Kilichonivutia kwa uchunguzi wa polisi juu ya Hamza

Kilichonivutia kwa uchunguzi wa polisi juu ya Hamza

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Kwa mara ya Kwanza polisi wetu wameweza kuchunguza kwa haraka zaidi na kwa muda mfupi mno na kupataa majibu mengi juu ya gaidi Hamza. Kuwa alijifunza Ugaidi mtandaoni, aliishi kwa Siri na kuwa alikuwa ni gaidi wa kidini, Imani kali.

Polisi wetu wameweza kufanya uchunguzi huku gaidi Hamza akiwa amekwisha kufa. Hicho kipengele ndio kilichonivutia zaidi.

Nadhani ni polisi hawa hawa walioshindwa kuchunguza tukio la watu waliopania na kukusudia kumuua Tundu Lissu. Walishindwa kuchunguza kwa sababu walizozitoa wao kuwa Dereva wa Lissu hayupo iko kutoa ushirikiano wa kuhojiwa, wakati huo Lissu akiwa hospitali za Nairobi na Belgium akiondolewa risasi na matibabu mengine.

Kama Hamza kafa na wameweza kupata taarifa zake za matendo yake ya Ugaidi, Walishindwaje kupata taarifa za Waliotaka kumuua Lissu bila na Dereva na Lissu kuwepo? Lakini wakiwa hai?

Nachojua Mimi Serikali za Kenya na Ubelgiji zingeombwa na polisi wetu kwenda kuwahoji Lissu na Dereva zisingekataa. Nawasifu polisi wetu kuchunguza kwa haraka na kupata majibu ya gaidi Hamza wakati akiwa amekwisha kufa.
 
Sababu ya polisi wetu uchunguzi wao kubarikiwa kubata majibu mapema ni kwasababu suala la Hamza lilikua limewakamata pabaya, ndio maana ili kujinasua kwa minogono kwa ile minogono ya mitandaoni kuwa tukio linatokana na Hamza kuzulumiwa na wao, basi ikaonekana Hamza awe gaidi na amepata mafunzo kupitia mitandao ya kijamii
 
Tukubali yaishe na tuendelee na mengine,hakuna umuhimu wa kulumbana.
Tunatakiwa kuwatwii walioko madarakani,mengine tumuachie aliye umba mbingu na nchi.
 
Back
Top Bottom