KIlichowaponza Yanga mechi dhidi ya Rivers united chabanika...

KIlichowaponza Yanga mechi dhidi ya Rivers united chabanika...

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
  1. Maandalizi hafifu ndani ya uwanja huku nguvu kubwa ikiwekwa katika kutimiza malengo ya wadhamini ambayo ni kuuuza bidhaa zao kwa kuwekeza zaidi katika njia ambazo kwao walizani zitaweza kutangaza bidhaa za Club zaidi na sio uwanjani...
  2. Vingozi wa Club Yanga kuingiliwa katika unendeshaji wa Club na wadhamini ambao malengo yao yameaninshwa hapo juu. Jambo lilozalisha matatizo mengi likiwemo swala la kushindwa kukamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji wa kigeni kwani wadhamini walichotaka wao ni kuona wachezaji wapya wanavaa uzi wa Yanga siku ya tamasah na jezi zinauzwa kwa wingi siku hiyo mengine kwao sio muhimu. Hata swala kumchukua aliyekuwa msemaji wa Club ya Simba (Aliyefurumishwa Simba) halikuwa lengo la viongozi wa Club wa Ynaga kwani walijua wazi kuwa hana tija katika Kuisadia timu uwanjani bali lilikuwa ni takwa la GSM (wadhamini) kwa ajii ya kutimiza malengo yao
NINI WANATAKIWA KUFANYA YANGA

Ni kuamua kuwekeza kwenye mpira uwanjani na kuhakikisha viongozi hawaingiliwa na mdhamini ambaye kwa bahati mbaya ana malengo tofauti kabisa na malengo ya Club na mbaya zaidi wamejishahu na ameshaweka mizizi kwene club yao.
 
Ufumbuzi wa yote ni mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ukamilike ili klabu iendeshwe kwa mfumo mpya vinginevyo Yanga itabaki hivyo hivyo milele wakati watani zao wakiendelea kuchanja mbuga. Uongozi hauna nguvu za kupinga matakwa ya mdhamini ambae kwa sasa ndio nguzo kuu ya uendeshaji wa klabu.
 
Back
Top Bottom