Ndugu Zangu,
Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.
.
Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.
CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....
Maggid,
Iringa.
He deserved that!! huyo ndio Slaa, anafichua mafisadi, and Thats the way those kind of people are supposed to be treated.
You are suggesting that he was supposed to be treated in a CCM way!! No my friend. Slaa Hayuko hivyo. huwa anawataja hadharani baba.
Kaa mkao wa kula baba. Slaa ndiye rais ajaye mkuu. Katika kipindi chake cha miaka mitano atabadilisha wengi, ukiwemo wewe!!
mAGID NI KILAZA WA FIKRA, Mtu alielelewa katika maisha ambayo hayana upendo , nasema hivi kwasababu moja kubwa.
ukilelewa katika upendo , hutishwi ukisema ukweli nyumbani, unasikilizwa na kuelimishwa, inakujenga kuwa Imara na mtu asie muoga.
Maggid amekulia kwenye maisha ya vitisho, hakupewa uhuru wa kujieleza akiwa nyumbani, hakupendwa, alichapwa bila kusikilizwa, anadhani bado hata leo akisema hali halisi anayoiona katika rangi zake atasutwa, atatiwa rumande, anadhani tunaishi karne ya 18, anamtazamo zalili dhidi yake binafsi.
mawazo yake dhaifu mno. amepelekee makamba na Kingunge wakasome ulimbukeni wa mawazo huu.
We mkali aisee, unajua yote haya lakini huna busara, hutaki, hupendi au huwezi kuvumilia kutofautiana, unaweza kuwa na mtazamo dhalili dhidi ya nafsi yako bila wewe kujua:A S 112:.
"Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule."
Maggid, wewe ni MNAFIKI. Ingawa unalalamika kwamba watu wanakushambulia unapoleta uchambuzi wako, mi sasa nakubaliana nao kwa sababu uko biased sana kwenye makala zako. Kuna mambo mangapi ya kejeli, dharau, utumbo, uvunjifu wa sheria, ambayo yamefanywa na Kikwete kwenye kampeni hizi na haujasema lolote?!
Umeamua kumwandama Slaa kwa sababu zako mwenyewe na unataka kuwaaminisha watu kuwa una nia nzuri! Huo ni UNAFIKI. Nimechukizwa, siyo na wewe personally, bali na tabia yako ya kujifanya mkweli wakati siyo.
Brother, you gotta be honest. Just be Crystal clear that you don't like Dr Slaa, you don't want him to win, and all you are doing is trying to pull him down. Don't pretend that you are offering good advice while you're digging him. Bot hypocrisy and pretense are immoral.
Acha hizo, Get REAL.
AMA ? wewe unaweza sana kuvumilia, , ccm na makada wake WANATAKA KUTUFUNDISHA NAMNA YA Kuendesha chama cha siasa, wanataka tufanane na chama chao cha Majambazi >? kamwe ccm hawawezi kutufundisha Uwazi na Ukwelim pamoja na uongozi.
Fikra zao dhalili zimelifikisha Taifa hapa, Taifa la manyang'au, Taifa la watu MDEBWEDO KAMA MAGGID, haiwezekani mtu kala Rushwa ,, asikemewe hadhalani, kisha tusubiri vikao vya chama, vya nini ? mwizi ni mwizi tu, mlafi ni mlafi.
CHADEMA inakataa ushauri wa kubembeleza watu wa hovyo hovyo katika maswala mazito ya Kitaifa,
AMA MWAMBIE MJENGWA AKAWASHAURI MAFISADI JUU YA UENDESHAJI WA CHAMA CHAO.
Ndugu Zangu,
Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.
huyu ni yule majid wa ccm au ? hutupati ng'o. eti hawajui ofisi za chadema. sisi tunataka mabadiliko tutamchagua dr Slaa. habari za chama chake hatuna mpango nazo. mi nakaa karibu kabis na ofisi za chadema makao makuu lakini .lakini sijawahi hata kutia mguu pale wala kuomba kadi yao ila kura yangu ni kwa Dr.slaa
Wapenda chapati wewe!!! eeeh!
Haya bana! Ina maana JK anweza kuwapa shavu la U-DC watu kama hawa!!! Wapendao chai na pilau, siju nn!!!
Pamoja na yote uliyoaandika, huna uvumilivu wa kisiasa, hupendi, hutaki, hukubali kutofautiana ndio maana unapenda kuita wenzio majina.