Kilichomponza Magufuli: Hakuchukua hatua kwa waliohusika na mauaji, watekaji na waliopotezwa

Status
Not open for further replies.
Baada ya 28 October ,mtaanza kulalamika Maguful lazima ashinde kwa kishindo kikubwa sana Mungu ameona kazi njema na mambo aliowafanyia watanzania
 
kweri kabisa mkuu ..kwanza huyu mgeni Dr Laz kutoka Malawi uraisi aliupatia baada ya mahakama kubatilisha uchaguzi wamwanzo ...mimi Mh Lissu nakubariana naye kama noma iwe noma sio habari za akina Lowassa eti "nyie munajua ,wenyewe wanajua na mungu anajua nilishinda basi tumuachie mungu" haki itakua streets tuu
 
Mtoto unamzaa, unamlea kwa tabu na shida. Kama kuna Wazazi humu, wanajua shida za malezi mpaka kuwa mtu mzima
Then mchana wa Jua Kali, watu wasiojulikana wanampiga Risasi zaidi ya 38, binadamu mwenzao eti wamepishana mtazamo kuhusu jambo Fulani.

Yaani mijitu Fulani ndiyo inaamua huyu aishi yule asiishi as if yenyewe ndiyo ilibeba mimba na ikaenda 'leba' kuzaa, alafu mijitu hiyo kila jumapili inashiriki meza ya bwana(Sacrament) huku mioyo yao na mikono yao imejaa damu na visasi.

Kwenye hili naunga mkono hoja, hakuna kumpigia kura tena, Vinginevyo aseme kile kikundi cha wasiojulikana ni akina nani, na walikuwa wanatumwa na nani?

Tukifanya makosa tena kama 2015, hao wasiojulikana ndiyo wataendelea kutuua, kututeka zaidi ya walivyokuwa wakifanya miaka hii 5 ya awamu ya 5
 
Kiukweli meco hajali maisha ya watu watu wanao msapot ni wale wanao nufaika nae tena wachache sana
Meko hana huruma kabsa wala utu we angalia kilichotokea bukoba watu wamepta majnga yy anajidai eti silet msaada wowote kwe huo ni ibinadam kwel hapan sio haki roho iliniuma san
 
Tuna rais wa hovyo sana nw, unakaa unajiuliz hyu mtu nafasi nyeti kama hii kaipataje sipati jibu,sijui ngekewa au bahati ? Ila kiukweli magu ana bahati eti nae ni rais hahahahahah
 
Mwenyezi Mungu akusimamie katika msimamo wako huu, tupo nyuma yako. Aisee
 
Dah!..haya matukio ya utekaji, kupotezwa na kushambuliwa kwa raia wema yaliiletea nchi yetu huzuni sana na kuchafua sifa yetu nzuri.

Raia walipaza sauti hata ardhi na mbingu zilisikia hivyo watu waliohusika na yale matukio hawatapata amani nafsini mwao kamwe.
 
Rais Magufuli ndiye Rais. Wengine wanapoteza muda tu. Nchi hii inahitaji viongozi shupavu na wazalendo hasa, wenye uchungu hasa na taifa lao sio mawakala na vibaraka wa mabeberu.
Wakala na vibaraka wa mabeberu ni CCM
Ambayo Magufuli amekuwa akilia lia kwamba tumechezewa sana.

Ccm ndiyo imeshika uongozi nyakati zote na hiyo michezo ya mabeberu wameicheza wao

Hata mheshimiwa Rais wetu, huyu huyu mpaka anaondoka huenda michezo yake na mabeberu wake ikajulikana

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mtu mwenye hofu kubwa ya Mungu nimkosaji mkubwa. Hofu yake ni juu ya hukumu atakayopata akisha kufa.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
kuna msemo unasema;

Hata ufanye mazuri kiasi gani!! kamwe huwezi kupendwa na watu wote...lazima watakuwepo wachache watakusema vibaya na kukuchukia na kukuzushia mabaya.
msemo huo unaweza kuthibitishwa na kila mmoja wetu ktk nafasi yake alipo, hiyo ndio hulka ya binaadamu, sio rahisi ukasemwa vizuri na watu woteee.

uzushi na uzandiki ni sehemu ya sera za watu wachache wanao mchukia bila sababu lkn hizo ni kelele za churaaa......au kelele za mlango..........

kwa asilimia kubwa Magufuli ametenda mengi mazuri kwa wananchi wanyonge na kwa wanchi wote kwa ujumla, kamwe hatuwezi kumbeza.

kuna msemo wa kiswahili unasema;

mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Magufuli anastahili kutunzwa trh 28/10 kwa kupewa kura za heshima.

watanzania wenzagu shime!! trh 28/10 saa 11 asubuhi tuwahi kupiga kura ili tuwathibitishie mabeberu na vibaraka wao kuwa Magufuli ni kwa ajili ya watanzania
 
Acha kujipendekeza, unazungumzia wanyonge gani wewe? Hawa waliobomolewa nyumba zao bila fidia? Hawa ambao wamekosa nyongeza mishahara kwa miaka mitano kwa mjibu wa sheria? Hawa waliodhulumiwa korosho zao? Hawa waliouziwa kikaratasi kwa 20, 000? Magufuli hafai, ni mtu wa visasi, kiburi, muuaji.
 
Hakuna asiyemheshimu . Mleta mada amezungumzia wasiojulikana, utekaji na mauaji ya watu wenye mtazamo tofauti naye. Wewe hapo unasemaje ?!.
 
Tanzania haijawahi kuwa Raisi mkatili mwenye roho ya ukatili kama jiwe yeye anaona wote wanamkosoa ni maadui hawatakiwi kuishi kabisa anasahau mwenye mamlaka ya kutoa hukumu ni Mungu tuu walikuwepo viongozi wakatili kuliko yeye leo wako wapi ?mshahara wa dhambi ni mauti
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…