Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Taarifa za Damascus kuanguka mikononi mwa waasi zikiwa zinaendelea kusambaa na kusubiria kuthibitishwa rasmi wengi wameshangazwa na waasi wa Syria kuweza kufanikiwa kirahisi na kwa haraka sana dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad
Hapa tunajifunza kwa vitendo pia kwamba majeshi ya Urusi, Iran na Hezbollah yaliyokuwa tegemeo kuu la Assad yameshindwa vibaya kumlinda na kumtegemeza mshirika wao muhimu.
Inaonekana Urusi hawezi kupigana vita katika front nyingi, Ukraine imemtoa upepo na bado inaendelea kumtoa jasho hadi anapoteza focus kwingine. Iran na Hezbollah wametikisiwa kidogo na Israel wametepeta.
Kilichotokea Syria inapaswa kuwa aibu kubwa kwa linalodiwa taifa kubwa la Urusi, mshirika wao amepigwa wakiwepo. Afghanistan ilianguka mikononi mwa Taliban baada ya Marekani kuondoka, Vietnam ilianguka mikononi mwa Viet Cong baada ya Marekani kuondoka. Syria imeanguka mikononi mwa waasi Warusi wakiwa wamejaa kwenye makambi yao ya kijeshi Syria wakishangaa tu waasi wanvyochukua nchi.