DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Kinyang'anyiro cha kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusaka Wagombea Ubunge, uwakilishi na udiwani kilichofanyika nchini kote Agosti 4, 2025, kimefichua hatari kubwa inayokikabili chama hicho kikongwe ambayo kama haitadhibitiwa haraka basi kinaweza kuleta shida.
Uchunguzi uliofanywa katika Jimbo la Msalala, Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga umebaini kushamiri na kukomaa kwa vitendo vya rushwa baina ya wagombea au watia nia na wajumbe wapiga kura, ambapo sasa vitendo hivyo vinafanyika wazi wazi kama zinavyofanyika biashara zingine halali.
Mwandishi wa habari hizi aliyepiga kambi jimboni humo usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura za maoni alishuhudia wagombea na wapambe wao wakipishana kugawa fedha kwa wajumbe bila woga, huku wajumbe wenyewe wakiwasaka wagombea kwa udi na uvumba na kudiriki kukesha usiku wakiwasubiria ili wawaletee mgawo wao.
Wapiga kura wa Jimbo la Msalala walikuwa wamepanga bei ya kura zao kama inavyofanyika kwenye biashara sokoni au gulioni, ambapo inadaiwa kura moja iliuzwa kuanzia shilingi 30,000 au 40000 au 50,000, mpaka 100,000.
Kwa hiyo, mazingira hayo yaliwanufaisha watia nia matajiri, na kuwaathiri watia nia wenye mkono wa birika (wasiotaka kutoa) na wale wenye fedha kiduchu ambao hawakuwa na ubavu wa kushindana kununua wapiga kura.
Watia nia walioongoza kura za maoni katika jimbo hilo ni Mabula Magangila, aliyeshika nafasi ya kwanza kwa kujikusanyia kura 5518, akifuatiwa na Ambrose Nakale aliyejikingia kura 929, na katika nafasi ya tatu alikuwa Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige aliyepata kura 791. Maige pia amewahi kuliongoza jimbo hilo kuanzia Mwaka 2005 mpaka 2020.
Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia mtia nia mmoja miongoni mwa hao watatu akiwa anagawa fedha kwa mkono wake mwenyewe kwa wajumbe wa Kata ya Segese akisaidiana na mmoja wa aliyekuwa Diwani wa kata hiyo.
Baadaye alikamatwa na TAKUKURU kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, huku swahiba wake anbaye ni miongoni mwa watia nia watatu waliotajwa hapo juu akiponea chupuchupu kunaswa.
Mtia nia huyo anadaiwa kununua kura kwa bei ya kati ya shilingi 30,000 mpaka 100,000 huku mzigo huo wa fedha ukielekezwa katika kata zenye wapiga kura wengi ili kujihakikishia ushindi dhidi ya wapinzani wake.
“Yaani hapa hapakuwa na uchaguzi bali kulikuwa na mnada wa kura, hapa kura zilinadiwa na mwenye fedha zake ndiye alipigiwa kura. Ni kama tulikuwa gulioni, lakini hapakuwa na biashara nyingine zaidi ya kura, kwa hiyo lilikuwa gulio la kura hapa Msalala siyo uchaguzi”, alisema mjumbe mmoja kutoka kata ya Segese.
Imeelezwa kwamba kata zilizonufaika zaidi ni Bulyanhulu na Bugalama ambako inadaiwa wapiga kura wake walilipwa shilingi 100,000 kila mmoja, huku wajumbe wa Kata za Segese, Mega, Bulige, na Kashishi inadaiwa walilipwa shilingi 50,000 kila mmoja.
Aidha, Kata za Busangi na Ngaya wajumbe wake walilipwa shilingi 40,000 kila mmoja ili kuwashawishi kumpigia kura mtia nia huyo ambaye inaelezwa anatoka kwenye familia yenye uwezo mkubwa kiuchumi.
Inadaiwa kuwa mtoa rushwa huyo aliweka mkakati madhubuti wa kuwadhibiti wajumbe aliowanunua ili wasimgeuke, ambapo inaelezwa aliwalipa nusu ya fedha alizowaahidi wanapokwenda kupiga kura na kuwamalizia nusu nyingine baada ya kupiga kura na kuthibitika kuwa kura zao walimpigia mtia nia huyo.
“Huyu jamaa (jina lake kapuni) kwa kweli alijipanga kuhakikisha pesa yake haiendi bure, inadaiwa alimlipa kila mjumbe kiasi cha shilingi 20,000 wakati anakwenda kupiga kura kituoni na kumalizia kiasi cha fedha kilichobaki baada ya kupiga kura”, alibainisha mjumbe kutoka kata ya Busangi.
Aliongeza kuwa “Wapiga kura wote waliopewa fedha na mtia nia huyo walipewa maelekezo kwamba wakifika kwenye vituo vya kupigia kura wajifanye hawajui kusoma na kuandika na hivyo kuomba usaidizi, kisha kusaidiwa na watu waliokuwa wameandaliwa na mtia nia huyo”, alifafanua mjumbe huyo.
Vitendo hivi vinakwenda kinyume cha miiko na kanuni za uchaguzi za CCM zinazopga marufuku vitendo hivyo. Aidha, vitendo hivyo vinakiuka maonyo na makatazo ya viongozi wakuu wa CCM ambao wakati wote wamekuwa wakikemea vikali rushwa katika chaguzi za chama hicho.
Viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wazi kushughulikia tatizo la rushwa kwenye kura za maoni ambapo mara kwa mara wamesikika wakisema wazi na kwa msisitizo mkubwa kwamba hawatasita hata kwa sekunde moja kuwaondoa kwenye kinyang’anyiro wana CCM wanaotumia rushwa kushawishi wapiga kura katika chaguzi mbalimbali za chama hicho, ikiwemo chaguzi za kutafuta wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani.