Tetesi: Kilichomponza Diamond ni Sakata la ATCL

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza kumfungia msanii Diamond Platnumz na mwenzake Rayvanny kufanya maonesho yoyote ndani au nje ya nchi kwa muda usiofahamika. Si hivyo tu, bali pia wamelifutilia mbali Tamasha la Wasafi Festival ambalo limekuwa gumzo kubwa katika siku za hivi karibuni.

Sababu zinazotolewa na Basata, ambazo zina ushahidi wa wazi, ni kwamba msanii huyo amekiuka maelekezo aliyopewa na Basata, ya kuacha kuperform wimbo wa Nyegezi (Mwanza) uliofungiwa na Basata kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kukiuka maadili ya Kitanzania.

Tukio la Diamond kupigwa pini na Basata, limekuja muda mfupi baada ya Mbongo Fleva huyo kusababisha hali ya sintofahamu katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha 'bwa mdogo' huyo akiwatemea mbovu wafanyakazi wa uwanja huo, kwa kile alichodai kwamba wamemchezea rafu kwa kuuza tiketi alizozifanyia booking mapema na kusababisha ashindwe kusafiri kurejea Dar baada ya kumalizika kwa shoo yake jijini Mwanza.

Madai hayo yalililazimu shirika la ndege la ATCL kutoa tamko rasmi na kukanusha madai ya Diamond ambapo taarifa ilieleza kwamba hakuna aliyeuza tiketi yake isipokuwa yeye ndiye aliyefanya makosa kwa kuchelewa kufika uwanja wa ndege hivyo kwa mujibu wa kanuni na taratibu, alipoteza sifa za kusafiri na ndege hiyo hivyo kuomba kupangiwa siku iliyofuatia.

Kabla ya ATCL kutoa ufafanuzi huo, watu wengi waliotazama video hiyo, waliamini kwamba kweli ATCL wamefanya uzembe, wamepiga dili kwa kuuza tiketi ya Diamond na kundi lake kwa watu wengine, kwa lugha nyepesi Diamond aliwaaminisha watu kwamba ATCL si waaminifu kwa wateja wake na ndiyo maana wameuza tiketi ambazo zilishafanyiwa booking kwa watu wengine.

Ikumbukwe kwamba ATCL ni shirika la serikali na serikali ya awamu ya tano imewekeza nguvu kubwa kulihuisha shirika hilo lililokuwa mahututi kwa kununua ndege mpya na kulifanya sasa angalau liwe na uhai baada ya kudoda kwa muda miaka mingi. Tayari ndege tano zimeshafika nchini na zinafanya kazi na matarajio ni kuleta mashine kubwa zaidi, Airbus mapema mwezi huu.

Wakati serikali ikihangaika kuhakikisha ATCL inapata wateja wa uhakika na kujiendesha kwa faida, anatokea 'mwehu' mmoja na kuibua tuhuma ambazo zinawafanya wateja wapoteze imani na shirika hilo na hivyo kulikosesha wateja na mapato.

Diamond ambaye kwa heshima na taadhima, alialikwa wakati moja kati ya ndege hizo ikiwasili nchini, badala ya kuwa balozi wa kuwahimiza watu wengine watumie huduma za ATCL, yeye anahujumu kwa kuibua tuhuma za uongo zenye lengo la kuikosesha ATCL wateja na mapato.

Fyekelea mbali ili siku nyingine ajifunze kuwa na adabu na uzalendo! Siku zote serikali inaweza kuwa inajua kwamba unafanya makosa lakini kwa sababu hugusi maslahi yake, ikakuacha uendelee kukosea! Ndiyo, kwani Diamond ameanza kuidharau Basata leo kwa kuimba Nyegezi? Upo ushahidi wa mpaka video akiwa Zanzibar na kwingineko, alionekana akiwaimbisha mashabiki kijanja.

Kama ishu ingekuwa ni hiyo tu, Basata wangeweza kuweka pamba masikioni au kuitana kishkaji, Mngereza alikuwepo kwenye uzinduzi kule Mtwara, kwa hiyo kwao siyo adui tena bali mlezi, wangeweza kunena kwa lugha moja wakayamaliza ili kuepusha hasara ya mamilioni ambayo sasa ataipata kwa kufungiwa.

Diamond, man up! Don't mess with the government!
 
Kabla ya ATCL kutoa ufafanuzi huo, watu wengi waliotazama video hiyo, waliamini kwamba kweli ATCL wamefanya uzembe, wamepiga dili kwa kuuza tiketi ya Diamond na kundi lake kwa watu wengine, kwa lugha nyepesi Diamond aliwaaminisha watu kwamba ATCL si waaminifu kwa wateja wake na ndiyo maana wameuza tiketi ambazo zilishafanyiwa booking kwa watu wengine.

Mkuu kama unaamini walichosema ATCL na kuona live ya Diamond ni uongo basi wewe ni mtu wa kuhurumiwa sana.

Ukweli ni kwamba, Diamond was right, na ATCL walichofanya ni damage control.

KIlichofanyika ni hivi, ATCL walikuwa wamebook abiria kuliko uwezo wa ndege. Sasa inapotokea hivyo, ATCL watachukua abiria walio -check in kwnza. Hata kama umefika airport ndani ya muda wa ku-check in, kwa kuwa kuna abiria waliozidi uwezo wa ndege, wale walio check in kwanza ndio watasafiri.

Kwa hiyo katika utetezi wao, ATCL WAMEDANGANYA UMMA kwa kusema Diamond alichelewa. Diamond alifika muda unaotakiwa bali kulikuwa na overbooking ya hiyo flight.
 
Ukweli ni kwamba hata kama hao jamaa wa atcl walifanya "machezo" kwenye hilo suala kamwe wasingekubali kukiri!
Nilimsikiliza yule msemaji nikajikuta nimepa kichefu chefu, alikuwa anaongea vitu vingine ambavyo kwa kweli sidhani kama anafaa kuwepo kwenye hiyo nafasi!
...imebaki tu kuwa mond alichelewa lakini hawakusema alifika uwanjani saa ngap!
...pia msemaji yule alisema ndege iliruka saa mbili na dakika 45 kutoka Mwanza na kutua saa mbili Dar. Ina maana alishindwaje kuwa makini kwenye kutaja muda wa kuruka na kutua?
..vile vile majina aliyotaja ambayo yaliandikwa kwenye tiketi ya mond ni tofauti na majina yake halisi tunayoyafahamu, alisema tiketi ilikuwa na jina "Isack Nassib" sasa sijui kama hili ndio jina halisi la Diamond...
Kiufupi ni kuwa ukifuatilia ile speech ya msemaji wa shirika ni kuwa bado kuna maswali mengi yanabaki bila majibu...
...pengine kulikuwa na mission nyuma ya pazia iliyokuwa imepangwa na hivyo basi ikawa sehemu ya kumkamatia ndio hapo!

Picha[emoji116]mapema leo akiwa na mstaafu, kabla ya barua kutoka "basata"
Screenshot_20181218-172727_Instagram~2.jpeg
 
Mkuu kama unaamini walichosema ATCL na kuona live ya Diamond ni uongo basi wewe ni mtu wa kuhurumiwa sana.

Ukweli ni kwamba, Diamond was right, na ATCL walichofanya ni damage control.

KIlichofanyika ni hivi, ATCL walikuwa wamebook abiria kuliko uwezo wa ndege. Sasa inapotokea hivyo, ATCL watachukua abiria walio -check in kwnza. Hata kama umefika airport ndani ya muda wa ku-check in, kwa kuwa kuna abiria waliozidi uwezo wa ndege, wale walio check in kwanza ndio watasafiri.

Kwa hiyo katika utetezi wao, ATCL WAMEDANGANYA UMMA kwa kusema Diamond alichelewa. Diamond alifika muda unaotakiwa bali kulikuwa na overbooking ya hiyo flight.
Ndio maana ukifuatilia hili sakata hawakutaja muda kamili ambao Diamond alifika uwanjani...
Btw wanatetea matumbo yao tu...
 
Mkuu kama unaamini walichosema ATCL na kuona live ya Diamond ni uongo basi wewe ni mtu wa kuhurumiwa sana.

Ukweli ni kwamba, Diamond was right, na ATCL walichofanya ni damage control.

KIlichofanyika ni hivi, ATCL walikuwa wamebook abiria kuliko uwezo wa ndege. Sasa inapotokea hivyo, ATCL watachukua abiria walio -check in kwnza. Hata kama umefika airport ndani ya muda wa ku-check in, kwa kuwa kuna abiria waliozidi uwezo wa ndege, wale walio check in kwanza ndio watasafiri.

Kwa hiyo katika utetezi wao, ATCL WAMEDANGANYA UMMA kwa kusema Diamond alichelewa. Diamond alifika muda unaotakiwa bali kulikuwa na overbooking ya hiyo flight.
Natamani ungemuelewa walau kidogo mleta mada ..ingekusaidia sana .

.. Iwe tickets za wcb ziliuzwa kwa watu wengine au wcb walichelewa Ujinga alioufanya domo nikuipaka kinyesi taasisi nyeti ya serikali " kisha akakipost kinyesi chake kwenye mitandao ya kijamii ... huu ni uzwazwa mkubwa Sana ambao unapaswa kukemewa " diamond alipaswa kuwasilisha malalamiko yake katika uongozi wa ATCL ama kwenda kufungua kesi na kudai fidia .. nasio kufanya upuuzi alioufanya " ambao unapelekea kuchafua brand ya ATCL kibiashara " ... diamond ni kioo cha jamii anafuatiliwa na watu wengi inapotokea akawa na conflict na taasisi nyeti kama ATCL ni rahisi " sana kuifanya tasnia hiyo isiaminike pia itaingia hasara kwakukosa wateja " .... diamond akiwa kama icon alipaswa " kuweka uzalendo mbele nakuficha madhaifu ya ATCL asiyaonyeshe kwenye public..
.
.kisha angefuata protocol ambayo ilikuwa ni kwenda kufikisha malalamiko yake ama maoni katika uongozi husika " ..... so ule alioufanya ni ujinga " unaoweza kuligharimu shirika na kulifilisi " pia amechangia kutaka kuwavunja moyo " wafanya kazi wote wa ATCL na Raisi wa nchi ambao wamekuwa wakitumia ma billions ya fedha kuhakikisha kwamba " taasisi hii ya usafiri wa anga inaleta matumaini upya nchini na kulipatia taifa faida

Mwambieni huyo jamaa Yenu apunguze misifa itamuharibia Maisha yake

Natumai huo ni mwanzo tu " kuna vikwazo vingi toka serikalini ambavyo sio vya kupendeza " vinavyo mfuata.
 
Na kwa kukazia hapo nimeona sasa PRECISIONAIR wamatake advantage kwa kutumia picha yake kuonesha ukarimu wao...
 
Mkuu ulichokiongea ndoo ukweli.
 
Back
Top Bottom