Kilichotokea Mtwara ni sampuli tu uonevu wa jeshi la polisi kwa raia, matukio mengi huwa yanafichwa. Mabadiliko makubwa yanatakiwa kwa nchi nzima

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Kisingizio kikubwa huwa ni kudhibiti uhalifu kwa kisingizio cha kupambana na wahalifu wasiotii bila shuruti.

Utasikia alikuwa ni mhalifu na hata ndugu wasio na uwezo wakifuatilia matukio ya ndugu zao kupoteza maisha au kuumia wakiwa mikononi mwa polisi huwa hawapati ushirikiano wowote.

Namna ya jeshi la polisi lilipofikia kwa sasa na malamiko dhidi ya uonevu unaofanywa na polisi dhidi ya raia ni wazi kuwa sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa.
 
Ndio wananchi tuamke sasa, tatizo sisi tumekaa kama mapunguwani, la sivyo watatupelekesha saana hawa UMBWA.
 
Inatakiwa pia kuundwe timu ya kuchunguza mkasa wa tukio na kifo cha Hamza.
 
Kuna wimbo mrisho mpoto alisema, "lilikuwa linapambana na polisi tukalishinda"
 
Kisingizio kikubwa huwa ni kudhibiti uhalifu kwa kisingizio cha kupambana na wahalifu wasiotii bila shuruti.

Utasikia alikuwa ni mhalifu na hata ndugu wasio na uwezo wakifuatilia matukio ya ndugu zao kupoteza maisha au kuumia wakiwa mikononi mwa polisi huwa hawapati ushirikiano wowote.

Namna ya jeshi la polisi lilipofikia kwa sasa na malamiko dhidi ya uonevu unaofanywa na polisi dhidi ya raia ni wazi kuwa sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa.
Naunga mkono. Polisi si sehemu ya kutafuta haki yako bali ni sehemu ya kukamuliwa pesa.
 
Hayo mabadiliko yaanzie kwa nani? wanasiasa? NO.

Mabadiliko ya kweli yataanzia kwetu wananchi, tuondoe udhalimu wote uliotuzunguka polisi ni sehemu tu ya udhalimu wenyewe, lakini wanasiasa wenye uchu wa madaraka wasiokubali kushindwa ndio dhalimu namba moja.

Bora tuanze kwanza kuwaondoa hawa wanasiasa wanaowatumia polisi kwa manufaa yao binafsi halafu tukimaliza ndio tulifanyie ukarabati wa hali ya juu jeshi la polisi, lisiwe tena na dalili za uwanasiasa.
 
Hayo mabadiliko yaanzie kwa nani? wanasiasa NO.

Mabadiliko ya kweli yataanzia kwetu wananchi, tuondoe udhalimu wote uliotuzunguka polisi ni sehemu tu ya udhalimu wenyewe, lakini wanasiasa wenye uchu wa madaraka wasiokubali kushindwa ndio dhalimu namba moja.
Wananchi tufanye nini sasa?
 
Hamza!Hamza!na wengine wote walodhulumiwa uhai wao Mungu awarehemu huko mlipo
 
Kisingizio kikubwa huwa ni kudhibiti uhalifu kwa kisingizio cha kupambana na wahalifu wasiotii bila shuruti.

Utasikia alikuwa ni mhalifu na hata ndugu wasio na uwezo wakifuatilia matukio ya ndugu zao kupoteza maisha au kuumia wakiwa mikononi mwa polisi huwa hawapati ushirikiano wowote.

Namna ya jeshi la polisi lilipofikia kwa sasa na malamiko dhidi ya uonevu unaofanywa na polisi dhidi ya raia ni wazi kuwa sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa.
"askari mwenye kiapo anawezaje kupora hela halali za mwananchi na kisha kumuua,hawa bado tunawaita walinda usalama"
 
Wapelekwe jeshini halafu wale wa jeshi waje kukaimu nafasi za upolisi kwa muda tuone matokeo
 
Back
Top Bottom