Kilichomponza Magufuli: Hakuchukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa

Status
Not open for further replies.
Hilo linawaumiza sana watanzania kuliko anavyodhani yeye

Amefanya watanzania wamchukulie ni katili, asiyejali na asiye na utu

Kingine ni kutojali wasomi waliokosa ajira tangu 2015 na kutopandisha madaraja na mishahara ya watumishi wa umma.
Magu ni Mtu Katili mno. Ktk Uongozi wake watu waliuawa direct/indirect na hiyo ndiyo furaha yake. Magufuli pamoja na genge lake wamekuwa wakiratibu na kutekeleza mateso na mauaji ya Wakosoaji wa Serikali yake na amekuwa akiyashangilia umwagaji wa damu za watu.

Naweza sema huyu siyo Binadamu wa kawaida. Kusema tuwe tunamtanguliza Mungu ni sawa kwani kuna miungu mingine. Hivyo isiwe ni kigezo kuwa ana hofu ya Mungu.
 
Magufuli alianzisha vikundi vya watu wasiojulikana ili kutisha na kunyamazisha watu. Hawezi kuvichukulia hatua wakati anavilipa mshahara. Ni mwajiri wa hivyo vikundi. Kama hatuvipendi hivyo vikundi, tuchague mtu mwingine kuwa Rais. Kama tunavipenda hivyo vikundi, tuchague Magufuli tena.
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza..hivo wewe Meku kula kisusio teremshia na mbege ukalale. Mambo magumu waachie wengine.
 
KILICHOMPONZA MAGUFULI, HIKI HAPA​

Na, Robert Heriel

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza kwa nini sitomchagua Magufuli, nini ambacho Magufuli amekifanya kibaya mpaka asipewe nafasi ya pili kuliongoza taifa letu. Pengine hata Magufuli mwenyewe hajui kwa nini watu hawatamchagua hiyo tarehe 28/10/2020.

Siku ya Leo nitaelezea kilichomponza Magufuli mpaka kufikia akakosa kura ya Taikon na kura ya Watanzania wengine.

Niseme wazi kuwa, Rais Magufuli angeweza kuwa Rais Bora sana tena ambaye watu wangejivunia naye na kumkumbuka kizazi na kizazi kama yasingetokea baadhi ya mambo ya kutisha ndani ya nchi yetu. Lakini sio hivyo, Magufuli sio Rais Mzuri, sio Rais bora na hatakuja awe Rais bora mpaka kiama.

Rais Magufuli hata angeibadilisha Tanzania kuwa Mbinguni, hata angefanya mabomba yatoe maziwa, hata angelipa kila mtu mshahara mnono, bado kuna mambo nyeti yangemharibia.

Hakuna chenye thamani hapa duniani kama uhai wa mwanadamu. Haijalishi mwanadamu yukoje, masikini au tajiri, mwema au muovu, mwenye elimu ima asiye na elimu, kila mtu uhai wake unathamani na unastahili kuthaminiwa. Haki ya kwanza hapa duniani ni haki ya kuishi. Hata kama binadamu amefanya makosa yanayostahili adhabu ya kifo bado anayohaki ya kupewa haki zake ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za kumpa adhabu hiyo ya kifo. Sio mtu auliwe kama panya, mtu sio panya. Yaani auawe tuu kiholela.

Thamani ya uhai wa mtu ni kubwa na ndio maana kuna utaratibu wa mahakama wa kisheria wa namna ya kuadhibu watu. Na sio watu kuuawa kama panya.

Nilipishana na Magufuli na upendo wangu ulipoa kwake baada ya matukio kadhaa ya utekaji na mauaji kutokea. Sisemi nani anahusika, lakini nasema wenye jukumu la kuchukua hatua za kufanya uchunguzi na kuhakikisha ulinzi wa kila mwananchi.

Magufuli kama Rais amekuwa akimtaja Mwenyezi Mungu bila shaka akimaanisha aliyeumba mbingu na nchi. Hii inanifanya nihisi huenda anahofu ya Mungu lakini ninapofikiri suala la waliouawa na kuteka na wengine kupotea kabisa bila hatua zozote kuchukuliwa inanipa hofu. Je serikali haijali watu hao, je watu hao uhai wako haukuwa na thamani?

Pengine kuna watu walimhujumu Mhe. Rais kwa kuua watu, kuteka na wengine kuwapoteza. Lakini kama huu ndio utetezi wangu na wengine wanaofikiri kwa namna hii ili kumtetea Magufuli kuwa alihujumiwa. Swali linalokuja kwa haraka ni hili; Je Magufuli kama Rais alichukua hatua gani kuonyesha hisia zake za uchungu na kuchukua hatua za kimamlaka dhidi ya matukio hayo yakidhalimu yasiyo ya kistaarabu.

Mimi kama Taikon, licha ya kuwa kijana mdogo lakini akili yangu haipatani na kiongozi asiyejali maisha ya watu. Huwezi sikia watu wanatekwa, wanauawa, wanajeruhiwa alafu wewe kama kiongozi usichukue hatua yoyote.

Biblia inasema; Mpende jirani yako kama nafsi yako ilivyo. Binafsi siwezi sema waliouawa hawanihusu, sio ndugu zangu japo ni kweli huenda hawanihusu, na pengine sio ndugu zangu kwa ukaribu lakini kwa umbali tuna undugu wa kibinadamu. Lazima tujali hisia za watu wengine.

Magufuli kilichomponza ni mauaji, utekaji, na baadhi ya watu kujeruhiwa na watu ati wasiofahamika alafu hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Hivi watu hao walikuwa ni panya?

Binafsi niliumia na nitaendelea kuumia kama hakuna hatua zitakazochukuliwa.

Mtu azae mtoto alafu watu waitwao wasiojulikana waje waue tuu watakavyo. Unaumba kiumbe cha Mungu, wakati huwezi kuumba hata Nzi! Mtu anauawa alafu hakuna kinachofanyika utadhani amekufa panya buku. Inasikitisha.

Huwezi sema unajali watu kwa kuwanunulia mandege, sijui kuwajengea maghorofa, kujenga mabarabara, hata ungejenga pepo hapa duniani kama hujali maisha ya binadamu basi hakuna ulichokifanya.

Biblia inasema; itakufaa nini upewe dunia nzima lakini unyimwe uzima wa milele.

Kumaanisha, uhai ndio jambo la thamani kuliko chochote hapa duniani.

Uhai wa mtu ukiondoshwa ndio umeondoshwa, hata ufanyeje hauwezi kurudi. Hata ungenunua magari, hata ungejenga sijui kitu gani bado uhai uliotolewa hauwezi kurudi.

Magufuli kuna kitu unapaswa ufanye, najua wewe mwenyewe inakuumiza kuona umeshindwa kufanya wajibu wako kama Kiongozi mkubwa hapa nchini.

Chukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa. Watu hawawezi kuuawa kama Panya, mtu sio panya.

Namkubali Mhe. Rais kwa mambo mengine lakini jambo moja la kushindwa kuchukua hatua kwa waliofanya mauaji, utekaji na kuwapoteza na kujeruhi watu namuondoa kwenye viongozi bora.

Mwisho niseme; Hii dunia mtawala ni mmoja na huyo ndiye tunayemtumikia na kufuata sheria zake. Ndiye Mungu aliyeumba kila kionekanacho na kisichoonekana. Huyo ndiye hakosei, huyo ndiye tutamsapoti kwa kila jambo hata kama mambo mengine yatatuumiza sisi wenyewe. Tutaheshimiana na kupendana sisi kwa sisi kama binadamu. Tutaonyana na kuelekezana sisi kwa sisi kama binadamu kwa upendo.

Kama mtu iwe wewe, yule au mimi hatakubali kuonywa na akatumia mabavu aidha kwa cheo chake, uweza na mamlaka, au sifa nyingine ambayo Mungu amempa, akatutisha basi namwambia yeye au wewe/mimi huna la ziada na huwezi kutisha watu kwa Uovu bali watu hutishwa kwa wema kwa maana kila afanye wema na haki huogopwa na hupendwa. Na kila afanyaye uovu hudharauliwa na kuchukiwa.

Narudia; Mtu sio panya mpaka umfanyie vile utakavyo ukadhani hutachukiliwa hatua zozote. Sisi tutasema na Mungu wetu atalipa kwa wakati autakao. Kunyamaza kwetu ni kuhalalisha na kuruhusu maovu yaendelee.

Magufuli siwezi kukuchagua kwa sababu umeshindwa kuchukua hatua za waliofanya udhalimu wa roho za watu na kujeruhi watu.

Watanzania tupendane, jali maisha ya mwingine kwa maana hivyo ndivyo impasavyo mtu.

Nimemaliza, mwenye swali leo anaruhusiwa kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
Andiko bora kabisa hili................

Hongera sana Mkuu
 
muuaji no yeye mwenyewe hata BenSaa8 aliteswa mbele yake.Anajulikana hata chato kafanya uharamia mkubwa wakati akitafuta ubunge. Urais umemfikisha kwenye 40 zake.Mungu ameamua anaondoshwa one mvua lije jua.Salama yake ni kuachia kwa amani akithubutu kuiba kura indigo mwisho wake. Amepaniwa na dunia nzima.
 
Rais anania mzuri ya kuiendeleza nchi Ila matukio haya ya kutisha ilimpasa hata kukemea na wahusika kusakwa ,lakini alikaa kimya Kama mtu asiyejali; tumsamehe jamani kwani inaonyesha itamcost hiyo tarehe 28
Kabla hujatamka neno MSAMAHA hebu jaribu kuvaa viatu vya Mh Lissu. Sasa hivi anatembea kwa msaada wa vyuma mwilini mwake na si kutokana na ajali au Mapenzi ya Mungu bali kwa mikono ya Binadamu mwenzake. Upuuzi mtupu Mtu Yule kuendelea kuwa Kiongozi wa Nchi yetu.
 
Hizi tabia za kuuwana sababu ya tumbo sio za kitz. Pili mtu aliyesoma na kuelimikia ustaarabika katu hawezi uwa mtu, unauwa vipi mtu Hali nawe ni marehemu mtarajiwa hata ulindwe na shetani huwezi zuia kifo.

Unauwa usiku pekee yako mchana Siri yote ipo nje unajulikana tabu yote ya nini kubeba mizimu ya roho za watu zikutese na kizazi chako milele, thus Wana kila kitu lkn hawana amani ya moyo. Hakuna utajiri Mkubwa duniani Kama huna hatia ya damu ya mtu.

Hata waikimbie dar sababu ya roho za waliouwa zinawatesa zitawafuata popote waendaako
 
Funny enough hajawahi hata kukemea . huyu jamaa sijui walimtoa wapi?
Mwizi mwenzake wa nyumba za serikali Hadi wakawapa mahawara zao ndie aliyemuweka ili kulindana.Nyumba za serikali zimeuzwa kihuni tena kwa mkopo kwa thamani ya nyumba za nyasi kijijini.
 
Nasema na narudia kusema

Hamna uchaguzi ulotakiwa kua mgumu kwa upinzan kama huu 2020, ukweli nikwamba, upinzani tulikua hatuna cha kusemea na wakumsimamisha...

Miezi mitatu ya kwanza ya Magufuli alitukaba kwelikweli.

Lkn Mungu akiwa kapanga kapanga, Siku ya kufa nyani miti huteleza yote.

Serikali ya magufuli ikaanza kuteka watu. Ikaanza kuua watu, ikaanza kutesa na kuumiza watu, wasanii , wafanyabiashara, serikali ikaanza kua ya Dharau, ikawaumiza wafanyabiashara, wafanyakazi kwa makisudi, hamna nyongeza za.mshahara, watu wakabomolewa nyumba zao bila malipo.,upinzani ukaonewa kwelikweli, waandishi wa habari wakaumizwa,, Clouds wakavamiwa, watu wakamfunguliwa makesi ya ajabu ajabu, watu wakafilisiwa, watu wakatolewa kazin...... MWISHO WAKAMPIGA TUNDU LISSU RISASI.....
MBAYA ZAIDI WANAENDELEA KUMPIGA, KUMUUMIZA NA KUMNYANYASA ..

Ni mpumbavu pekee, yaan ni mpumbavu pekee atakayeichagua CCM.
Nilkona mjumbe moja akisema kuwa kushinda ccm hakutegemei haki wala kweli ya Mungu. Ni lazima ccm itawale. Nikaona mwingine wa kutoka Zenji aliyesema kuwa hatuwezi kubadilisha utawala kwa kuweka alama ya V kwenye vikaratasi. Mwingine akasema lazina Magufuli atawale miaka yake 10. Hawa wote ni watu wakubwa huko kwenye system. Wameapa kuwa lazima iwe kwa udi au kwa uvumba. Kazi kwenu Wapinzani.
 
Rais anania mzuri ya kuiendeleza nchi Ila matukio haya ya kutisha ilimpasa hata kukemea na wahusika kusakwa ,lakini alikaa kimya Kama mtu asiyejali; tumsamehe jamani kwani inaonyesha itamcost hiyo tarehe 28
Tumsamehe wakati huu ambapo anaomba kura?
Kashindwa kutetea uhai wetu atupishe
Halafu ikimcost ndio vizuri zaidi sababu sisi alishatucost sana.
 
Ukiwasomesha watu namba nao watakusomesha namba pia hii ni kanuni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom