Ukanda huo mambo hizo ni nyingi sana
Mwezi wa kwanza nilikuwa mwananyamala nilikuwa nafatilia vaccin ya corona sasa doctor alikuwa anaringa hatari ni mbibi hivi nilienda kuonana naye akanambia nimsubiri, nikaona uzushi kukaa ndani hospital... kama unapajua panapopatikana chanjo ya corona hapo mwananyamala.. nikakaa Kwa nje kuna frij na mbibi anauza soda nikaagiza mirinda nyeusi nikawa naigigida kidogo kidogo nikimsubiri doctor
Basi ndipo wakaja kusimama pembeni yangu na kuanza kuadithiana wadada watatu na kasichana kalichokuwa kanafanywa na uncle wake
Wadada wawili walimpeleka hospital huyo msichana, ni kasichana kadogo kama cha darasa la pili hivi mjomba ake alikuwa akimwingilia kila siku unaambiwa na bibi yake inasemekana anajua kama mwanae anamuingilia mjukuu wake ila hakuwa akimkalipia.. yaani ushenzi sanaa
Na hako kasichana nacho kalikuwa kanaadithia jinsi alivyokuwa anafanywa mpaka nikajisikia haibu, aisee.. na hako kasichana kanaadithia kuwa alimwambia mjomba wake kuwa atamsemea kwa mama yake ambaye hakuwa anaishi hapo.. mjomba alikuwa anamjibu.. kuwa mambo madogo kama hayo ya nini? Kwenda kumsemea
Walikuwa wanapanga watafute mwanasheria wamfunge huyo ndugu yao ila bibi ambaye ni mwanae huyo mjomba bado anamtetea na wakati imedhihirika kuwa ni kweli amefanya hilo tendo
Kisichana kiliulizwa kwann! Siku zote hausemi na unafanyiwa hivyo anasema alikuwa anatishiwa na huyo mjomba wake na ikitokea akimwambia bibi yake, bibi huwa anamkalipia na kumwambia aache uongo
Nilikaa hapo pembeni nilijisikia vibaya na haibu juu maana nilikuwa naangaliwa kana kwamba mm ndio muusika
By the way na chanjo yenyewe sikuchanja nilichoka kumsubiri doctor plus na ilee haibu nikajiondokea zangu