Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Nchi yeyote inayothamini Uhuru wake huadhimisha siku iliyopata Uhuru huo kutoka kwa wakoloni weupe au weusi kwa shangwe kuu iliyotukuka , hii ni siku ambayo nchi husika husherehekea minyororo ya utumwa kukatwa , nchi zilizopambana kupata uhuru huo kwa vita , huwakumbuka mashujaa wao waliokufa kwenye mapambano ambayo hatimaye yalileta ukombozi wa kweli , kwa kifupi siku kama hii ni siku Tukufu .
Baada ya awamu ya 5 kuingia madarakani ilikuja na mpango tofauti wa kusherehekea siku hii , sherehe na shamrashamra zilizoambatana na gwaride pamoja na halaiki vilizimwa kwa maelezo ya kuokoa pesa ili kujazia maendeleo ya nchi , ikiwemo kujenga barabara kadhaa , hospitali na shule .
Sikuwa na mgogoro wowote na jambo hili kutokana na " uzito " wa sababu zilizoelezwa na wakubwa ili kuhalalisha mpango wao wa kutoadhimisha siku hii kama ilivyozoeleka , bali kilichonishangaza ni kuona mwaka huu yakifanyika maandalizi makubwa ambayo bila shaka yametumia gharama kubwa ili kufanikisha maadhimisho haya Jijini Mwanza , ambako karibu kila kiongozi wa Taasisi kubwa ndani ya nchi hii amehudhuria , tena kwa gharama kubwa mno !
Swali langu ni hili : Je kilichokwamisha sherehe hizi miaka yote hii sasa kimetatuliwa ?
Naomba kuwasilisha .