ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Kilichomwondoa unaibu Waziri Elimu mhe. Hamim Agustino Philipo Mulugo nini...? Kuna wengi tulimpima na kumwona ni mchapakazi mzuri ukilinganisha na Waziri wake Dr. Shukuru Kawambwa. Hata hivyo, inasemekana Mulugo baada ya kuboronga kwenye ili Hotuba yake ya "Tanzania Kuuundwa na Tanganyika na Zanzibar na Zanzibar Kuuundwa na visiwa vya Pemba na Zimbabwe", sio tu ilimkosesha Amani Waziri wake,Bali pia Mkuu aliyemteua na kuonekana Uteuzi wa watendaji wakuu katika Serikali hii haupo makini na haufanyiwi upekuzi "vetting" ya kina wa kujua sifa na undani wa wale wanaoteulliwa kwenye majukumu nyeti. Itakumbukwa kuwa hata baada ya kutoa Hotuba ya hivyo, Mulugo aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari akijitetea kienyeji kuhusu udhaifu Wa kushindwa kutoa Hotuba yenye mashiko na kutumia kiingereza kizuri. Wengi walihoji, inakuwaje mhe. Rais alimteuwa Waziri ambae hata historia ya nchi yake wala lugha haijui.
kwa suala la kiingereza, japonica sio Lugha yetu ya Taifa, Mulugo alionekana kanjanja kutokana na nafasi aliyokuwa nayo na wasifu. Kama Waziri kujua lugha ni muhimu sana hasa kwa kutilia maanani Watu ambao Waziri hukutana nao na ziara anazofanya nje ya Tanzania. Mulugo pia kwa kudai kwake kuwa yeye ni mwalimu wa Sekondari, swala kutojua kiingereza lilimuondolea Sifa za kwamba alifanya kazi au anataaluma ya ualimu. Pamoja na kasi kuwa aliyokuwa nayo hasa ya kuzifungia na kuwachukulia hatua za nidhamu watendaji wa shule Kama mlivyomwona Mara nyingi kupitia vyombo vya habari, bado Mulugo hakuweza kumfurahisha Waziri wake na hata Yule aliyemteua.