Kilichonifanya nikaacha kuvaa suruali za kitambaa

Kuna kipindi nilinunua suruali ya kitambaa nikaona ni pana mno nikaenda kwa fundi aninyongee ibane kidogo!
Siku nimeivaa niko town naruka mtaro ile kutua tu ngoma ikachanika kuanzia matakoni hadi kwenye zipu ya mbele
Nilibaki nimesimama vilevile kama askari kwenye gwaride
Nikaita boda ikanifuata mpaka nilipo nikapanda chap kama flash aliponishusha getini kwangu nilishuka kama flash nikiwa wima nikampa nauli
Ila yule boda alibaki kunishangaaa sana wakati anaondoka
 
Duh so uliingia gharama sana usafiri, au haikua mbali sana na home?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…