Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

Maggid, hiyo habari ya kuogopa kudhalilishana ndiyo iliyoifikisha nchi yetu hapa. Kama wewe umeona kwamba uliyoelezea ni mapungufu basi umekosea. kwa kiasi kikubwa hiyo ni strength ya Dr Slaa kwamba hana muda wa kumwangalia mtu usoni. Anayevurunda anashughulikiwa instantly. Na huyo ndiye kiongozi tunayemtaka. Siyo kiongozi anayesema akikamata mafisadi nchi intatikisika. What a shame. Hongera Dr Slaa kwa kuonyesha ujasiri huo bila unafiki.
 
Ndugu Zangu,

Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.

.

Kama umestuliwa na kitendo cha Dr Slaa kumtaja mtu aliyepokea rushwa kuacha kutekeleza wajibu wake basi ni lazima uwe una walakini. Kitendo cha kunyamazia wala rushwa ndicho kilichotufikisha hapa. Kikwete anajua kuwa Chenge alipokea rushwa na kuna ushahidi wa wazi uliotolewa na makachero wa SFO lakini leo anampigia kampeini kama vile anakubaliana na kitendo hicho. Tunamtaka kiongozi kama Slaa ambaye hatasita kuchukulia hatua mtu yeyote anayepokea rushwa hata kama mtu huyo ni swahiba wake. Huo ndio uongozi.
 
Maggid,

ushauri wako unatokana na style yenu ccm kuoneana aibu hata kama mtu amekosea kiasi gani. Chadema wana utaratibu wao tofauti na wenu. We mwenyewe umekiri kuwa jamaa alimpigia makofi Dr. Slaa baada ya kuelezwa ukweli wake. Na kwakuwa Dr. Slaa na chadema hawapendi unafiki, wamemueleza ukweli na ameelewa makosa yake bila shaka na ndio maana bado yupo chadema, ingawa ccm hamtachelewa kwenda kumghilibu na kumnunua ili mtimize malengo yenu.
 
Maggid Mjengwa

Ninakumbuka makala zako za mwaka 2005 zikimshabikia JK lakini ungelikuwa ni muungwana angalau ungelituomba msamaha watanzania kwa kutupotosha. Hilo hujalifanya na sasa hili unatuletea ambalo ni "credit" kwa Dr. Slaa wewe unatoa tafsiri hasi! Hivi miaka mitano ya JK wewe binafsi umenufaika nini? Huko nyuma ulikwisha kuandika makala ya kiingereza kwenye gazeti le Sunday Citizen ukilaumu CCM kuwa imeshindwa kuleta elimu bora baada ya kuhudhuria mkutano wa Edward Lowassa akiwa Ni Waziri Mkuu pale chuo cha Mkwawa. Au unafikiri tumesahau? Na kichwa cha habari ulikiita "EDUCATION: QUALITY VERSUS QUANTITY". hawa CCM walikubeza lakini bado unajipendekeza kwao hebu tuume sikio kulikoni?

Maandiko yako haya kweli yananishtua mwenzetu hivi una "convenant" gani na hawa mafisadi?

Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.

CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....

Maggid,
Iringa.

Kwanza unajuaje ndani ya Chadema mtuhumiwa huyo hakupewa nafasi ya kujitetea? Wewe vile vile unafanya makosa ya kumhukumu Dr. Slaa bila ya kuwa na punje ya hata ushahidi wa kumnyima jaa yule nafasi ya kujitetea. Yaani unalaumu makosa ambayo wewe unaona una kibali cha kuyatenda. Hicho kibali mwenzetu umekitoa wapi?

Dr. Slaa anachofanya ni kuwahakikishia watanzania kuwa serikali yake itakapokuwa madarakani kutakuwa na "Zero tolerance on graft" badala ya kufurahia mwenzetu una majonzi hivi tukueleweje? Hayo unayoyazungumza JK amejaribu na matunda yake sote tunayaona. Rushwa ndiyo mtaji wa kisiasa kwa CCM...............Usiri na kutunziana heshima ndiko kumeifikisha CCM hapo ilipo..........FISADI HAJALI FAMILIA ZA WENZIE SASA KWANINI TUMWONEE HURUMA YEYE AU FAMILIA YAKE?
 
He deserved that!! huyo ndio Slaa, anafichua mafisadi, and Thats the way those kind of people are supposed to be treated.
You are suggesting that he was supposed to be treated in a CCM way!! No my friend. Slaa Hayuko hivyo. huwa anawataja hadharani baba.
Kaa mkao wa kula baba. Slaa ndiye rais ajaye mkuu. Katika kipindi chake cha miaka mitano atabadilisha wengi, ukiwemo wewe!!

Mkuu hapo unanifanya nicheke tena
 
mAGID NI KILAZA WA FIKRA, Mtu alielelewa katika maisha ambayo hayana upendo , nasema hivi kwasababu moja kubwa.
ukilelewa katika upendo , hutishwi ukisema ukweli nyumbani, unasikilizwa na kuelimishwa, inakujenga kuwa Imara na mtu asie muoga.
Maggid amekulia kwenye maisha ya vitisho, hakupewa uhuru wa kujieleza akiwa nyumbani, hakupendwa, alichapwa bila kusikilizwa, anadhani bado hata leo akisema hali halisi anayoiona katika rangi zake atasutwa, atatiwa rumande, anadhani tunaishi karne ya 18, anamtazamo zalili dhidi yake binafsi.

mawazo yake dhaifu mno. amepelekee makamba na Kingunge wakasome ulimbukeni wa mawazo huu.

We mkali aisee, unajua yote haya lakini huna busara, hutaki, hupendi au huwezi kuvumilia kutofautiana, unaweza kuwa na mtazamo dhalili dhidi ya nafsi yako bila wewe kujua:A S 112:.
 
Maggid,

Tofauti na wewe mimi nataka kumpongeza Dr. Slaa kwa kuwa muwazi (kama anayosema ni kweli). Siwezi kutaka mambo ya aibu kama uongozi kuhongwa yamalizwe vikaoni, wananchi wana haki ya kujua uongozi wao ukoje, na kwa kusema haya hadharani CHADEMA inaweza kusema inaleta uongozi wa uwazi zaidi kuliko CCM. Haya mambo ya kulindana na kumaliza mambo vikaoni ni mambo ya CCM tunayoyakataa kila siku. Kwa hiyo hili la kumsema mtu aliyechukua hongo hadharani si la kuonea haya na kumsema Dr. Slaa, actually ni jambo la sifa na kujivunia kwa CHADEMA na Dr. Slaa.

Hivi kweli unataka kuendeleza usiri na kulindana eti tu kwa sababu ya kutomdhalilisha mtu ambaye ni dhalili tayari ? Tutalindana mpaka lini? Naelewa kuna swala la political expediency, kwamba it is convenient to air this sucker out right now, but the central question should be, is it true or not ? If the allegations are true then Slaa is justified. Tunataka uongozi unaotuonyesha hata mapungufu yake, sio kufanya vyama vya siasa kama dini, havikosei.

Kama kuna kitu ninachoweza kuwasema vibaya CHADEMA ni ukweli kwamba wana viongozi wa ajabu ajabu wengi wa aina hii wanaoweza kurubuniwa kirahisi.Chama kinachoshindwa kuwa na uongozi thabiti na unaochujwa kwa makini kiasi cha kuweza kuji organize kwenye chaguzi kinanipa mashaka kama kinaweza kuendesha nchi.
 
Majjid nimefurahi sana kwa maelezo yako na nimetambua kuwa wewe ni mmoja kati ya watu ambao mmemezwa na roho ya kuficha mambo ambayo nanarudisha nyuma maendeleo na demokrasia kwa ujumla.
Katika nchi hii suala la uwazi ni jambo ambalo lipo nyuma sana na ndio maana wananchi bado ni masikini kwa kuwa hawajui kodi yao inayokatwa iwe kwenye mazao,biashara na hata kazi hawajui inatumikaje,laiti kama kungekuwa na uwazi katika mambo ya msingi basi tungekuwa mbali.
Turudi kwenye hoja,suala la mtu kusemwa wazi kwa jambo au kitu fulani hasa kama ametenda na inajulikana wazi hakuna haja ya kusubiri mpaka kwenye vikao bali ni kusema wazi ili watu waelewe kinachoendelea,kwa muungwana inabidi upige makofi tu hata kama unaumia kiasi gani maana kama jambo umefanya huwezi kutegemea watu makini na wasiopenda kufumbia mambo muhimu kukaa kimya.
 
Ndinani, Mbona maneno makali kwa mchangiaji mwenzio? amefanya alivyoweza, bila kujali individual political inclination (JF ni ya wote wenye mapenzi mema na Tanzania) na kama unafikiri analysis yake ina mapungufu na ungeweza kuongezea vitu fulani fulani, si uongezee tu? ndiyo maana na madhumuni ya JF. Let's all give positive and constructive criticisms that deal with issues and not cotributors contributors.

Big up Mjengwa and keep up the good work!

CHAGUA MABADILIKO, Chagua CHADEMA, Chagua Doctor wa ki kweli kweli: Dr Slaa
 
We mkali aisee, unajua yote haya lakini huna busara, hutaki, hupendi au huwezi kuvumilia kutofautiana, unaweza kuwa na mtazamo dhalili dhidi ya nafsi yako bila wewe kujua:A S 112:.

AMA ? wewe unaweza sana kuvumilia, , ccm na makada wake WANATAKA KUTUFUNDISHA NAMNA YA Kuendesha chama cha siasa, wanataka tufanane na chama chao cha Majambazi >? kamwe ccm hawawezi kutufundisha Uwazi na Ukwelim pamoja na uongozi.
Fikra zao dhalili zimelifikisha Taifa hapa, Taifa la manyang'au, Taifa la watu MDEBWEDO KAMA MAGGID, haiwezekani mtu kala Rushwa ,, asikemewe hadhalani, kisha tusubiri vikao vya chama, vya nini ? mwizi ni mwizi tu, mlafi ni mlafi.
CHADEMA inakataa ushauri wa kubembeleza watu wa hovyo hovyo katika maswala mazito ya Kitaifa,
AMA MWAMBIE MJENGWA AKAWASHAURI MAFISADI JUU YA UENDESHAJI WA CHAMA CHAO.
 
"Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule."

Maggid, wewe ni MNAFIKI. Ingawa unalalamika kwamba watu wanakushambulia unapoleta uchambuzi wako, mi sasa nakubaliana nao kwa sababu uko biased sana kwenye makala zako. Kuna mambo mangapi ya kejeli, dharau, utumbo, uvunjifu wa sheria, ambayo yamefanywa na Kikwete kwenye kampeni hizi na haujasema lolote?!
Umeamua kumwandama Slaa kwa sababu zako mwenyewe na unataka kuwaaminisha watu kuwa una nia nzuri! Huo ni UNAFIKI. Nimechukizwa, siyo na wewe personally, bali na tabia yako ya kujifanya mkweli wakati siyo.
Brother, you gotta be honest. Just be Crystal clear that you don't like Dr Slaa, you don't want him to win, and all you are doing is trying to pull him down. Don't pretend that you are offering good advice while you're digging him. Bot hypocrisy and pretense are immoral.
Acha hizo, Get REAL.
 
Mganga njaa tu huyu,anataka apate jina kupitia hapa. Kamshauri mwenzako michuzi kiblog chake kinakufa kule
 
Sishangai sana maana ni hivi majuzi tu huyu jamaa alikuwa ananunua makala zinazoandikwa na vijana wa sekondari na vyuoni kwa tshs 50,000/= kwa makala moja halafu anazitoa magazetini.
Sasa kama hii kaandika yeye sijui au bado wanamwandikia na yeye ananunua...kazi ipo!
 
"Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule."

Maggid, wewe ni MNAFIKI. Ingawa unalalamika kwamba watu wanakushambulia unapoleta uchambuzi wako, mi sasa nakubaliana nao kwa sababu uko biased sana kwenye makala zako. Kuna mambo mangapi ya kejeli, dharau, utumbo, uvunjifu wa sheria, ambayo yamefanywa na Kikwete kwenye kampeni hizi na haujasema lolote?!
Umeamua kumwandama Slaa kwa sababu zako mwenyewe na unataka kuwaaminisha watu kuwa una nia nzuri! Huo ni UNAFIKI. Nimechukizwa, siyo na wewe personally, bali na tabia yako ya kujifanya mkweli wakati siyo.
Brother, you gotta be honest. Just be Crystal clear that you don't like Dr Slaa, you don't want him to win, and all you are doing is trying to pull him down. Don't pretend that you are offering good advice while you're digging him. Bot hypocrisy and pretense are immoral.
Acha hizo, Get REAL.

Kuna kosa gani kuwa biased?

Kuna wanaopenda Kikwete, wako Biased kwake! Kuna wanaopenda Slaa, wako biased kwake, kuna wanaopenda Lipumba, na wanasiasa wengine. Ka kutake side ni unafiki, basi nawe umo kwenye hilo kundi la wanafiki alilomo Maggid:argue:
 
AMA ? wewe unaweza sana kuvumilia, , ccm na makada wake WANATAKA KUTUFUNDISHA NAMNA YA Kuendesha chama cha siasa, wanataka tufanane na chama chao cha Majambazi >? kamwe ccm hawawezi kutufundisha Uwazi na Ukwelim pamoja na uongozi.
Fikra zao dhalili zimelifikisha Taifa hapa, Taifa la manyang'au, Taifa la watu MDEBWEDO KAMA MAGGID, haiwezekani mtu kala Rushwa ,, asikemewe hadhalani, kisha tusubiri vikao vya chama, vya nini ? mwizi ni mwizi tu, mlafi ni mlafi.
CHADEMA inakataa ushauri wa kubembeleza watu wa hovyo hovyo katika maswala mazito ya Kitaifa,
AMA MWAMBIE MJENGWA AKAWASHAURI MAFISADI JUU YA UENDESHAJI WA CHAMA CHAO.

Pamoja na yote uliyoaandika, huna uvumilivu wa kisiasa, hupendi, hutaki, hukubali kutofautiana ndio maana unapenda kuita wenzio majina.
 
Ndugu Zangu,

Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.

Hebu tuambie unaichukuliaje ile list ya Mwembe-yanga? Kulikuwa pia na uwezekano wa kutafuta vikao vya kuiongelea ile list! Kwenye thread yako iliyopita ulimalizia kwa kusema tuweke MASLAHI YA TAIFA mbele. Labda utuambia maslahi ya taifa ni pamoja na kulindana?
 
huyu ni yule majid wa ccm au ? hutupati ng'o. eti hawajui ofisi za chadema. sisi tunataka mabadiliko tutamchagua dr Slaa. habari za chama chake hatuna mpango nazo. mi nakaa karibu kabis na ofisi za chadema makao makuu lakini .lakini sijawahi hata kutia mguu pale wala kuomba kadi yao ila kura yangu ni kwa Dr.slaa

DU.....
 
Maggid umetumwa na nani wewe mbona unadanganyika kirahisi hivyo akili mukichwa baba..sasa ulitaka Dr. Slaa aseme 'Well done' kwa huyo kiongozi mbona habari zako zinaenda kinyume nyume.. We bana kaendelee kunywa chai na chapati hapa unalikoroga kwa raha zako utawachukia watu bure weh! haya weh! Mbona JK hutuba zake huzichambui au yeye anazungumza mazuri tu hana mabaya wewe nawe umefulia kweli kweli halafu unajidai leo TUMJADILI LIPUMBA MJADILI MWENYEWE NA FIKRA ZAKO...watu wengi mnatupa hasira
 
Pamoja na yote uliyoaandika, huna uvumilivu wa kisiasa, hupendi, hutaki, hukubali kutofautiana ndio maana unapenda kuita wenzio majina.

AMA, unadhani kwakua kunakundi la waandishi uchwara wanaweza kuyumbisha adhma ya mabadiliko ya WaTz wamepotea, huyu anajaribu kucheza na msukumo wa fikra sahihi za mabadiliko katika Taifa hili, kwa zaidi ya miezi 3 , amekua akiandika fikra zako rojorojo juu ya mageuzi na wanamageuzi, kwa wiki mbili hizi ameamua kuishanvbulia CHADEMA, na akae akijua na najua anasoma mawazo haya, kuwa, HATUDANGANYIKI LABDA AKAMWAMBIE KINGUNGE NA MAKAMBA MAWAZO JUU YAKE JUU YA KUENDESHA CHAMA NA SERA ZAKO MDEBWEDO JUU YA UKWELI NA UWAZI.
 
Back
Top Bottom