Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kinachomsumbua Mjengwa ni njaa tu.......Ukiwa na njaa huna mawazo huru!
Kama kazi ya kuandika balanced news umeshindwa muombe Muhingo uingie kwenye Team ya Campaign!
Maggid,
Wakati mwalimu Nyerere alipoona mzee Malecela haendi vizuri wala hakusita kumtaja hadharani wakati huo Malecela akiwa waziri mkuu na hadharani hapo hapo akamshauri rais amuondoe madarakani na ikafanyika hivyo, ili kulinda heshima ya CHAMA. Na si hivyo tu alimtungia na kitabu na mpaka leo kinasomwa na kila mmoja. Kulinda heshima ya CHAMA.
Hii unayotaka kutuambia ni ubabaishaji uliotufikisha hapa tulipo. Mtu kafanya sabotage eti asisemwe hadharani? Mtu kashusha heshima ya chama sirini eti asisemwe hadharani? Wewe unajua heshima ya Dr Slaa imeletwaje? Kusema hadharani bila kificho. Ukiiba mali ya umma wasemwa hadharani, ebu niambie sasa, mbona yeye kasemwa hadharani kwa kisa cha mchumba? Acha hizo bana!
Na wewe Maggid wajuaje kwamba mpaka anamtaja hadharani bado vikao vya ndani vya chama havijafanyika? Ukifanya ujinga wacha jamii ikufahamu na hata watoto wako na familia yako wakufahamu na upate hukumu ya haki.

Omarilyas,Kaka natumai Dr Slaa atakuwa tayari kumtaja hadharani yule kiongozi wa CHADEMA kule Kigoma ambako amekuwa mbele kusabotage kampeni za mgombea wao na pia atamtaja aliyemhonga zile milioni kadhaa ili mgombea huyo aanguke.....
Msameheni maana hao wengine hakuwasikia ila amemsikia Dr Slaa tu maana yeye uishi Iringa tu, na kuripoti mambo ya Iringa tu.Ndugu yangu Maggid,
Katika cases hizo mbili za Lipumba na JK sijakusikia ukisema umeshitushwa, ila Dr. Slaa kumtuhumu Mwenyekiti wa CHADEMA (mkoa) imekuwa nongwa?
Maggid, hiyo habari ya kuogopa kudhalilishana ndiyo iliyoifikisha nchi yetu hapa. Kama wewe umeona kwamba uliyoelezea ni mapungufu basi umekosea. kwa kiasi kikubwa hiyo ni strength ya Dr Slaa kwamba hana muda wa kumwangalia mtu usoni. Anayevurunda anashughulikiwa instantly. Na huyo ndiye kiongozi tunayemtaka. Siyo kiongozi anayesema akikamata mafisadi nchi intatikisika. What a shame. Hongera Dr Slaa kwa kuonyesha ujasiri huo bila unafiki.
Hapa ni kama yale ya Ilala enzi zile. Hii ya leo ni kama vile mtu unatembea kwa miguu peke yako kutoka viwanja vya Jangwani kupandisha kwenda Magomeni Mapipa. Juu mlimani unakutana na umati wa watu wanashuka kwa miguu kutoka Magomeni Mapipa kwenda Viwanja vya Jangwani. Ni lazima utasababisha majadiliano kwa wanaoshuka jangwani. Na hiii ndio staili ninayoitumia hapa katika kuamsha fikra.
Katika Uchaguzi wa mwaka 2005 niliandika makala kwenye Rai kuwakemea wale waliokuwa wakimbagua Dr Salim kutokana na rangi yake. Niliamini na bado naamini kuwa hawakumtendea haki. Dr Salim ni Mtanzania mwenzetu, hakukuwa na sababu za kuja na hoja za uhizbu na mengineyo.
Kuna mwandishi wa habari akaandika makala kwenye gazeti moja la kila wiki kunizushia mambo ya uongo yenye sura ya uchochezi. Aliandika mambo ya kunigombanisha mimi na wenyeji wa Iringa wa kabila la Wahehe. Ilikuwa ni stori ya uongo toka mwanzo hadi mwisho. Na kibaya zaidi mwandishi yule akafikia hata kutoa nukuu ya niliyoyaandika kwenye Rai. Nukuu kutoka kichwani mwake na si kile nilichoandika.
Nikamwandikia mhariri wa gazeti lile kumwomba kiungwana afanye mambo mawili; mosi, aniombe radhi kwa kuchapa taarifa ya kuniomba radhi ukurasa wa mbele wa gazeti lake katika matoleo matano mfululizo. Pili, achapishe makala halisi niliyoiandika katika Rai.
Kwamba asingefanya hivyo, basi, ningefikiria hatua zaidi za kuchukua. Mhariri alinielewa na akatekeleza ombi langu hilo.
Hoja hapa ni kwa nini tunatakiwa kuwa waangalifu katika kuandika na kutamka mambo ambayo kimsingi yanaweza kuwaletea wengine madhara, ya kijamii au hata kiuchumi. Pamoja na mimi kuombwa radhi mara tano na gazeti lile, bado naamini kuwa kuna Wahehe wa Iringa waliosoma makala ile potofu na hawakusoma kingine tena baada ya hapo. Kwao, mimi nabaki kuwa ni yule mchochezi na niliyewadharau Wahehe. Itabaki hivyo daima. Ni hasara kwangu.
Mi nafikiri katika wakati huu mijadala kama hii ina umuhimu. Aliyetuhumiwa na kuhukumiwa pale Mwembetogwa ni mtu mdogo sana katika nchi hii. Amehukumiwa hadharani na mgombea urais bila kupewa nafasi ya kujitetea. Labda habari zake ndio kwanza mnazisoma humu.
Nafikiri ni muhimu hata hao tunaokwenda kuwachagua nao wajue tunafikiri nini juu yao, maana wanakwenda kubeba dhamana kubwa. Kwa kufanya hivyo, tutawapa nafasi ya kutafakari yale ambayo huenda wasingeyatafakari kama si kuibuliwa mijadala kama hii. Mimi sitachoka kuanzisha mada na kuchokoza mijadala, kwa staili hii hii, na ni kuhusu mambo mbali mbali ninayoyatafakari ili tutafakari pamoja.