Kilichomuondoa Mulugo.....

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Kilichomwondoa unaibu Waziri Elimu mhe. Hamim Agustino Philipo Mulugo nini...? Kuna wengi tulimpima na kumwona ni mchapakazi mzuri ukilinganisha na Waziri wake Dr. Shukuru Kawambwa. Hata hivyo, inasemekana Mulugo baada ya kuboronga kwenye ili Hotuba yake ya "Tanzania Kuuundwa na Tanganyika na Zanzibar na Zanzibar Kuuundwa na visiwa vya Pemba na Zimbabwe", sio tu ilimkosesha Amani Waziri wake,Bali pia Mkuu aliyemteua na kuonekana Uteuzi wa watendaji wakuu katika Serikali hii haupo makini na haufanyiwi upekuzi "vetting" ya kina wa kujua sifa na undani wa wale wanaoteulliwa kwenye majukumu nyeti. Itakumbukwa kuwa hata baada ya kutoa Hotuba ya hivyo, Mulugo aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari akijitetea kienyeji kuhusu udhaifu Wa kushindwa kutoa Hotuba yenye mashiko na kutumia kiingereza kizuri. Wengi walihoji, inakuwaje mhe. Rais alimteuwa Waziri ambae hata historia ya nchi yake wala lugha haijui.

kwa suala la kiingereza, japonica sio Lugha yetu ya Taifa, Mulugo alionekana kanjanja kutokana na nafasi aliyokuwa nayo na wasifu. Kama Waziri kujua lugha ni muhimu sana hasa kwa kutilia maanani Watu ambao Waziri hukutana nao na ziara anazofanya nje ya Tanzania. Mulugo pia kwa kudai kwake kuwa yeye ni mwalimu wa Sekondari, swala kutojua kiingereza lilimuondolea Sifa za kwamba alifanya kazi au anataaluma ya ualimu. Pamoja na kasi kuwa aliyokuwa nayo hasa ya kuzifungia na kuwachukulia hatua za nidhamu watendaji wa shule Kama mlivyomwona Mara nyingi kupitia vyombo vya habari, bado Mulugo hakuweza kumfurahisha Waziri wake na hata Yule aliyemteua.
 
Ivo Mulugo alikuwa hajui kiingereza au hakujua muungano wa Tanzania Ni nchi ipi na ipi ilihusika. Tatizo sio lugha hapa. Tatizo Ni umakini
 


Ili kufidia mapungufu yake kitaaluma ndio maana alikuwa mtu wa kutumia nguvu nyingi, ziara nyingi, vitisho kibao na kupenda makuu; nafahamu kuna siku alitembelea Chuo cha Ualimu Vikindu Dar es Salaam na akawafokea wakufunzi pale eti kwa nini hawakusimama kumsalimia alipofika kutembelea chuo hicho bila kutoa taarifa hata kwa mwenyeji wake mkuu wa Chuo. Jitu limbukeni tu ambalo kupata uwaziri lilijiona limekuwa Raisi na kwamba kila mtu alistahili kulijua. Good riddance.

Nakiri uteuzi Jenister Mhagama; kwa kigezo cha jinsi dada huyo anavyoendesha bunge kila anapokuwa Mwenyekiti na kumuondoa Hamim Mulugo kwenye baraza la mawaziri ni moja ya hatua zilizonifurahisha sana japo furaha yangu ilikuwa short lived baada ya kuona kwamba wakati huo huo Raisi alikuwa amewateua wapuuzi wengine kama Juma Nkamia na Mwigulu Nchemba kuwa manaibu waziri!!! unaruka tope unakanyaga kinyesi!
Huo ndio umakini wa serikali nya CCM.

God save this country.
 
Kwa uandishi huu, kuna watu wengi tu wa aina ya Hamim, ila labda tofauti ni kwamba tu wao hawajapewa uwaziri!
 
kati ya watu wajinga na wasiokuwa na akili hata kidogo ni mlugo,kuteuliwa kuwa waziri kulimshangaza kila mtu hapa mbeya,ukwrli ni kwamba elimu yake pale songea alipata ziro,na hata wahindi walimpa kazi ya kufundisha kwa sababu alikuwa tayari kulipwa mshahara wa kijinga kabisa,alivyo fanya mpaka wahindi wakampa usimsmizi wa hiyo shule wanajua walimua aliokuwa nao pale,ambao waliamua kukimbia kuponya maisha yao,baada ya kupata hiyo nafasi alikuwa akipiga walimu wakofi mbele ya wanafunzi,na nyie walimu alowapiga acheni ujinga jitokezeni mmburuze maakamani,huyu ndo akapewa uwaziri unategemea nini? heti kisa aligharamia ziara ya rizione huku mbeya,upumbavu mtupu,hadi kwa uteuzi how comes unampa mtu borgas kama huyu kuongoza sector nyeti kama elimu.
 
Kwa uandishi huu, kuna watu wengi tu wa aina ya Hamim, ila labda tofauti ni kwamba tu wao hawajapewa uwaziri!

Kaka hili suala hata mimi huwa linanishangaza mtu anaandika habari fupi ila ina makosa mengi! Sijui ni haraka au ndio div 5? Tuwe tuna edit thread zetu kabla hatuja ziposti. Inakera jamani!
 
Kaka hili suala hata mimi huwa linanishangaza mtu anaandika habari fupi ila ina makosa mengi! Sijui ni haraka au ndio div 5? Tuwe tuna edit thread zetu kabla hatuja ziposti. Inakera jamani!

Ni teknolojia imechanganya herufi...auto edit kwenye Ipad inaweza kukudhalilisha wakuu..
 
mleta uzi na hamimu wote ni walewale waliokunywa uji wa mgonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…