Kila mahali we ni kumponda Mungu tuu, hujaona hoja kuu ya mleta mada.
Mkuu,
Ukichofanya hapa ni logical fallacy. Kilatini inaitwa "ad hominem ". Yani, umeshindwa kujibu hoja ya mtu, unaiacha hoja, unamshambulia mtu.
Mara nyingi hii hufanywa na mtu asiye na hoja ya kujibu hoja, anakimbilia kumkashifu mtoa hoja, bila ya kuigusa hoja.
Hoja ya imani ya Mungu ni mtambuka.
Mimi sikuileta hoja hii, mtoa mada kaitaja. Na kaitaja kwa sababu huko kwetu ipo katikati ya kila kitu. Haikwepeki.
Mimi sikuanzisha habari za Mungu katika thread ambayo haijamtaja Mungu. Nimeangazia tu habari ya Mungu ambayo ilishaletwa na mtoa mada.
Yani badala ya kuangalia Geological Survey Mwanza kuna uwezekano wa kuwa na tetemeko la ardhi kubwa kiasi gani, kila baada ya miaka gani, na likitokea, yale mawe yatadondoka vipi, na yakidondoka tutajikinga vipi, tunasema tumuombe Mungu ambaye hayupo atuepushe na majanga!
Sasa mbona humshambulii mtoa mada kwamba nyie mbona kila kitu mnamuweka Mungu, unanishambulia mimi kwa kusema habari za Mungu ni upuuzi tu?
Huoni kwamba una selective and convenient outrage, kwa mtu ambaye yuko against worldview yako tu?
Mtu anaweza kuona hili hapa jiwe nikijenga hapa ni hatari sana, lakini akaamua kujenga bila hata kupata ushauri wa wataalamu, kwa kuamini tu "Mungu atanilinda".
Ndivyo majanga nengi yanavyotokea hivyo, kutojali usalama katika vyombo vya usafiri, katika kujenga, katika mambo mengi sana.
Sasa, katika utamaduni kama huu wa kuishi kwa kudra za Mungu, kulitazama hili suala la uwepo wa Mungu ni muhimu sana.
Kwa sababu, kama kweli huyo Mungu hayupo, na watu hawataki kujua hilo, ni muhimu angalau wajue kuwa huyo Mungu hayupo na wanapochujua risk ya kujenga ovyo, kuna siku linaweza kutokea janga, wakaumia au kufa, wasije kufikiri kumuomba Mungu kutawasaidia.
Tubishane kwenye facts. Mungu yupo au hayupo?
Kama unaweza kuthibitisha yupo, halafu mimi nasema uongo, hapo unaweza kuwa na point ya kunishambulia.
Lakini, wewe hujaweza kukanusha kile ninachokisema, unakuja kunifanyia censorship? Unanifunga mdomo nisitoe maoni yangu kwa uhuru? Hapa JF ambapo tunasema "We Dare to Talk Openly"?
Pinga hoja kwa hoja, usitake kunyamazisha watu wasitoe maoni yao.