ya Adadi Rajabu bungeni, tuwe na tubakie humo
 
Inatosha aache wengine wale mema ya nchi. Ashakuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kwa muda mrefu na baadae Balozi, atulie ale pension yake
 
Na yule Jamaa anayetokea Chemba aliyekuwa anang'ang'aniza Bw Mkubwa aongezewe muda mbona naye yamemkuta, ina maana nae alimuudhi Bw Mkubwa?.
 
Angalia vizuri walioteuliwa, vijana wote wenye umri wa miaka 20+ wenye shule na waliogombea na kupata kura chache wamepitishwa kugombea lengo ni kuweka damu changa katika system za chama, CCM haiwazi uchaguzi wa 2020 inawaza pia wa 2030.
 
Hahahaha hahahaha
 
Back
Top Bottom