Kilichomponza Magufuli: Hakuchukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa

Kilichomponza Magufuli: Hakuchukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa

Status
Not open for further replies.
Rais anania mzuri ya kuiendeleza nchi Ila matukio haya ya kutisha ilimpasa hata kukemea na wahusika kusakwa ,lakini alikaa kimya Kama mtu asiyejali; tumsamehe jamani kwani inaonyesha itamcost hiyo tarehe 28
Nivigumu tayari kesi imekabidhiwa kwa raia ili tarehe 28 atowe hukumu hatari mno.
 
Mkuu ulitegemea kweli mhusika mkuu wa kupotea kwa Watanzania, kubambikiwa kesi na hata kuuawa achukue hatua dhidi ya maovu ambayo yeye mwenyewe ameamuru yafanyike? Angalia shambulizi la Lissu hakuna uchunguzi zaidi ya miaka mitatu sasa, akamnyima pesa zake chungu nzima za matibabu utadhani alitakiwa azitoe mfukoni mwake, bado haikutosha akampora na Ubunge wake mchana kweupe, Unadhani mhusika Mkuu anaweza kweli kukemea maovu yake?
Na, Robert Heriel

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza kwa nini sitomchagua Magufuli, nini ambacho Magufuli amekifanya kibaya mpaka asipewe nafasi ya pili kuliongoza taifa letu. Pengine hata Magufuli mwenyewe hajui kwa nini watu hawatamchagua hiyo tarehe 28/10/2020.

Siku ya Leo nitaelezea kilichomponza Magufuli mpaka kufikia akakosa kura ya Taikon na kura ya Watanzania wengine.

Niseme wazi kuwa, Rais Magufuli angeweza kuwa Rais Bora sana tena ambaye watu wangejivunia naye na kumkumbuka kizazi na kizazi kama yasingetokea baadhi ya mambo ya kutisha ndani ya nchi yetu. Lakini sio hivyo, Magufuli sio Rais Mzuri, sio Rais bora na hatakuja awe Rais bora mpaka kiama.

Rais Magufuli hata angeibadilisha Tanzania kuwa Mbinguni, hata angefanya mabomba yatoe maziwa, hata angelipa kila mtu mshahara mnono, bado kuna mambo nyeti yangemharibia.

Hakuna chenye thamani hapa duniani kama uhai wa mwanadamu. Haijalishi mwanadamu yukoje, masikini au tajiri, mwema au muovu, mwenye elimu ima asiye na elimu, kila mtu uhai wake unathamani na unastahili kuthaminiwa. Haki ya kwanza hapa duniani ni haki ya kuishi. Hata kama binadamu amefanya makosa yanayostahili adhabu ya kifo bado anayohaki ya kupewa haki zake ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za kumpa adhabu hiyo ya kifo. Sio mtu auliwe kama panya, mtu sio panya. Yaani auawe tuu kiholela.

Thamani ya uhai wa mtu ni kubwa na ndio maana kuna utaratibu wa mahakama wa kisheria wa namna ya kuadhibu watu. Na sio watu kuuawa kama panya.

Nilipishana na Magufuli na upendo wangu ulipoa kwake baada ya matukio kadhaa ya utekaji na mauaji kutokea. Sisemi nani anahusika, lakini nasema wenye jukumu la kuchukua hatua za kufanya uchunguzi na kuhakikisha ulinzi wa kila mwananchi.

Magufuli kama Rais amekuwa akimtaja Mwenyezi Mungu bila shaka akimaanisha aliyeumba mbingu na nchi. Hii inanifanya nihisi huenda anahofu ya Mungu lakini ninapofikiri suala la waliouawa na kuteka na wengine kupotea kabisa bila hatua zozote kuchukuliwa inanipa hofu. Je serikali haijali watu hao, je watu hao uhai wako haukuwa na thamani?

Pengine kuna watu walimhujumu Mhe. Rais kwa kuua watu, kuteka na wengine kuwapoteza. Lakini kama huu ndio utetezi wangu na wengine wanaofikiri kwa namna hii ili kumtetea Magufuli kuwa alihujumiwa. Swali linalokuja kwa haraka ni hili; Je Magufuli kama Rais alichukua hatua gani kuonyesha hisia zake za uchungu na kuchukua hatua za kimamlaka dhidi ya matukio hayo yakidhalimu yasiyo ya kistaarabu.

Mimi kama Taikon, licha ya kuwa kijana mdogo lakini akili yangu haipatani na kiongozi asiyejali maisha ya watu. Huwezi sikia watu wanatekwa, wanauawa, wanajeruhiwa alafu wewe kama kiongozi usichukue hatua yoyote.

Biblia inasema; Mpende jirani yako kama nafsi yako ilivyo. Binafsi siwezi sema waliouawa hawanihusu, sio ndugu zangu japo ni kweli huenda hawanihusu, na pengine sio ndugu zangu kwa ukaribu lakini kwa umbali tuna undugu wa kibinadamu. Lazima tujali hisia za watu wengine.

Magufuli kilichomponza ni mauaji, utekaji, na baadhi ya watu kujeruhiwa na watu ati wasiofahamika alafu hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Hivi watu hao walikuwa ni panya?

Binafsi niliumia na nitaendelea kuumia kama hakuna hatua zitakazochukuliwa.

Mtu azae mtoto alafu watu waitwao wasiojulikana waje waue tuu watakavyo. Unaumba kiumbe cha Mungu, wakati huwezi kuumba hata Nzi! Mtu anauawa alafu hakuna kinachofanyika utadhani amekufa panya buku. Inasikitisha.

Huwezi sema unajali watu kwa kuwanunulia mandege, sijui kuwajengea maghorofa, kujenga mabarabara, hata ungejenga pepo hapa duniani kama hujali maisha ya binadamu basi hakuna ulichokifanya.

Biblia inasema; itakufaa nini upewe dunia nzima lakini unyimwe uzima wa milele.

Kumaanisha, uhai ndio jambo la thamani kuliko chochote hapa duniani.

Uhai wa mtu ukiondoshwa ndio umeondoshwa, hata ufanyeje hauwezi kurudi. Hata ungenunua magari, hata ungejenga sijui kitu gani bado uhai uliotolewa hauwezi kurudi.

Magufuli kuna kitu unapaswa ufanye, najua wewe mwenyewe inakuumiza kuona umeshindwa kufanya wajibu wako kama Kiongozi mkubwa hapa nchini.

Chukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa. Watu hawawezi kuuawa kama Panya, mtu sio panya.

Namkubali Mhe. Rais kwa mambo mengine lakini jambo moja la kushindwa kuchukua hatua kwa waliofanya mauaji, utekaji na kuwapoteza na kujeruhi watu namuondoa kwenye viongozi bora.

Mwisho niseme; Hii dunia mtawala ni mmoja na huyo ndiye tunayemtumikia na kufuata sheria zake. Ndiye Mungu aliyeumba kila kionekanacho na kisichoonekana. Huyo ndiye hakosei, huyo ndiye tutamsapoti kwa kila jambo hata kama mambo mengine yatatuumiza sisi wenyewe. Tutaheshimiana na kupendana sisi kwa sisi kama binadamu. Tutaonyana na kuelekezana sisi kwa sisi kama binadamu kwa upendo.

Kama mtu iwe wewe, yule au mimi hatakubali kuonywa na akatumia mabavu aidha kwa cheo chake, uweza na mamlaka, au sifa nyingine ambayo Mungu amempa, akatutisha basi namwambia yeye au wewe/mimi huna la ziada na huwezi kutisha watu kwa Uovu bali watu hutishwa kwa wema kwa maana kila afanye wema na haki huogopwa na hupendwa. Na kila afanyaye uovu hudharauliwa na kuchukiwa.

Narudia; Mtu sio panya mpaka umfanyie vile utakavyo ukadhani hutachukiliwa hatua zozote. Sisi tutasema na Mungu wetu atalipa kwa wakati autakao. Kunyamaza kwetu ni kuhalalisha na kuruhusu maovu yaendelee.

Magufuli siwezi kukuchagua kwa sababu umeshindwa kuchukua hatua za waliofanya udhalimu wa roho za watu na kujeruhi watu.

Watanzania tupendane, jali maisha ya mwingine kwa maana hivyo ndivyo impasavyo mtu.

Nimemaliza, mwenye swali leo anaruhusiwa kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mkuu ulitegemea kweli mhusika mkuu wa kupotea kwa Watanzania, kubambikiwa kesi na hata kuuawa achukue hatua dhidi ya maovu ambayo yeye mwenyewe ameamuru yafanyike? Angali shambulizi la Lissu hakuna uchunguzi zaoidi ya miaka mitatu, akamnyima pesa zake chungu nzima za matibabu utadhani alitakiwa azitoe mfukoni mwake, bado haikutosha akampora na Ubunge wake mchana kweupe, Unadhani mhusika Mkuu anaweza kweli kukemea maovu yake?
Yote yanakwenda kuisha tarehe 28 mwanaume amesharuka viuzi vingi sana
IMG_20201014_194645.jpeg
 
Rais anania mzuri ya kuiendeleza nchi Ila matukio haya ya kutisha ilimpasa hata kukemea na wahusika kusakwa ,lakini alikaa kimya Kama mtu asiyejali; tumsamehe jamani kwani inaonyesha itamcost hiyo tarehe 28
Dhana ya kiongozi kuwaletea watu maendeleo ni ya kijima sana na kidikteta. Kiongozi wa kweli ni yule anayewawekea wananchi mazingira ya kujiletea maendeleo wenyewe.
 
Mkuu ulitegemea kweli mhusika mkuu wa kupotea kwa Watanzania, kubambikiwa kesi na hata kuuawa achukue hatua dhidi ya maovu ambayo yeye mwenyewe ameamuru yafanyike? Angalia shambulizi la Lissu hakuna uchunguzi zaidi ya miaka mitatu sasa, akamnyima pesa zake chungu nzima za matibabu utadhani alitakiwa azitoe mfukoni mwake, bado haikutosha akampora na Ubunge wake mchana kweupe, Unadhani mhusika Mkuu anaweza kweli kukemea maovu yake?
Maji yapo kwenye meno Magu ....siwezi kusahau alishasema laivu "Mimi mtu kama ananishauri anakua ameshapoteza bure" badae anapiga magoti tumpigie kura yani full of contradictions .
 
Ama neno HAKI haliko kwenye kamusi yake kichwani au analielewa tofauti. Pili good governance endelevu ni tatizo kwake.
Kuna mzee alipata kuandika kwamba kama mtu hajui utawala basi asitafute uongozi!
 
Rais Magufuli ndiye Rais. Wengine wanapoteza muda tu. Nchi hii inahitaji viongozi shupavu na wazalendo hasa, wenye uchungu hasa na taifa lao sio mawakala na vibaraka wa mabeberu.
Safi sana kiongozi
 
Ogopa sana Mtu ambaye hathamini utu wake kwa kujiita kichaa na jiwe, ogopa sana mtu asiyemuheshimu mama yake na kuongea hadharani kwamba atamgawa mama yake kwa jamaa, mama yake ambaye yuko hoi bin taabani kwa kipindi kirefu sasa.
Maji yapo kwenye meno Magu ....siwezi kusahau alishasema laivu "Mimu mtu kama ananishauri anakua ameshapoteza bure" badae anapiga magoti tumpigie kura yani full of contradictions .
 
Ogopa sana Mtu ambaye hathamini utu wake kwa kujiita kichaa na jiwe, ogopa sana mtu asiyemuheshimu mama yake na kuongea hadharani kwamba atamgawa mama yake kwa jamaa, mama yake ambaye yuko hoi bin taabani kwa kipindi kirefu sasa.
hahahahaha............lakini mkuu mimi naona Kosa kubwa la kiufundi ilifanya Tume ya uchaguzi nikuweka campaign period iwe 60days yani hata wangesema tuu 1 week Mh Lissu angefanikiwa kuizima CCM .....wangesema Campaign iwe siku moja tuu...
 
Magufuli amekosa utu kwa kiasi kikubwa mno!
kiongozi yeyote anayejiapiza kukomoa na kukejeli raia hafai , huyu iko video inamuonyesha akijinasibu kwamba akiwa Rais wananchi watalimia meno , badala apiganie hali nzuri kwa wananchi wake yeye anataka wananchi wateseke ! aibu ! kingine ni dhuluma za kishamba sana na za aibu , wafanyabiashara wamedhulumiwa waziwazi , hatuna haja ya kurudia kusimulia , lakini amedhulumu hata wahanga wa majanga , zikiwemo maiti za MV Nyerere , yale si majeneza ya kuzikia marehemu , hata kama walikuwa makapuku , nina uhakika Mungu atamlipa huyu kwa kadri ya matendo yake.

Laana kubwa sana iwapate wote waliomleta madarakani pamoja na vizazi vyao vyote
 
Hata kama Lissu hatashinda kutokana na wizi wa kutisha na hata kama Chadema itaporwa Wabunge wake walioshinda kihalali. Watanzania na dunia tumeiona nguvu ya Chadema nchini ambayo nadhani itawapa motisha mkubwa sana Viongozi wake. Na uchaguzi huu Lissu kishasema kama kukiwa na figisu dhidi ya mawakala wake za namna yoyote ile basi hatakubali matokeo maana yake tutakuwa na Serikali haramu. Iweje ushindi wa Mbunge uweze kupingwa mahakamani lakini wa Urais hauruhusiwi kupingwa?
hahahahaha............lakini mkuu mimi naona Kosa kubwa la kiufundi ilifanya Tume ya uchaguzi nikuweka campaign period iwe 60days yani hata wangesema tuu 1 week Mh Lissu angefanikiwa kuizima CCM .....wangesema Campaign iwe siku moja tuu...
 
Hata utu, hekima wala busara. Abaki tu kuburuza familia yake ila si Taifa la Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom