Kilichotekea Geita Gold FC ni ushamba tu

Kilichotekea Geita Gold FC ni ushamba tu

Nope, ni ya Halimashauri GGM ni wadhamini
basi siasa ishaanza ,itakuja kuwa kama Singida United,wakianza kupambana wasishuke daraja na siyo kupambana ubingwa na nafasi za kimataifa basi ujue hamna kitu tena ,Yale yale ya KMC na Dodoma Jiji
 
Vitu usivyovijua ni bora unyamaze, hiyo ni nyumba ya jirani ina siri nyingi tulia mkuu.
Unataka mtu aingie kambini bila mkataba?
tatizo mnasoma halafu hamjielewi. Ndiyo maana kasema Mambo km hayo ndiyo yanaigharimu timu.

Hili Jukwaa la michezo kila MTU ana Uhuru wa KUWEKA mtazamo wake au Jambo lolote la kimichezo kuhabarisha wengine.
 
Mpaka ligi inaanza bado watu wanasikika hawapo kambini.

Ilianzia kwa kocha Minziro, wenzao wanawatambulisha wachezaji kwa maana ya kujiandaa kwa ligi, ikasemekana yupo Dar na hajasaini mkataba wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Jana tu ikasikika mchezaji G. Mpole hayupo kambini na akasikika anasubiri mkataba mpya au kujiunga na timu nyengine. Wakati akihojiwa alikuwa kwake Mbeya.

Hapa ndio natatizwa kwani timu hii inatuwakilisha kimataifa yaani mashindano ya CAF.

Sasa ni aidha kocha Minziro na mchezaji G. Mpole wamelewa sifa na kuanza kudai pesa nyingi ya kulipwa na klabu au uongozi kimpira hawako makini.

Ndio maana nawafananisha na USHAMBA tu walichokifanya.
Hayo yote yalikua na mauongo ili kuwaingiza Simba Chaka, mbinu za kishamba kwel
 
Kuhusu Minziro ni kosa la Geita GFC kudhani wangepata kocha bora zaidi yake kwa bei nafuu na mission imebuma.

George Mpole baada ya kuwa mfungaji bora akawehuka. Simba walipomhitaji akawatajia bei ya Sadio Mane wakamgeukia Habib Kyombo.
Ndio maana Leo alikuwa na hasira
 
Back
Top Bottom